Maandamano dhidi ya matabaka marekani(wenye nacho na wasio nacho)

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Maelfu ya waandamanaji katika mji wa
New York wameendelea na harakati
zao wakielekea kuvuka daraja la
Brooklyn, kuonyesha ghadhabu zao
dhidi ya kuendelea kuwepo matabaka
nchini humo. Waandamanaji wanaadhimisha kuanza
kwa kampeini ya kupinga mfumo wa
kiuchumi unaosababisha matabaka
nchini Marekani ambapo walipiga
kambi katika mtaa wa Wall Street
kuliko na soko kuu la hisa na taasisi kubwa za kifedha Marekani. Mwezi
uliopita, polisi waliwakamata mamia ya
waandamaji . Taswira nje ya soko kuu la fedha la
Marekani ni raia wenye ghathabu
kubwa wakiendelea kukaribia jumba la
soko hilo na kulizingira kabisa.Polisi
wamekuwa na wakati mgumu
kuwazuia kwa kuweka vizuizi nje ya jumba hilo. Baadhi ya waandamanaji
wamekamatwa huku kukiwa na
makabiliano na ujibizanaji wa maneno
makali. Hamasa ya waandamanaji hao ni
kufuatia hatua ya polisi kuwafurusha
katika eneo walikokita kambi katika
bustani ya Zuccotti. Hii imewafanya
kushindwa kukesha huko. umati wa
watu ambao walikuwa wamekusanyika nje ya Wall Street
wameondoka. Hata hivyo wamepanga kukusanyika
tena katika kituo cha treni na jioni
watafanya jaribio jingine la kuvuka
daraja kuu ya Brooklyne. Waandamanji hao wanasisitiza
kwamba ni haki yao kuandamana.

My take :Je serikali yetu imejipanga vipi kupunguza gepu hili la wenye nacho na wasionacho?

Source:BBC
 
Back
Top Bottom