Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

na Mwandishi Wetu, Dodoma (Tanzania Daima)

Mjumbe huyo jina tunalo, alifikia hatua ya kusema Sitta ameanzisha kikosi...
Kama "jina tunalo" na hutaki kulisema, mimi msomaji unanambia jina unalo ili iweje, niifanyie nini siri yako wewe?

Hivi umepita mafunzo ya uandishi au mliokotwa okotwa Uwanja wa Fisi mkawe cheap labor kwenye newsroom?

Unaogopa kutaja jina la mjumbe wa Halmashauri ya CCM?
 
Last edited:
- Hapana mkuu wangu, tatizo ni Muungwana haeleweki na unajua kwua rais wetu kisheria ana power ya ajabu sana, so far anakuwa tatizo kubwa sana na everything!

Respect.

FMEs!

Sasa Mkuu wangu kama Rais ambaye ndio Mwenyekiti wa CCM haeleweki, na inaonyesha mafisadi wamemshika pabaya ama wamezidi nguvu, hivi kweli hapo kuna matarajio kwamba hiyo vita mtashinda from within?

Mzee Malecela hakuwepo kwenye kikao, na sijui kama Mama Kilango alikuwepo. Sasa kama hao ambao wanaongoza vita vya ufisadi wanashindwa kuhudhuria vikao kama hivyo ambavyo ni muhimu sana katika mapambano, huoni kwamba na wao wanaonekana kama wamekata tamaa? Walitakiwa wahudhurie hicho kikao ili wapambane na mafisadi kwa hoja na kuwaambia usoni kwamba fulani ni fisadi alifanya hiki na kile na kwamba kwa chama kuendelea kuwakumbatia wanakichafua chama na kukiweka kwenye hali ngumu kwenye uchaguzi ujao.

Mzee Malecela aliposema uchaguzi wa 2010 utakuwa mgumu alikuwa anatumia hali halisi aliyopambana nayo Busanda wakati wa Uchaguzi mdogo, kila kona mnazowema mafisadi. Bila kuiba kura 2010 hakitakuja kueleweka.

Mafisadi wote walikuwa Dodoma na walishapangana kuanzia kamati ya Maadili, CC mpaka kwenye NEC.

Kamanda FMES tuseme ukweli, hivi kweli hoja ya ufisadi ikiletwa kwenye kikao cha kamati ya maadili, Chenge atachangia kitu? Hao wengine nao usafi wako una mashaka. Ukienda kwenye CC same story, wajumbe wengi wa CC wana tuhuma za ufisadi, sasa ikiletwa hoja ya ufisadi unategemea wataipigia debe kwamba chama kisafishwe wakati wanajua wazi kwamba usafi ukianza na wao wenyewe watatakiwa kuondolewa. Kwa hiyo kupendekeza kwamba watu wenye tuhuma waondoke CCM ni sawa na kusema vunja secretariat yote ya CCM, Vunja kamati ya Maadili, vunja CC na vunja NEC, yaani watu waanze moja.

Ndiyo maana ninasema kwamba CCM kama chama kimechafuka, unaweza ku-single out very few members kwamba ni wasafi lakini majority ni wachafu na hao wachafu ndo wameshikilia nafasi muhimu kwenye secretariat ya chama, kamati ya maadili, CC na NEC.

Kwa mwendo huu hatuwezi kufika na CCM kuwa safi ni ndoto ya mchana. Dawa pekee ni kama Mwawado alivyosema ni kuwaondoa kwa kutumia sanduku la kura, japo ni ngumu sana kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ni ya kwao, Jeshi la Polisi ni la kwao, TAKUKURU ni ya kwao na Usalama wa Taifa unalinda maslahi ya mafisadi. Bado tuna safari ndefu kufikia uhuru kamili na Zuma ninamuona anakuja kwa kasi kubwa sana.
 
-
Dataz nyingine ni too hot kuzitoa kwa sasa, naomba time kidogo tuone upepo kwanza! Maana nyingi ya dataz ni za kukatisha tamaa sana kwa the so called mashujaaa!

Respect.

FMEs!

Vipi mkuu?

Mashujaa hawakuwa na courage ya kutetea wanachokiamini? Ndio siasa zetu hizo, maneno mengi lakini matendo kinyume. Inapofika wakati wa kuchukua maamuzi magumu, wengi wanaingia mitini.
 
Vipi mkuu?

Mashujaa hawakuwa na courage ya kutetea wanachokiamini? Ndio siasa zetu hizo, maneno mengi lakini matendo kinyume.

- Mashujaa wengi wanaponzwa sana na midomo yao mirefu huko pembeni, wengine wanaongea mno kwa kuamini kwamba wanakubalika na kila kiongozi, kumbe hao hao wanaishia kuwauza kwa mafisadi, mbinu zao zote zinajulikana mapema, wanaishia kuwaumiza mashujaa wengine walio serious zaidi na hii vita na hasa kuwaumiza wananchi zaidi at large! Kwa sababu Lowassa anatumia maneno yao wenyewe kuwasulubu kwenye hivi vikao!

- I hope they get the strong message ya hiki kikao ya kufunga midomo yao pasipohusu, au kwa maneno mengine shut up! garademit I am very upset!

Respect!

FMEs!
 
Jamani mjadala usiende kwenye personalities, tulenge kukikosoa chama. Hayo ya kuanza kutuhumiana usafi na uchafu wa mtu, tuwaachie wenye chama wanaosuguana huko kwenye vikao vyao.

Ndugu yangu Mtanzani ukianza kujibu vitu vidogo vidogo kama hivi kesho utajikuta kwenye magazeti ya Majira na title kubwa kweli kamba unatetea mafisadi. Ukiona post inakugusa na haijakufurahisha ipite tu kama vile hujaiona, ukianza kujibu tu ndiyo utakuwa unafungulia chokochoko na chimba chimba maana kambi ya upinzani ndani ya chama chako iko makini kuangalia mabandiko yako na ukiteleza tu wanayachukua kama yalivyo na kwenda kuyaweka gazetini kama jinsi ulivyojibu.

Hizo ndiyo siasa ndugu yangu, hata uwe msafi kama malaika lakini bado jamaa watatafuta hata kidoa kidogo sana ili kukutoa kasoro.
 
Sasa Mkuu wangu kama Rais ambaye ndio Mwenyekiti wa CCM haeleweki, na inaonyesha mafisadi wamemshika pabaya ama wamezidi nguvu, hivi kweli hapo kuna matarajio kwamba hiyo vita mtashinda from within?

Mzee Malecela hakuwepo kwenye kikao, na sijui kama Mama Kilango alikuwepo. Sasa kama hao ambao wanaongoza vita vya ufisadi wanashindwa kuhudhuria vikao kama hivyo ambavyo ni muhimu sana katika mapambano, huoni kwamba na wao wanaonekana kama wamekata tamaa? Walitakiwa wahudhurie hicho kikao ili wapambane na mafisadi kwa hoja na kuwaambia usoni kwamba fulani ni fisadi alifanya hiki na kile na kwamba kwa chama kuendelea kuwakumbatia wanakichafua chama na kukiweka kwenye hali ngumu kwenye uchaguzi ujao.

Mzee Malecela aliposema uchaguzi wa 2010 utakuwa mgumu alikuwa anatumia hali halisi aliyopambana nayo Busanda wakati wa Uchaguzi mdogo, kila kona mnazowema mafisadi. Bila kuiba kura 2010 hakitakuja kueleweka.

Mafisadi wote walikuwa Dodoma na walishapangana kuanzia kamati ya Maadili, CC mpaka kwenye NEC.

Kamanda FMES tuseme ukweli, hivi kweli hoja ya ufisadi ikiletwa kwenye kikao cha kamati ya maadili, Chenge atachangia kitu? Hao wengine nao usafi wako una mashaka. Ukienda kwenye CC same story, wajumbe wengi wa CC wana tuhuma za ufisadi, sasa ikiletwa hoja ya ufisadi unategemea wataipigia debe kwamba chama kisafishwe wakati wanajua wazi kwamba usafi ukianza na wao wenyewe watatakiwa kuondolewa. Kwa hiyo kupendekeza kwamba watu wenye tuhuma waondoke CCM ni sawa na kusema vunja secretariat yote ya CCM, Vunja kamati ya Maadili, vunja CC na vunja NEC, yaani watu waanze moja.

Ndiyo maana ninasema kwamba CCM kama chama kimechafuka, unaweza ku-single out very few members kwamba ni wasafi lakini majority ni wachafu na hao wachafu ndo wameshikilia nafasi muhimu kwenye secretariat ya chama, kamati ya maadili, CC na NEC.

Kwa mwendo huu hatuwezi kufika na CCM kuwa safi ni ndoto ya mchana. Dawa pekee ni kama Mwawado alivyosema ni kuwaondoa kwa kutumia sanduku la kura, japo ni ngumu sana kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ni ya kwao, Jeshi la Polisi ni la kwao, TAKUKURU ni ya kwao na Usalama wa Taifa unalinda maslahi ya mafisadi. Bado tuna safari ndefu kufikia uhuru kamili na Zuma ninamuona anakuja kwa kasi kubwa sana.

- Mkuu Keil inaudhi sana!

Respect.

FMEs!
 
Kwa nini Sitta hasisimame kidete, kwani anaogopa kudondosha kitumbua kwa kupigania haki za raia? Simama uhesabiwe, si lazima uwe spika. Unaweza kwenda kugombea ubunge chama chochote na kushinda as long as wananchi wako nyuma yako.
 
Masatu,

Waongera kutiki?

Lete more updates bana, maana wewe umekunywa maji ya bendera ya chama na bado una matumaini na chama chako.
 
Heri wewe ni msafi kuliko mimi? Sasa unaogopa nini kutaja jina lako?

Hata Sitta anasema yeye ni msafi huku anasahau ya CDA, anasahau ya nyumba ya TIC, anasahau ya dawa ya milioni mbili, naweza kujaza kurasa juu ya mambo ya Sitta.

I hope usafi wako sio kama huo wa Sitta.

shukurani kwa kututajia uchafu wa sita (naamini unauthibitisho wa uchafu huo). hata hivyo pamoja na uchafu wake na yeye anayohaki ya kudeal na wachafu wengine kwani hatimaye sisi wananchi tunapata nafasi ya kufahamu uchafu wa viongozi wetu katika ujumla wao.
 
Kumekucha na matumaini yangu ni kuwa hata wenye kudai wana damu ya kijani, watagundua kuwa binadamu mwenye afya nzuri damu yake ni nyekundu na wanaodai ni wasafi wataamka na kukuta kumbe wanalala na kuishi kwenye uchafu.

Kumekucha na huruma yangu inaelekezwa kwa wale waliojenga tumaini lao kwenye chama cha mafisadi na kwamba kansa ya ufisadi inayokitafuna hicho chama chao imeenea mwili mzima na hakuna ujanja wala matibabu yanayoweza kukiokoa.

Iliyoaminika kuwa ni vita dhidi ya ufisadi ndani ya CCM imekwisha na sasa wakereketwa wanaamka, kumbe ilikuwa ni ndoto tu ! Mafisadi huteteana, huchaguana na hulindana wakiongozwa na nia moja tu - usalama wao unaotegemea mshikamano wao.
Huu usanii unatupeleka pabaya, tuamke ! :(
 
Ni wakati wa kurejesha nidhamu ndani ya chama. Chama Cha Mapinduzi si mali ya mtu na yeyote anayeona kuwa ameonewa basi apeleke madai yake katika vikao halali, vinginevyo arudishe kadi.
Bravo Mzee Kingunge, sauti yako imesikika.
 
wrong haTUPO PAMOJA..ila wewe ndio upo pamoja naye...kwenye kufoji risiti za fansida za dola elfu2

si MZEE WETU bali ni mzee wako peke yako

wengine wazee wetu si MAFISADI kama huyu SITTA

Got that right

GT wafadhili wako wanaokuweka hapa mjini tunawajua kuwa wote ni mafisadi,tokea huyo wa NSSF, Malima mpaka Kingunge! Nakuhakikishia kuwa hao jamaa zako Sitta hawamuwezi.
 
Hawa watu wana matatizo...si kidogo. Nazungumzia watu waliochukizwa na kukerwa na procedures za Bunge na technicalities na kusifiwa kuwa walizungumza kwa hasira na kuonesha kukerwa. Yaani, zawadi kubwa wanayogombania ni nani abakie CCM nani asibakie. Watu walioshiwa uongozi huonekana kwa kufuata mkumbo.

Yaani humo kwenye kikao chao chote watu na akili zao na wengine "wasomi" wamekaa kujadili Mtu? Kwamba kati ya mambo yote yanayolihusu taifa letu saa na wakati huu wao wanagombania chama?

Kwa kweli imebidi niwatolee uvivu kuanzia Mwenyekiti wao hadi x,y!!
 
Mzee Mwanakijiji,
Nguvu hii wangeiweka kuwajadili kina Lowassa, Rostam na viongozi wengine mafisadi waliojiuzuru hakika wananchi tungewapa mkono mzito mkutano huu wa CC..hata kama wangefikia maamuzi wakasema tumetoa ONYO KALI kwa mafisadi..basi wananchi wangeivaa kamba hii shingoni..
Hizi ndio political game zinazotakiwa kuchezwa na CC lakini hili la Sitta, bila shaka ndio kwanza wanamwongezea sifa, Umaarufu na nguvu kubwa ya ushindani.

Kweli sasa hivi Sitta ni sawa na Nyati aliyejeruhiwa, lakini wanachoshindwa kujiuliza ni kwamba kwa nini walitaka kumwinda Nyati ngangari kati ya kundi zima! Siku zote Simba humchagua Nyati dhaifu ktk kundi..

Wametumia mifano ya kina Jumbe, Seif Sharrif Hamad na Mrema lakini wanasahau kwamba watu hawa kwa wakati tofauti wamewapa shida kubwa sana ktk chaguzi zilizofuata na wananchi hawakuwa makini na macho kama leo hii kiasi kwamba tutarudia makosa yaleyale..

Toka kuondoka kwa Jumbe Muungano umekosa kabisa mshikamano.. Seif kuondioka CCM ukweli utabakia kwamba CCM haiwezi kushinda Pemba na Unguja mwaka 2010..Mrema maskini wa watu kajiishia kweli lakini hakuna mtu aliyetetemesha utawala wa CCM kama Mrema na bahati mbaya tu wananchi walikuwa bado kizani..

Leo hii kumnyang'anya Sitta kadi ya chama ni sawa na CCM na kumnyang'anya kadi Nyerere kwani Sitta mzizi wake unagusana na vigogo wengi sana nchini. Ni mmoja kati ya wazee waliopeana Uongozi hivyo kumgusa yeye ni sawa na kuwagusa waasisi wa chama hicho - vita yake haitakwisha kirahisi..
 
Ni wakati wa kurejesha nidhamu ndani ya chama. Chama Cha Mapinduzi si mali ya mtu na yeyote anayeona kuwa ameonewa basi apeleke madai yake katika vikao halali, vinginevyo arudishe kadi.
Bravo Mzee Kingunge, sauti yako imesikika.

Nidhamu hairejeshwi kwa kukumbatia ufisadi. CCM imepoteza mwelekeo, chama kilichodaiwa kuwa cha wakulima na wafanyakazi sasa kimetekwa na mafisadi na ndiyo ambao wanaongoza nchi. Ninawashangaa ambao sio mafisadi kuendelea kung'ang'ania chama ambacho kimeishaonyesha wazi kwamba mwelekeo wake ni upi.

Hao mafisadi wanaomwaga hela ili kupata support kwenye NEC na CC, hawaendi kuzomewa wakati wa kampeni na chaguzi, wala hawapazi sauti kwenye majukwaa kujitetea kwamba wao siyo mafisadi.

Tusibiri 2010 inakuja na by then wananchi watakuwa walishajua fisadi ni nani na nani achaguliwe kuwa kiongozi. CCM itakapoteza majimbo ya kutosha ndipo watakapojifunza kwamba walifanya kosa kukumbatia ufisadi.
 
Keil,
Mkuu unajua umesema kitu kimoja amabcho nilikisahau siku nyingi.. CCM ni chama cha WAKULIMA na WAFANYAKAZI....wakati huo huo siku hizi sera za CCM zinawakandamiza wakulima na Wafanyakazi..
 
Tatizo CCM wanawapenda mafisadi na wote wenye nia mbaya na nchi yetu kama wanao saini mikataba feki n,k.Sitta uwe macho wasije wakakukolimba!
 
Hawa watu wana matatizo...si kidogo. Nazungumzia watu waliochukizwa na kukerwa na procedures za Bunge na technicalities na kusifiwa kuwa walizungumza kwa hasira na kuonesha kukerwa. Yaani, zawadi kubwa wanayogombania ni nani abakie CCM nani asibakie. Watu walioshiwa uongozi huonekana kwa kufuata mkumbo.

Yaani humo kwenye kikao chao chote watu na akili zao na wengine "wasomi" wamekaa kujadili Mtu? Kwamba kati ya mambo yote yanayolihusu taifa letu saa na wakati huu wao wanagombania chama?

Kwa kweli imebidi niwatolee uvivu kuanzia Mwenyekiti wao hadi x,y!!

Mimi sala zangu ni CCM wasambaratike manake tumechoka hata nishindwa nichangie nini hapa. Yaani unashangaa watu wengine kama ulivyosema "wasomi" lakini wako busy kumjadili mtu ili wamwondoe ktk chama kisa eti anatetea wananchi, kweli CCM mmefikia hapo??

Tuna haja ya kuanzisha mapambano ya ana kwa ana na wezi akina Lowasa, Karamagi, Rostam, Kingunge (japo huyu amekwisha), mkapa, Londa, akamba, n.k. yaani ni wengi sijui utaanzia wapi kusafisha CCM.
 
Sasa Mkuu wangu kama Rais ambaye ndio Mwenyekiti wa CCM haeleweki, na inaonyesha mafisadi wamemshika pabaya ama wamezidi nguvu, hivi kweli hapo kuna matarajio kwamba hiyo vita mtashinda from within?

Mzee Malecela hakuwepo kwenye kikao, na sijui kama Mama Kilango alikuwepo. Sasa kama hao ambao wanaongoza vita vya ufisadi wanashindwa kuhudhuria vikao kama hivyo ambavyo ni muhimu sana katika mapambano, huoni kwamba na wao wanaonekana kama wamekata tamaa? Walitakiwa wahudhurie hicho kikao ili wapambane na mafisadi kwa hoja na kuwaambia usoni kwamba fulani ni fisadi alifanya hiki na kile na kwamba kwa chama kuendelea kuwakumbatia wanakichafua chama na kukiweka kwenye hali ngumu kwenye uchaguzi ujao.

Mzee Malecela aliposema uchaguzi wa 2010 utakuwa mgumu alikuwa anatumia hali halisi aliyopambana nayo Busanda wakati wa Uchaguzi mdogo, kila kona mnazowema mafisadi. Bila kuiba kura 2010 hakitakuja kueleweka.

Mafisadi wote walikuwa Dodoma na walishapangana kuanzia kamati ya Maadili, CC mpaka kwenye NEC.

Kamanda FMES tuseme ukweli, hivi kweli hoja ya ufisadi ikiletwa kwenye kikao cha kamati ya maadili, Chenge atachangia kitu? Hao wengine nao usafi wako una mashaka. Ukienda kwenye CC same story, wajumbe wengi wa CC wana tuhuma za ufisadi, sasa ikiletwa hoja ya ufisadi unategemea wataipigia debe kwamba chama kisafishwe wakati wanajua wazi kwamba usafi ukianza na wao wenyewe watatakiwa kuondolewa. Kwa hiyo kupendekeza kwamba watu wenye tuhuma waondoke CCM ni sawa na kusema vunja secretariat yote ya CCM, Vunja kamati ya Maadili, vunja CC na vunja NEC, yaani watu waanze moja.

Ndiyo maana ninasema kwamba CCM kama chama kimechafuka, unaweza ku-single out very few members kwamba ni wasafi lakini majority ni wachafu na hao wachafu ndo wameshikilia nafasi muhimu kwenye secretariat ya chama, kamati ya maadili, CC na NEC.

Kwa mwendo huu hatuwezi kufika na CCM kuwa safi ni ndoto ya mchana. Dawa pekee ni kama Mwawado alivyosema ni kuwaondoa kwa kutumia sanduku la kura, japo ni ngumu sana kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ni ya kwao, Jeshi la Polisi ni la kwao, TAKUKURU ni ya kwao na Usalama wa Taifa unalinda maslahi ya mafisadi. Bado tuna safari ndefu kufikia uhuru kamili na Zuma ninamuona anakuja kwa kasi kubwa sana.
Мкuu unamaanisha nini hapa?
 
Kama "jina tunalo" na hutaki kulisema, mimi msomaji unanambia jina unalo ili iweje, niifanyie nini siri yako wewe?

Hivi umepita mafunzo ya uandishi au mliokotwa okotwa Uwanja wa Fisi mkawe cheap labor kwenye newsroom?

Unaogopa kutaja jina la mjumbe wa Halmashauri ya CCM?

Tanzania Daima ni miongoni mwa viji gazeti ambavyo Sitta alisema vinatumiwa na mafisadi. Usishangae kuona takataka kama hizi.
 
Back
Top Bottom