Maana na matumizi ya neno "Hayati"

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Ninavyoelewa origin ya neno "hayati" ni kwenye lugha ya Kiarabu ambalo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni "my life". Lakini kwa mujibu wa dictionary ya Kiingereza neno "hayati" linatumika zaidi "in an affectionate way usually towards someone who means a lot to you." Kwa mfano, "Goodbye my life" ni sawa na "Goodbye my Hayati".

Kwenye Kiswahili, neno "hayati" huwa linatumika zaidi kwa mtu ambaye ni marehemu. Je, lina maana sawa na ile maana ya Kiarabu? Ni marehemu wa aina gani wanaostahili kuitwa "hayati"?
 
Ninavyoelewa origin ya neno “hayati” ni kwenye lugha ya Kiarabu ambalo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni “my life”. Lakini kwa mujibu wa dictionary ya Kiingereza neno “hayati” linatumika zaidi “in an affectionate way usually towards someone who means a lot to you.” Kwa mfano, “Goodbye my life” ni sawa na “Goodbye my Hayati”.

Kwenye Kiswahili, neno “hayati” huwa linatumika zaidi kwa mtu ambaye ni marehemu. Je, lina maana sawa na ile maana ya Kiarabu? Ni marehemu wa aina gani wanaostahili kuitwa “hayati”?

Hayati kwa kiarabu kwa asilimia kubwa ni kama ulivyo lielezea,na mara nyingi katika nyimbo za kiarabu utasikia kitu kama "anta hayat" na katika lugha kuna mambo mawili huwa yanagongana sana nayo ni tafsiri na maana.Sasa kwa waarabu kumwambia mtu 'anta hayat' ni kumaanisha wewe ndio kila kitu kwangu...au anaweza kuwa kafurahishwa na mpenzi au hata mtoto wake akamkumbatia na kumwambia 'Hayatiiii'

Tukirudi katika swali lako,nadhani katika kiswahili tulipokea vibaya na ndio pale tunapomuelezea marehemu tunatumia neno hayati,ni kiwa na maana waswahili tunasema,hayati Babu yetu,hayati kaka yetu kwa marehemu,labda kwa kuongezea tu hata Waturuki wana tumia neno Hayati,mfano mtu anapokufa wanasema 'hayati kaibet'..sidhani kama kuna marehemu anaye stahili na asiye stahili kuitwa Hayati kwa sisi waswahili

Kwa kumalizia labda niongezee kuwa katika lugha wakati mwingine baadhi ya maneno huwa yanazaliwa kwa kupokea vibaya mfano hai ni neno MELI.
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Asante Mkuu kwa ufafanuzi. Kwa hiyo kwenye lugha ya Kiswahili hayati inaweza kutumika kwa marehemu yoyote, na sio tuu kwa "waheshimiwa" kama mchangiaji mmoja aliposema hapo juu? Maana wengi tunadhani kuwa "hayati" huwa inatumika zaidi kwa viongozi au watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii na "marehemu" kwa kila mtu.
 
Kwa kiswahili cha Tanzania Hayati limetumika kisiasa zaidi. Huwatambulisha Marehemu ambao katika uhai wao walikuwa na mchango mkubwa na tena maarufu kwa jamii. Mifano ni baadhi ya viongozi wakuu wa kabila waliopambana vikali kuupinga ukoloni, viongozi walioshiriki kwa namna mbalimbali harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, Zanzibar, na wale waloshika uongozi wa Taifa ngazi za juu. HaaMifano ni Hayati Chifu Mkwawa, Hayati Seti Benjamin, Hayati Abedi Amani Karume, Hayati Moringe Sokoine, Hayati Julius Kambarage Nyerere, nk.
 
Hapo unaweza kuonisha vipi na Steven Kanumba kuitwa hayati?
 
Ninavyoelewa origin ya neno hayati ni kwenye lugha ya Kiarabu ambalo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni my life. Lakini kwa mujibu wa dictionary ya Kiingereza neno hayati linatumika zaidi in an affectionate way usually towards someone who means a lot to you. Kwa mfano, Goodbye my life ni sawa na Goodbye my Hayati.

Kwenye Kiswahili, neno hayati huwa linatumika zaidi kwa mtu ambaye ni marehemu. Je, lina maana sawa na ile maana ya Kiarabu? Ni marehemu wa aina gani wanaostahili kuitwa hayati?
Hayati inatakiwa itumike kwa kila mfu mwanadamu na kwa aliye hai,kama wewe ni islamic kuna aya inasema(Fih hayati dunia wal akhera)sina hakina na spelling.Hii inamaanisha kwamba kuna hayati wa duniani na hayati wa akhera.
Ila kwa taratibu za kibinadamu aliye hai huwezi kumuita hayati ingawa aya hii inamaanisha kwamba aliye hai ni hayati mtarajiwa bila kujari kipato chake.
So ata wewe hata kama unaishi under $1 per day ukifa inatakiwa tukuite"hayati EMT"
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapo unaweza kuonisha vipi na Steven Kanumba kuitwa hayati?

Kwa misingi ya kisiasa nakijamii niloitaja mwanzo Kanumba hakuwa na sifa kama nilowataja na hivyo hayati halimstahili. Bado hatuna jinsi ya kuwazuia rafiki wala ndugu kumtaja wapendavyo ila kwenye kumbukumbu rasmi za Serikali ya Tanzania ndo hatutegemei aorodheshwe kama hayati.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hayati inatakiwa itumike kwa kila mfu mwanadamu na kwa aliye hai,kama wewe ni islamic kuna aya inasema(Fih hayati dunia wal akhera)sina hakina na spelling.Hii inamaanisha kwamba kuna hayati wa duniani na hayati wa akhera.
Ila kwa taratibu za kibinadamu aliye hai huwezi kumuita hayati ingawa aya hii inamaanisha kwamba aliye hai ni hayati mtarajiwa bila kujari kipato chake.
So ata wewe hata kama unaishi under $1 per day ukifa inatakiwa tukuite"hayati EMT"

Yea, Uarabuni mtu anaweza kuitwa Hayati kama first name. Ni jina kama majina mengine tuu. Lakini lugha ya Kiswahili sidhani kama unaweza kumwita mtu hai Hayati.
 
.

Mkuu, EMT,

Neno Hayati lina maana mbili:

Maana ya Kwanza: deceased, departed

Hayati huwakilisha mtu aliyekufa … yaani the late Mfano The Late Sokoine etc

Maana ya Pili: Life

Hayati huwakilisha Uhai (maisha) mfano kama una mgonjwa anaumwa alafu mtu akikuuliza vipi EMT anaendeleaje unaweza kumjibu .. Aah yupo yupo tu si hayati wala si mamati ikimaanisha EMT is still unwel

Haya hii hapa ni kwa mujibu wa
KAMUSI ya TUKI kuhusiana na tafsiri / Matumizi ya Hayati

hayati nm [a-/wa-]

1. deceased, departed, the late: ~ Shaaban Robert the late Shaaban Robert.

2. life. (mt) Si hayati si mamati, si mzima si mgonjwa he/she is still unwell.

.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ninavyoelewa origin ya neno “hayati” ni kwenye lugha ya Kiarabu ambalo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni “my life”. Lakini kwa mujibu wa dictionary ya Kiingereza neno “hayati” linatumika zaidi “in an affectionate way usually towards someone who means a lot to you.” Kwa mfano, “Goodbye my life” ni sawa na “Goodbye my Hayati”.

Kwenye Kiswahili, neno “hayati” huwa linatumika zaidi kwa mtu ambaye ni marehemu. Je, lina maana sawa na ile maana ya Kiarabu? Ni marehemu wa aina gani wanaostahili kuitwa “hayati”?

Tatizo la Lugha, neno moja linalotoholewa kwenye lugha nyingine linaweza likabaki na maana ileile ama inayofanana na ile au ni kinyume kabisa,
Lakini cha muhimu ni kulichukulia hilo neno jipya kama lilivyo na linavyotumika katika hiyo lugha husika, hata Lugha za kibantu pia zina hiyo tabia

mfano wa maneno yaliyobadilika maana ni wa Kiswahili na Kishona (Zimbabwe,Botswana,SouthAfrika/Mozambique)

KISU (Swahili) , Shona wao waasema BANGA(PANGA)
MAVU.ZI (Swahili), Shona wao wanasema NUWELE (NYWELE)
NYWELE (
Swahili), Shona wao wanasema MAVUDZI
MAJI (Swahili),
Shona wanasema MVULA (MVUA)
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Asante Mkuu kwa ufafanuzi. Kwa hiyo kwenye lugha ya Kiswahili hayati inaweza kutumika kwa marehemu yoyote, na sio tuu kwa "waheshimiwa" kama mchangiaji mmoja aliposema hapo juu? Maana wengi tunadhani kuwa "hayati" huwa inatumika zaidi kwa viongozi au watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii na "marehemu" kwa kila mtu.

vp unatafuta neno la kumwita ndugu yenu kanumba?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom