Maandamano haya ni ushahidi tosha kuwa 'intelijensia' ya polisi ni ya kisiasa

Teeh..HAWA JAMAA SIO WAJINGA,WANAJUA KABISA HII NCHI YAO KUANZIA VIONGOZI WAKUU WA POLISI,USALAMA,SERIKALI NA SASA WANADAI MAHAKAMA YAO YA KADHI.ANGALIA TV NA REDIO IMANI ZINAVYOFANYA ZITAKAVYO WAKAT MWANAHALIS WANAKIONA CHA MOTO...HII NCHI IMEPEWA WENYEWE MKUUU

Comment yako inadhihirisha ni jinsi gani wakristo kupitia mfumo kristo wamekuwa favoured kwa miaka 50.
 
Jana nilishangaa
nikiwa pale Magomeni naona Landcriser ya polisi inageuza halafu kuna
taharuki na maandamano yanaelekea town wakisema maneno ambayo mimi
siyajui nikafikiri wanaenda kuzika kukawa foleni kubwa lkn kufika
wanaendelea, kufika Nyerere nikakutana na kundi jingine, na hamna
askari. Ni kwanini nchi hii isiendeshwe hivyo?? Nimechoka kuwaona askari
wakiwa na silaha hata kama kuna issue ndogo na sasa nina aledge nao.
mungu atusaidie.

ni 'allergy' siyo 'aledge'!
 
Mimi ni mkristo na ninaiamini imani yangu. Bahati nzuri baba yangu wa kufikia ni muislam(RIP) na nina wadogo na kaka waislam. Kiujumla familia yetu ina mchanganyiko wa kiimani lakini ina upendo.

Baba yangu wa kufikia alikuwa mcha Mungu na alitusisitiza sana sisi kushika imani. Wakati wa mfungo wa Ramadhan tulikuwa tunafunga. Mama yangu(ni mkristo) alikuwa anajifunga mtandio kichwani mara zote anapokuwa nje. Kiujumla zile taratibu/maadili ya kidini kwa pande zote yalikuwa yanapewa kipaumbele sana.

Sasa kaka yangu Hussein(si jina lake) alikuwa China, he is one of the best intelligent guys in Tanzania. Amefungua kampuni na mawazo yake yapo kwenye kusaidia wasio na uwezo na kujiendeleza elimu dunia na dini.

Am so proud of him! Natamani matatizo ya sijui mfumo Kristo etc yatatuliwe, tuwe na upendo.

Nasoma Quran kuna mafundisho makubwa mazuri ingawa sifurahii kabisa kuniita Kafir!

Anyways wote tutakufa! Waliotangulia wanajua siri. Wewe unayesoma na mimi ninayeandika tutakufa siku fulani na tutajua yaliyofichwa!

Tupendane!

Wewe kweli mkimbizi kama jina lako.
 
Hapo ndo tujue wanazuiaga nguvu ya umma tu hakuna cha intelijensia wala nini.
Wanawaogopa sana polisi.
 
angekuwa mkapa angewaua kabisa hao kama muembe chai na zanzibar kule

Mwembechai waliuliwa 27,raid alikua mkapa na rpc Gewe!
Waislam walipolalamika wakaobekana wajinga na maaskofu wakasifia upuuzi ule.Leo tunataharuki Lyons mitaa ya jiji imejaa! Waacheni watumie uhuru wao,kesho jumapili nasi tuingie mitaani kudai igp,rpc,mkurungezi usalama na Mzee wa kaya na makamu wake tuache uvivu wa kufikiri,tusiendeshwe na fikra za udini!
 
Mi sikutaka mtu yeyote apigwe risasi wala kiuguswa!
Ninachotaka ni haki iendelee kutendeka kama ilivyo tendeka jana sio wengine wakiandamana wanapigwa risasi!





ndo yalishafanyika hayo! imebaki story! na IGP wamewa disappoint kweli.. maana mlitaka watu wapigwe risasi .. hehe! poleni sana! kazi ya polisi ni kulinda usalama na ku re store order jana waislam walikuwa wastaarabu sana , ila next time cdm mkitaka kufanya maandamano msitume msg za vitisho wala kubeba silaha



mtei ana beef na imani yangu! alilithibitisha hilo JF

 

Mi sikutaka mtu yeyote apigwe risasi wala kiuguswa!
Ninachotaka ni haki iendelee kutendeka kama ilivyo tendeka jana sio wengine wakiandamana wanapigwa risasi!

sidhani kama polisi wanpiga risasi raia kwa makusudi -

1 ) bahati mbaya

2) Maandamano yanatishia amani .." vurugu"

 
Tatzo na kuzaliwa na kua mkatoliki mnajazwa chuki za udini,,mi nko ndanda sec.cha kushangaza ndanda mission inatangaza udini hadi kwa wanafunzi sisi,,ndo maana nawaona wakristo mnaokerwa na juhudi za waislam ni wajinga tu,,kueni na upeo wa kujadili mambo ya dini yenu na si dini ya wenzenu
 
Kwa hiyo mnaolalamika humu jf mlitaka jana tupigwe mabom ili tue sawa na chama cha kanisa??acheni waislam wadai haki zao,au mlipenda waendelee kukaa sero??
 
Mimi ni mkristo na ninaiamini imani yangu. Bahati nzuri baba yangu wa kufikia ni muislam(RIP) na nina wadogo na kaka waislam. Kiujumla familia yetu ina mchanganyiko wa kiimani lakini ina upendo.

Baba yangu wa kufikia alikuwa mcha Mungu na alitusisitiza sana sisi kushika imani. Wakati wa mfungo wa Ramadhan tulikuwa tunafunga. Mama yangu(ni mkristo) alikuwa anajifunga mtandio kichwani mara zote anapokuwa nje. Kiujumla zile taratibu/maadili ya kidini kwa pande zote yalikuwa yanapewa kipaumbele sana.

Sasa kaka yangu Hussein(si jina lake) alikuwa China, he is one of the best intelligent guys in Tanzania. Amefungua kampuni na mawazo yake yapo kwenye kusaidia wasio na uwezo na kujiendeleza elimu dunia na dini.

Am so proud of him! Natamani matatizo ya sijui mfumo Kristo etc yatatuliwe, tuwe na upendo.

Nasoma Quran kuna mafundisho makubwa mazuri ingawa sifurahii kabisa kuniita Kafir!

Anyways wote tutakufa! Waliotangulia wanajua siri. Wewe unayesoma na mimi ninayeandika tutakufa siku fulani na tutajua yaliyofichwa!

Tupendane!

ni kweli! ila tatizo ni moja wakristo wanawaona waislamu kama sio watz, ilo ndo tatizo kubwa.
 
mwembechai mlivunja mabucha ya watu ya nguruwe mlidhani tuko iran hapa!!!!mbona wakristo hawaui ngamia wenu mnaokula ebo....mwembechai mkuu wa mkoa mustapha nyang'anyi(muislam),rpc dar mwindadi ali(muislam),mwinyi rais(muislam)....waliouliwa mwembechai..igp omari mahita(muislam)

kweli wewe nyabhingi wa kunyabingiwa....! umezaliwa lini? jana? alafu umekuwa kwa kudungwa masindano nini! yani hata hujui mwinyi awamu ya urais wake ulikoma mwaka gani! hata mumeo kamanda gewe pia umemsahau! yani uko empty kichwani, afu ndo unajifanya unajuuuua kumbe wewe ni juha.
 
[h=2]Waislamu wazingira Wizara ya Mambo ya Ndani Dar [/h][h=2]Dar [/h] Jumamosi, Septemba 08, 2012 08:50 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

Kurasa 1 kati ya 3
waislamu.jpg
Baadhi ya waumi wa Dini ya Kiislamu wakiswali katika Barabara ya Ghna karibu na Ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dar es Salaam jana baada ya kufanya maandamano kwa ajili ya kushinikiza kuachiwa kwa watu waliokamatwa baada ya kukataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa. Picha na Anthony Siame

*Walianza kuandamana wakitokea misikitini
*Waendesha swala mbele ya jengo la wizara
*Wataka Dk. Ndalichako ang’olewe NECTA
MAELFU ya waumini wa dini ya Kiislamu, jana walitikisa Jiji la Dar es Salaam, baada ya kuandamana na kuizingira Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, pamoja na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Pamoja na mambo mengine, waliandamana ili kupinga kukamatwa kwa wenzao waliogoma kuhesabiwa wakati wa Sensa ya Watu na Makazi inayomalizika leo.
Pia waliandamana ili Serikali imwondoe madarakani, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Joyce Ndalichako, ambaye wanamshutumu, kwamba alihusika katika kufeli kwa wanafunzi wa shule za Kiislamu, wakati wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.

Kabla maandamano hayo ya aina yake hayajaanza jana mchana, waislamu hao walianza kuhamasishana asubuhi kwa kusambaziana vipeperushi vilivyokuwa vikiwataka waandamane kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya swala ya Ijumaa.

Katika kutekeleza maandamano yao, waislamu hao walikuwa wakitokea katika misikiti waliyokuwa wakiswalia, baada ya swala hiyo ikiwamo misikiti iliyoko Kariakoo, Posta, Magomeni, Kinondoni na mingineyo.

Wakati wa maandamano hayo, mamia ya askari polisi waliokuwa na silaha za moto na magari ya kuwasha waliwasindikiza kwa amani.

Waandamanaji walibeba pia mabango mbalimbali, huku baadhi yakisomeka, Miaka 51 ya Uhuru bado tunadhulumiwa, sasa Waislamu tumechoka kunyanyaswa.

Maandamano hayo yaliongozwa na viongozi kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na miongoni mwao, alikuwapo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahadhiri wa Kiislamu nchini, Kondo Bungo.

Viongozi wengine waliokuwapo ni Rajab Katimba, Jafari Mneke pamoja na Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maandamano hayo, Muccadam Swalehe.

Baada ya kutokea katika misikiti waliyokuwa wakiswalia huku wakisindikizwa na mamia ya askari polisi, hatimaye waliwasili wizarani hapo.

Walipofika mahali hapo, viongozi wa maandamano hayo waliingia ndani ya wizara na kuwaacha wenzao wakiwa nje ya wizara hiyo.

Walipokuwa ndani ya wizara hiyo, walikutana na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakil.

Mazungumzo kati yao na Abdulwakil yalipohitimishwa baada ya saa tatu kuanzia saa 8 hadi saa 10.30 hivi, Katibu MKuu huyo alitoka nje ya ofisi yake na kuwasikiliza.

Abdulwakil, alisimama katika uwanja wa wazi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kusomewa risala na viongozi wa waandamaji hao.

Akisoma risala iliyoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Muccadam Swalehe, alisema kumekuwa na ukamataji wa Maimamu, Masheikh na waumini wa dini yao kinyume cha sheria tangu ilipoanza Sensa ya Watu na Makazi Agosti 26 mwaka huu.

“Sensa ni utaratibu wa kitaalam unaohitajika, ili kuliwezesha taifa kupata takwimu sahihi za mambo yote muhimu.

“Hata hivyo, Waislamu walitangaza msimamo wa kutaka kipengele cha dini kiingizwe katika dodoso la Sensa, sambamba na kuwepo wawakilishi wa dini zote katika ukusanyaji wa takwimu na majumuisho kwa kuundwa tume huru ya Sensa.

“Pamoja na kutoa mapendekezo hayo na kuyawasilisha Serikalini, bado Waislamu tulitoa msimamo wa kutoshiriki iwapo mambo haya hayataingizwa katika dodoso la Sensa.

“Pamoja na msimamo huu, bado Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata wanawake wa Kiislamu na kuwavua nguo na wakati mwingine, watuhumiwa kunyimwa haki ya dhamana kinyume cha sheria.

“Polisi wamekuwa wakivunja nyumba zao usiku kwa kushirikiana na maofisa wa Sensa, huku wakiwalazimisha kwa nguvu kuhesabiwa chini ya mtutu wa bunduki.

“Kwa hali hii, tunalaani vitendo vyote vya unyama na unyanyasaji vinavyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya Waislamu na tunataka vikomeshwe mara moja,” alisema Muccadam
 
ni kweli polisi hawakujua kinachoendelea?

Je walikuwa na kibali cha kufanya maandamano?

Je viongozi wao watashitakiwa kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria kama wanavyowashitaki viongozi wa vyama vya siasa?

Je huu si ushahidi kuwa bila polisi kiungilia maandamano hakuna fujo wala mauaji?

Huu si ushahidi kuwa polisi wanatumika kisiasa?

Au hii ni mbinu ya kisiasa ya watawala ili chadema wakilalamika waonekane wana chuki na uislamu?

This is typical double standard.

tunapo hoji tujaribu kuwa na sababu za msingi. Mimi naona tungeanza na kujiuliza je ni hili tu la sensa au kuna lingine

mbona double standard kwenye intelijensia yetu iko wazi sana.. Wanatia aibu maana kazi yao ni ya kitaaluma, unapoona mwanataaluma anaweka taaluma pembeni na kuabudu watawala ujue anajiaibisha ndani na nje ya nchi yake! Wemaa, uwt nk amkeni bado mnaweza kurejesha heshima zenu.

hata kama kuna lingine je ni halali kipindi hiki cha sensa?

ongeazea je haya maandamano wakati shughuli za sensa inaendelea ni halali? Leo nimesikia tena mbunge wa cuf huko kilwa ameleta noma polisi akishinikiza waliokamatwa kwa kukataa kuhesabiwa waachiwe.

..most probably they had the information about muslims demonstration.

..ukweli ni kwamba polisi kwa sasa hivi wamenywea kutokana na habari za mauaji ya mwangosi.

..muda kidogo ukipita, na wa-tanzania na haswa waandishi wa habari wakisahau, basi polisi watarudia tena matendo yao machafu na ya kikatili.

jk ni dini gani vile?hapigwi mtu bomu hapo!!!!

hatuna haja ya kujiuliza, imepigwa maarufuku mikutano na maandamano yote isipokuwa kama mnasali, mpaka sensa iishe! Ni matumaini yetu wengi kuwa polisi watalisimamia hili kwa dhati ili waeleweke!

ila mmeshahesabiwa!! Kweli mmeonyesha jinsi gani mlivyo kichwani

hadi sasa wameshindwa kueleweka na imeshadhihirika wazi kuwa polisi wanatumika kuikandamiza cdm!

cdm wanatakiwa wasitoe tamko kuhusu maandamano haya, kwani tamko lolote litatafsiriwa kivingine na waislam wachache walioishia chuo tu.

na igp mwema na kova ni dini gani vile? Chora mstari!!! Ila tu polisi wetu kama hawajatumwa kutawanya mikusanyiko ya cdm au kibosile ambaye amekwapua nyumba ya mjane kama papa msofe na tajiri ambaye shamba lake limevamiwa, hua wanakuwa wapole sana!!! Si unaona tukio la ujambazi jana walivyokuwa wapole?? Hivi hakuna hata tetesi ya mtuhumiwa kukamatwa?

Islam is not a political party. Waisalamu wanapo amua hakuna mtu yoyote anae weza kuthubutu.
 
Jamaa walioandamana town center leo huku zoezi la senza likiendelea wameibuka washindi baada ya lile lililowafanya kuandamana kutekelezwa bila masharti......wameahidi wanaenda kujipanga safari hii watalala Necta.

Wakishafanikiwa necta waji waungane na wakristo ktk kuiondoa hii serikali legelege madarakani
 
Ametumwa na kikwete na mwema nayule mwenye jicho la chura kuwa njia rahisi waende kwa yule nchimbi wataachiwa.full stop.hi mbegu ya udini iliypandwa na ccm wanavuna sasa

teh eti mwenye jicho kama chura,
 
Back
Top Bottom