Maandamano baridi na Legal and Human Rights Centre, Salender Bridge

Hivi waziri wa afya, naibu wake na katibu mkuu wanaenda kazini kufanya nini? Wanataka watu wangapi wafe ndio waachie ngazi? Wanajisikiaje ndani ya mioyo yao? Hata kama mgogoro utamalizika hii timu itakuwa na mahusiano gani na madaktari?
 
Tayari wanaharakati wamefunga Ally Hassan Mwinyi na Ocean Road jijini Dar es Salaam ili kufikisha ujumbe kwa wenye mamlaka. Lengo ni kuwaonyesha watoa maamuzi kuwa haturidhiki na hatua wanazochukua katika kushughulikia mgogoro wa madaktari.
Hawa wanaharakati ni akina nani?
 
:poaAisee mambo yameiva....wamechoka kuona serikali inapuuzia madai yao ya msingi kwa kukaa kimya na kuwasababishia lawama kutoka kwa watanzania ambao wanapoteza ndugu zao kwa kukosa matibabu. ngoja tuone itakuwaje...:A S-coffee:
 
Hi ni hatari jamani poleni watanzania wenzetu ndo nchi yetu mkuu wa kaya azungumze sasa hi ndo nini sasa jamani hawa wakina mizengo wameshashindwa kuzungumza na hawa madokta sasa zamu yake
 
Hivi vyombo vya habari vya Bongo vina kazi gani?
issue kama hii hata hawatoi breaking news??
wanasubiria kutafsiriwa kwenye vyombo vya habari vya Magharibi na Asia??
 
ngoja tuangalie akili za askari wetu sasa na wakubwa wao..kama wakiwapiga madaktari watakuwa wanampiga mkunga huku wana mimba
 
kumbe tanzania ina madaktari wengi hivi....
Soon and very soon.....!
TahrirWar1-375x250.jpg
 
Yaani ni kitu cha kushangaza sana. Mgomo unaingia wiki ya pili sasa Watanzania wanakufa huku na kule na Rais yuko kimya kabisa!!!! Duh! niliwahi kuandika hapa jamvini kwamba huyu jamaa akiachiwa kuendelea kuwepo madarakani mpaka 2015 basi ataiacha nchi katika hali mbaya sana. Naona sikukosea kabisa.

Mkuu mpaka sasa mbona hali ni mbaya sana. Sema labda anangojea kuiuza, na nafikiri huyu jamaa lazima atatorokea uarabuni huyu akimaliza utawala wake 2015
 
Niko hapa barabara ya Ali Hassani Mwinyi,madaktari kwa wingi wao na umoja wao wamefunga barabara,foleni inatisha.Kwa sasa barabara hii haifai kupita.

Hayo maandamano ni ya wanaharakati na sio madaktari, acha kupotosha umma tafadhali
 
Back
Top Bottom