Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Kuhusu Kikwete kuwa sehemu ya tatizo nafikiri lazima utakubaliana na mimi ya kwamba bila ya Kikwete CCM ilikuwa inakwenda KUOZAAAAA KABISAAAA na ninachomsifu huyu bwana ni kuvipa sana uhuru vyombo vya habari maaana anaelewa kabisa wanahabari ndio wakombozi na wanamapinduzi hasa kwenye huu muda wa mkanganyiko na hawa mafisadi.

.
Unakumbuka Kauli aliyowahi kuitoa JK? Kelele za mbwa hazimzuii mwenye mbwa kulala? Ndo uhuru huo? Kama Wanahabari wanapiga kelele kila siku na kelele zao hazifanyiwi kazi na wapigiwa kelele( Kina JK) Kweli sifa zinamstahili?
 
Ccm kumkomalia sitta imeendelea kujiumbua zaidi na zaidi.Muda wote najaribu kufikiria kuwa hivi ningekuwa sitta sijui ningefanyaje(nijiuzuru?uspika napenda kwani kuna maslahi makubwa,lakini je maslahi binafsi ni bora kuliko ya taifa?,je kweli mimi ni mzalendo au natafuta tu umaarufu?)Sitta aachie ngazi huwezi kuwa mpiganaji ndani ya ccm.Ndio maana akina slaa,zitto hawaguswi pamoja na kuwa mwiba mkali kwa serikali kwani wako upande salama ccm si salama na hata walipojaribu kuwawajibisha ili kuwatiisha ikiwa ni pamoja na kuwekewa vinasa sauti ndani ya nyumba zao bado wakabaki na msimamo,slaa alikataa walipomtisha kuwa atakamatwa kwa kuwa anamiliki nyaraka za siri hakujali,alijiamini aliwajibu kwa kuwa tu yuko nje ya ccm.Wabunge wa ccm wamecharuka kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakishuhudia wenzao wanavyojichotea keki ya taifa bila hata aibu wameamua kusema na wanayo mengi sana ila hawawezi kuyasema kwa sababu wapo ndani ya ccm.Akina mwakyembe walitishia kueleza kila kitu ambacho kingewagusa wakubwa kuhusu richmond kwani wanasiri nyingi ambazo hawawezi kuzisema kwa kuwa wapo ndani ya ccm.Wale majemedali wa ccm wa vita kuu dhidi ya ufisadi(mwakyembe,kilango,sitta,sendeka n.k)wanajua fika kuwa ccm ni mahututi ila wameamua kufa nayo hivyohivyo wakipigana,ccm yenyewe imewatisha.Watoke wote kwenye hilo tanuli ambamo kuna moto,wajimalize kabla hawajamalizwa na ccm.Wameambiwa kuwa bila ccm wasingeweza kuwa maarufu nao wamekubali wanaamini ccm ndio mama na baba yao wanogopa kuasi hawataki kuleta upinzani wa kweli ambao Baba wa taifa alishatabili kuwa utatoka ccm na ambao tuna usubiri kwa hamu.Tuta pata upinzani ulio na picha ya kitaifa hasa kuliko chama cha upinzani chochote kilichopo,we fikiria hawa wanaamua kujiengua kwa maslahi ya taifa(mwakyembe,kilango,sitta,sendeka,na wale wengine)hapa utapata chama chenye sura ya kitaifa kuliko vilivyopo sasa ambavyo eidha kuna udini au kuna ukabila au vyote.
ahadi zimetekelezwa mnataka atekeleze ahadi gani tena?maisha bora hamuyaoni?mbona waalimu wamepandishiwa mishahara?madaktari mbona siku hizi mambo yao super?huoni mishahara ya wabunge na mawaziri juu?shule hamzioni jamani?mbona barabara tumejenga nyingi tu?au nyie ndo wale wa mahakama ya kadhi kwamba haitatekelezwa?
Tuendako siko,maamuzi mazito yanatakiwa ili kujinusuru na hali itakayojitokea.
''USAWA HAUPATIKANI KWA MZANI KUWA SAWA ,INATEGEMEA NA MPIMAJI MWENYEWE''
 
Tena mimi nawambie kuhusu iyo ishu ya sita ni kiini macho tu "Nyoka mwezi kuluma nyoka mwenzake" kuna jambo wanalipanga and they just use Mr 5+1 But he still on they side we will see soon..
 
Pdiddy,
Mkuu sina hakika kama haya ni mawazo yako au ume copy na Ku paste hivyo hukuweka jina la mwandishi..Lakini kitu kimoja tu ukumbuke kwamba Kumlaumu JK kwa kutomlinda Sitta ndio excuses walizotumia Mafisadi kuhisana na Sitta, ya kwamba Sitta kama Spika na mbunge wa CCM hakuweza kuwalinda wabunge wa CCM bungeni against Wapinzani..

Sasa Unapoimtaka JK alinde Sitta kwa sababu yeye nirais na anazo nguvu kubwa sana sijui utakuwa na tofauti gani na Mafisadi ambao walitaka Spika Sitta atumie nguvu ya wadhifa wake kuwakwamisha Upinzani.

MKUU MKANDARA UNAWEZA KUMLINDA MTUMISHI WA BWANA YAANI MCHUNGAJI/ASKOFU NK LAKINI KAMA ATAENDA KINYUME NA MAPPENZI YA MUNGU HATA SIKU MOJA AKUNA ATAKAEKUWA NYUMA YAKE...NINI MAANA YAKE...SITTA CHAGUO LA MUNGU NDIO MAANA WATANZANIA WOTE TUKO NYUMA YAKE
 
By the time mtakapojua kuwa Siita ni msanii tu mtakuwa mmechelewa sana.

The whole thing ni comedy kama kweli ana uchungu simple atoke huko ajiunge na wapiganaji wa kweli badala aya kutuchezea game. Huyu jamaa ni mjanja sana anauma na kupulizia, subiriini muda si mrefu rangi zake halisi zitaonekana.

.........TUAMBIE SITTA UNAYEMJUA WEWE,
SITA AKITOKA NDANI YA CCM HAWEZI KUFANYA KAZI ANAYOIFANYA SASA.VITA NZURI UNAPIGANA UKIWA NDANI YAO.
Kumbuka enzi za MREMA,alikubalika kwa wananchi alipokuwa CCM akadhani anaweza kuwa prizda,akajituoa CCM na kujiunga na NCCR,KILICHO FANYIKA NA MATOKEO YAKE SOTE TUNAYAJUA.
Hivyo ni vyema abakie CCM na ujasiri wake hadi hapo wananchi watakapo IFAHAMU CCM KWA RANGI ZAKE ZOTE.
NB.UKIWA NJE YA CCM,KILA UTAKACHO FANYA NI KAMA KELELE ZA CHURA,LAKINI UKIWA NDANI YA CCM,KILA UTAKACHO FANYA HATA MWANANCHI wa kawaida atajua na kuchukua kwa uzito mkubwa
 
  • Maandalizi kumg'oa ya muda mrefu
  • Kikwete alinong'onezwa mapema
Na Saed Kubenea
MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

NJAMA za kumng'oa Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta ziliratibiwa na baadhi ya viongozi wa juu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limedokezwa.

Taarifa zimeeleza kwamba maandalizi ya mashambulizi ya wajumbe wa vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), yamekuwa yakiandaliwa kwa muda mrefu sasa.
Lakini kilele cha maandalizi kilikuwa pale Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipotua uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Dar es Salaam, tayari kwa vikao hivyo, wiki mbili zilizopita.

Imeelezwa kwamba mara baada ya rais kutoa mguu wa mwisho kwenye ndege, Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba alimweleza, “Mwenyekiti, safari hii uwaache wajumbe waseme.”
Taarifa zinasema hata kabla Kikwete hajatafakari alichokuwa ameambiwa, Makamba aliongeza, tena karibu na sikio lake, “…Mwenyekiti, tafadhali waachie wajumbe wazungumze.”

Mtoa taarifa anaeleza kuwa baada ya mfululizo wa “maombi” ya Makamba kutaka Kikwete aachie wajumbe kusema walichonacho, Rais Kikwete alimgeukia na kuuliza, “Una maana gani?”
Ndipo Makamba alinukuliwa akipasua, “Wajumbe wamenituma nikueleze mwenyekiti, kwamba wanataka wazungumze. Wana jambo lao, waache waseme tena watasema sana….”

Hiyo ndiyo siri ya mlolongo wa wajumbe, mmoja baada ya mwingine, waliomtuhumu Sitta kutumia bunge kudhoofisha chama na serikali na kutaka afukuzwe uanachama.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, wajumbe kutoka Zanzibar waliandaliwa mapema pia. Ujumbe wa watu wawili kutoka Dar es Salaam (majina tunayo) ulitumwa Visiwani kuandaa wajumbe kwa hoja za kumsulubu Sitta.

Mmoja wa wajumbe wa NEC ambaye hakuongea kwenye kikao hicho aliliambia MwanaHALISI, kwamba mpango huo ulikuwepo kwani hata rais Kikwete alionekana kuuthibitisha wakati wa kuanza vikao hivyo.

Kama asiyejua kuweka siri, wakati kikao cha NEC kinaanza, Kikwete alinukuliwa akisema, “Tumekuja hapa, nimesikia watu wamenoa mapanga. Wanataka kufyeka watu. Haya…”
Lakini katika hatua nyingine, mwishoni mwa kikao cha NEC, Rais Kikwete ambaye aliruhusu milipuko dhidi ya Sitta, alinukuliwa akisema, “…Nadhani wametusikia; tuwasubiri Novemba. Tutajua kama wametuelewa au hapana.”

Taarifa zimeeleza kuwa rais alisisitiza kauli yake kwa kusema, “…Wenzetu ninyi (Bunge) mnapokutana, hali ya hewa inachafuka. Mkimaliza inatubidi tupite tena upya ili kuweka mambo sawa.”
Akielekeza hoja hiyo kwa mjumbe, rais amenukuliwa akisema, “…Dk. Mwakyembe (Harrison Mwakyembe), kwa nini mnatafuta umaarufu binafsi badala ya umaarufu wa chama?”

Awali Dk. Mwakyembe akiunga mkono kazi anayofanya spika Sitta, alisema mgogoro ulioko ndani ya chana unatokana na makundi mawili – moja alinalopinga ufisadi na jingine linalounga mkono ufisadi.

“Ugomvi huu utaisha pale ufisadi utakaposhindwa. Zaidi ya hapo hakuna kinachoweza kumaliza ugomvi wetu,” alisema.
Wiki mbili zilizopita, NEC ilitoa azimio la kutaka hoja kuhusu ufisadi zisijadiliwe bungeni bali kwenye vikao vya chama ili kuepusha kunufaisha upinzani na kudhoofisha chama na serikali (soma makala uk.5).

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha NEC, “Tumesema inatosha. Hapa tulipofika tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo linajiona kama ni wateule wa kuzungumzia ufisadi.”
Kauli hii ya CCM ililenga wabunge jasiri ambao wamekuwa wakiikosoa serikali, miswada yake na kutaka watuhumiwa wa ufisadi kuchukuliwa hatua.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, William Kusila alinukuliwa akisema, “…Wanachokifanya wabunge kwa upande wa serikali ni kama uhaini…”

Miongoni mwa waliopata fursa ya kumshindilia Sitta alikuwa John Guninita, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
Amenukuliwa na mtoa habari wetu akisema, “Ukimwachia mnyama aliyejeruhiwa, atakujeruhi wewe. Mwenyekiti, huyu mtu tumemwonya mara mbili, hajasikia. Tukimwacha leo atakuja kukung’oa wewe. Tumalizane naye hapahapa.”

Baada ya wajumbe zaidi ya 40 kumtuhumu, kumtishia na kumkejeli, mwishoni Sitta alikiambia kikao, “Nimewasikia. Mimi ni mtu mzima. Tuiachie kazi kamati iliyoundwa.”
Sitta amethibitishia MwanaHALISI kuwa taarifa za awali kwamba aliomba radhi hazikuwa sahihi. Ameuliza, “Niombe radhi kwa kitu gani?”
Taarifa zinaeleza kuwa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye alisema katika kikao hicho kuwa “kufanya kosa si kosa, bali kosa ni kurudia kosa.”

Sitta aliwaambia wananchi kwenye tamasha la kwaya la wakriso katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora mwishoni mwa wiki, “Uongo sasa umekuwa biashara. Watu wanatumia uongo kuficha mambo. Nchi haiwezi kubaki katika uongo kwa kuwa uongo ni laana.”

Alisema kumeibuka tabia ya waovu wanaosambaza “uongo uliopakwa asali; hugeuza uongo huo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Siwezi kukubaliana nao kwa sababu ni waovu," amesisitiza Sitta akiwalenga waliotaka avuliwe uanachama wa CCM.
Alisema, “Ninajua kuwa Mungu peke yake ndiye anayenilinda, kwa hivyo sitatetereka hata kidogo." Aliapa kupambana na mafisadi hadi ushidi upatikane.

Alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya baadhi ya watu nchini, kulazimisha yale wanayoyafanya wao yaonekane kuwa ndiyo ya ukweli kabisa hata kama ni ya uongo.
Naye mke wake spika, Margaret Sitta ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto amenukuliwa akisema kuwa “maisha ni mpito na kifo ni faida.”
Alikuwa anaunga mkano hoja ya mumewe, akinukuu kauli ya Askofu Norbert Mtega wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea, alipokuwa akizungumza katika msiba wa baba wa Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.
"Kauli ile ya Askofu Mtega tunaichukua na sasa tunaifanya kuwa falsafa ya maisha yetu, kwa maana hiyo kwetu sisi sasa maisha ni mpito tu na kifo kwetu ni faida," alisema waziri huyo.
Kikao cha NEC kiliunda kamati ya watu watatu kutafuta kiini cha kile kilichoita mgogoro miongoni mwa Bunge, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, serikali na CCM na jinsi ya kuuondoa.
Kamati hiyo iliyoko chini ya rais mstaafu Mwinyi inahusisha aliyekuwa spika wa bunge la Jamhuri, Pius Msekwa na aliyekuwa spika wa Baraza la Kutunga Sheria la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana.
 
  • Kikwete alinong'onezwa mapema
Na Saed Kubenea
MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

Taarifa zimeeleza kwamba ...mara baada ya rais kutoa mguu wa mwisho kwenye ndege, Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba alimweleza, "…Mwenyekiti, tafadhali waachie wajumbe wazungumze."

Rais Kikwete alimgeukia na kuuliza, "Una maana gani?"
Ndipo Makamba alinukuliwa akipasua, "Wajumbe wamenituma nikueleze mwenyekiti, kwamba wanataka wazungumze. Wana jambo lao, waache waseme tena watasema sana…."

Hiyo ndiyo siri ya mlolongo wa wajumbe
Kubenea, weka picha ya Kikwete anatoa mguu kwenye ndege na Makamba anamnong'oneza, halafu tuone huyo ndugu "Taarifa Zinasema" alikuwa karibu kiasi gani kuweza kusikiliza wanachonong'onezana Rais na Makamba. Mwongo, mdaku mkubwa we, fisadi wa hela za wasomaji wako, wale ambao hawako sophisticated kujua uhoro wa magazetini, una bahati sana, ndio unapogangia njaa hapo, shukuru Mungu kwa hilo.
 
kama kawa
kuna watakaong'aka wakiambiwa ukweli.
Ila kilichotokea kule dom kinaashiria kwamba kulikuwepo na mpango since mwanzo. Mie nasema wazi wazi kwamba serikali haipo kwa ajili ya wananchi ndo maana masuala muhimu kwa ustawi wa taifa inayapuuzia. sana sana inajali maslahi na ustawi wa viongozi.

Dilunga wote tunajua humu kwamba umetumwa ila si haba unachangamsha jukwaa kwa fikra zako mgando
 
kama kawa kuna watakaong'aka wakiambiwa ukweli.

Dilunga wote tunajua humu kwamba umetumwa ila si haba

Weeeka evidence!

Kwa nini tuandikie mate bana? Tujue nani mzushi, tundikeni picha hapa ya Kikwete anashuka kwenye ndege, Makamba anamnong'oneza kitu, na bwana "Taarifa Zimeeleza" yuko beneti anasikilizia. Weka tuone!
 
Kubenea, weka picha ya Kikwete anatoa mguu kwenye ndege na Makamba anamnong'oneza, halafu tuone huyo ndugu "Taarifa Zinasema" alikuwa karibu kiasi gani kuweza kusikiliza wanachonong'onezana Rais na Makamba. Mwongo, mdaku mkubwa we, fisadi wa hela za wasomaji wako, wale ambao hawako sophisticated kujua uhoro wa magazetini, una bahati sana, ndio unapogangia njaa hapo, shukuru Mungu kwa hilo.

Mkuu swala si kuwa huyo msemaji alikuwa umbali gani, swala ni kwa namna gani habari kama hizi zinaua uwezo wa kufikiri!

1. JK anaena kwenye kikao kisicho na ajenda mpaka anatua uwanja wa ndege? is this could be true??

2. JK ambaye anajua mambo mengi kutoka source nyingi KUWA alikuwa hajui kuwa kuna watu wanataka wamseme Sitta?????(unbelievable)

3. Kuwa katika kikao hicho wajumbe 40 wote walimsema vibaya Sita na hakuna top officials yeyote aliyekuwa upande wa sita??(this sita should think twice)

4. Kuwa JK kasema mwakyembe anajitafutia sifa binafsi na sio za kichama? na Mwakyembe akajibu kuwa kuna wapinga mafisadi na wasiopinga ufisadi!!!!!!!! and then JK response was what??????

Tumekuwa tukiambiwa habari zinazowafanya watanzania wakilala na kuamka wafikirie CCM, waiseme CCM, wapewe moyo na CCM, tujione kuwa CCM is the only one, and this country without CCM is no longer exists!

Tutakapoacha kuwaz katika CCM context, ambazo akina KUBENEA WITH VERY CAREFULLY TECHNIQUES THEY HAVE BY MANY MEANS TRIED TO MANIPULATE MANY TANZANIANS! tukisema hivi tunaonekana, wasaliti

Angalia uandishi wa Cheche la MKJJ na mwanahalisi utagundua namnaanisha nini Cheche makes you to think beyond! mwanahalisi linakufanya ubaki katika uMBEA na kuwaza ndani ya BOX LA CCCM ......eti....ALIMNONG'ONEZA SIKIONI!!! ETI WAACHIE WAJUMBE WASEME!!! WHAT SHAME IS THIS!!!!!!!!!

CCM watumieni mtakao, but we are thinking otherwise how to take our country from you monsters!

kwa kupenda habari za udaku ndio akina Shigongo matajiri leo!

message sent!
 
Tatizo sio Sitta wala Kikwete tatizo ni Chama kizima cha CCM,hiki Chama kimechoka sana na hawana lolote la kuwambia wananchi zaidi ya kuwadanganya na kuwabadilishia matokeo ya kura zao.

CCM iko katika hali mbaya sana kiutawala na haina dawa ya kukaa sawa zaidi ya kuiondoa madarakani ili wake benchi na kuanza upya,
Kiutawala katika CCM kila mmoja ni mwamba dhidi ya mwenziwe na walichonacho viongozi hao wa CCM ni kila mmoja kutaka kujionyesha kuwa yeye ana nguvu zaidi ndani ya Chama ya kumpiku na kumueka kiti moto mwengine ikiwezekana kumuengua katika uongozi,kama tulivyoona kuwa mbinu za kumuondoa Sitta hazikuanza jana wala juzi ni mkakati ambao uliandaliwa kwa muda mrefu sana.

Sasa isionekane kuwa mambo yametulia bali kilichotokea kwa kukingiwa kifua Sitta ni kundi hilo linalompinga Sitta kujiandaa kivingine na kuwachanganya wale wote walioonekana kumlinda Sitta na nani na nani walifanikiwa kuwezesha Sitta kutoondolewa ,hao ndio watakaopata tabu katika shughuli za CCM zijazo ukiwemo uchaguzi Mkuu ,kwa maana kundi la wahafidhina wa ufisadi litaweza au kushaurika hata kumfagilia mtu mwengine kutoka Chama Cha upinzani ikiwemo kuwanunua mawakala na wajumbe wa tume katika kuhakikisha bora CCM izame kuliko kupita CCM ambao wanaonekana ni mujahidina katika kukwamisha dili za kifisadi. Tusubiri mepya.
 
Weeeka evidence!

Kwa nini tuandikie mate bana? Tujue nani mzushi, tundikeni picha hapa ya Kikwete anashuka kwenye ndege, Makamba anamnong'oneza kitu, na bwana "Taarifa Zimeeleza" yuko beneti anasikilizia. Weka tuone!

Siku hizi mijifisadi haijambo kwa kusema 'Weeeka evidence'! Inajua kabisa likamanda lao JK linawalinda...
 
Duh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani mtu akinong'onezwa wewe unasikiaje?

Unless Makamba au JK mwenyewe wawe watoa taarifa
 
...mwanahalisi linakufanya ubaki katika uMBEA na kuwaza ndani ya BOX LA CCCM ......eti....ALIMNONG'ONEZA SIKIONI!!! ETI WAACHIE WAJUMBE WASEME!!! WHAT SHAME IS THIS!!!!!!!!!

kwa kupenda habari za udaku ndio akina Shigongo matajiri leo!

Right, national news zanaandikwa kidaku daku dakuuu...

Unajua, nimekuelewa vizuri sana, kwamba hata kama ingeonyeshwa picha ya Makamba ananong'onezana na Rais, bado hiyo siyo evidence ya walichoambiana, kwamba Rais Kikwete alikuwa anaenda kwenye kikao ambacho amepewa agenda kwenye runway ya airport!... na kwamba Mwakyembe alivyojibizana na Rais kwamba kuna makundi ya mafisadi na wasafi, Rais alijibu nini, etc. etc., hiyo level ya sophistication kuuliza data hizo, unaenda mbali saaana. Kubenea hana sophistication ya kuelewa hayo, ndio maana nashusha ile bar, nampa Kubenea benefit of the doublt kwamba akionyesha picha Kikwete anatoa mguu kwenye ndege na Makamba anamdaka kumpa siri ya kikao, na kuna mpambe wa Kubenea anasikiliza nitamwamini.

Kwa sababu yeye Kubenea ametushusha so low, kutufanya wajinga kwamba Kikwete kapewa agenda ya mdomo airport, basi na mimi nataka ku dili nae huko huko kwenye mawazo shalow, sitaki discourse ndeeefu na Kubenea, namwambia, nionyeshe picha tu! Mwongo, shambenga mkubwa Kubenea.
 
This is very interesting. Perhaps it would be better if all news items in all newspaper in this country will be accompanied by photos. But the problem is how can we confirm what is written in the caption and what is actually being said. Inabidi Kubenea aanze kuweka audia kwenye gazeti.
 
Back
Top Bottom