Maamuzi ya spika makinda juu ya Zitto

Magarinza

Senior Member
May 9, 2008
122
13
Wadau huyu mama kamlazimisha Zitto kuthibitisha kauli yake ya malobbist huku akimnyima nyaraka za serikali alizoomba. Ivi sheria inasemaje juu ya nyaraka za serekali kupatikana pale mbunge anapozihitaji hasa kwanufaa ya nchi??
 
zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto zitto
 
Kama uthibitisho wake unategemea hivyo vielelezo na hataki kumpa hataweza kumbana. By the way, mbona ya ripoti ya mtoto wa mkulima kulidanganya bunge kuhusu mauaji ya Arusha haileti bungeni japo Lema alishatoa vielelezo?
 
Huyu mama anakwaza maendeleo ya nchi kabisa
cheki jimboni kwake 2007 hii picha
 
Attachments

  • a primary school at Njombe.jpg
    a primary school at Njombe.jpg
    91.3 KB · Views: 943
Wadau huyu mama kamlazimisha Zitto kuthibitisha kauli yake ya malobbist huku akimnyima nyaraka za serikali alizoomba. Ivi sheria inasemaje juu ya nyaraka za serekali kupatikana pale mbunge anapozihitaji hasa kwanufaa ya nchi??

huyo mama ni galasa.

kesi ndo imeisha hivo.
 
Kishaona ukweli sasa hataki wananchi wajue.
Mbona huyu ni mpinga maendeleo no 1
 
*Kuthibitisha leo tuhuma za Baraza la Mawaziri

Na Grace Michael, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, leo anawasilisha maelezo yake kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni akituhumu Baraza la Mawaziri kutoa maamuzi yanayotokana na ushawishi watu wenye nia ya kuua mashirika ya umma.

Tuhuma hizo alizitoa bungeni wiki iliyopita wakati akichangia azimio la kuongeza muda wa uhai wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).

Kutokana na tuhuma hizo, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda alimpa muda wa siku saba ambazo zinamalizika leo, kuthibitisha kauli yake.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Zitto alisema leo atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika Makinda kama alivyoagizwa.

Katika mjadala huo, Bw. Zitto alipingana moja kwa moja na azimio hilo ambalo lilitaka kuongezwa muda wa miaka mitatu kwa CHC ambapo yeye alishauri liongezwe muda wa kutosha ili kukamilisha majukumu yake.

Hoja nyingine iliyomfanya apinge na kushikilia tuhuma hiyo kwa mawaziri, alisema kuwa maamuzi yaliyofikishwa bungeni yanatofautiana na makubaliano yaliyofikiwa katika Kamati ya Uchumi na Fedha.

Bw. Zitto aliwataka wabunge kukataa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa kuwa yametokana na kurubuniwa na watu wenye lengo la kuua CHC kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Alisema kuwa CHC ni chombo kinachoangalia mali za umma na mashirika, lakini pia kuna kesi mbalimbali za watu ambao wanadaiwa na mashirika, hivyo kwa kutoa muda wa mfupi ni kutaka kuua shirika hilo.

Shughuli zinazofanywa na CHC ambazo mpaka sasa hazijakamilika ni pamoja na urekebishaji wa TRL baada ya kampuni ya Rites kuondoka, kushughulikia uuzaji wa hisa za serikali NBC (T) Ltd, uhakiki wa mashirika yaliyobinafsishwa, urekebishaji wa mashirika 34 yaliyobaki na kukamilisha ufilisi wa mashirika ya umma 24 yaliyobaki, ukusanyaji wa madeni ya iliyokuwa NBC yenye thamani ya sh. bilioni 15.8 na urekebishaji wa kampuni ya TTCL baada ya hatua ya awali ya ubinafsishaji kushindikana na mwekezaji wa Airtel kuonesha nia ya kutoka katika ubia.
 
Huyu mama anakwaza maendeleo ya nchi kabisa
cheki jimboni kwake 2007 hii picha

WAKIENDELEA KUBAKI KATIKA HALI HII NDIYO INAKUWA RAHISI KUWATAWALA. HAWA HAWATAJUA KINACHOENDELEA DUNIANI HAPA. HAWA WAKISHIBA UGALI BASI, WANAONA SHIDA HAKUNA TENA. KUMBUKA WAHENGA WALISEMA UKILA NA KIPOFU USIMGUZE MKONO.
 
si nasikia amenyimwa ushirikiano na baadhi ya ofisi a serikali katika kukusanya nyaraka? mfano ofisi ya Spika. Ngoja tuone itakuwaje. Namshauri Spika, siku anayotolea uamuzi wa ushahidi wa Zitto pia atoe uamuzi wa ushahidi wa Lema.
 
Wadau huyu mama kamlazimisha Zitto kuthibitisha kauli yake ya malobbist huku akimnyima nyaraka za serikali alizoomba. Ivi sheria inasemaje juu ya nyaraka za serekali kupatikana pale mbunge anapozihitaji hasa kwanufaa ya nchi??

Zitto ameingia choo cha kike safari hii, nyaraka alizokuwa anazitaka ni siri, haiwezekani mtu km yeye kuzipata, asubiri rungu tu la Bunge !
 
Huyu mama anakwaza maendeleo ya nchi kabisa
cheki jimboni kwake 2007 hii picha

Hawana tofauti na wa Kigoma kaskazini mkuu wanasiasa ni baba mmoja mama mmoja.
 
Attachments

  • Kigoma N. Soccer Balls.jpg
    Kigoma N. Soccer Balls.jpg
    34.3 KB · Views: 43
Maskini wee ht zitto wawatu apeleke ushahidi wa ukweli kias gani huyu mmaza atauchimbia kapuni km kawaida yk na kunyamaza kimya kama
 
Back
Top Bottom