Maamuzi ya Kidemokrasia kufanywa na Consultant.

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
Maamuzi ya kidemokrasia hufanywa na watu.

Ilimshangaza kila mpenda haki pale Chadema waliposhindwa kuwapata wabunge wa viti maalum wanawake kwa njia ya kura na badala yake wakatoa tenda ya kuchagua wabunge hao kwa mtu mmoja akiwa kama Mshauri Mwelekezi (consultant).

Consultant akawapangia orodha ya aliowataka kwa kipaumbele (wa kwanza mpaka wa mwisho).

Matokeo yake tumeyaona - Viongozi na Wanachama wanakitupa mkono chama kama wamepagawa.

Naomba tujadili ndugu wanachama wa Chadema; hii ni demokrasia ya kweli kama ambavyo inatanabaishwa kupitia jina la chama chenu?

au nd'o tuiite 'democracy ala chadema'?
 
We Mjinga kalale saa hizi!!!! Acha kupoteza muda wako na taratibu za chama kisichokuhusu. Huyu aliyekulipa kukiandama CHADEMA, hana sera zaidi ya kuchakachua kura tu. Mwambie kwanza mwenyekiti wako akatangaze baraza la mawaziri kuliko kung'ang;ania vitu visivyokuwa na mshiko!
 
Maamuzi ya kidemokrasia hufanywa na watu.

Ilimshangaza kila mpenda haki pale Chadema waliposhindwa kuwapata wabunge wa viti maalum wanawake kwa njia ya kura na badala yake wakatoa tenda ya kuchagua wabunge hao kwa mtu mmoja akiwa kama Mshauri Mwelekezi (consultant).

Consultant akawapangia orodha ya aliowataka kwa kipaumbele (wa kwanza mpaka wa mwisho).

Matokeo yake tumeyaona - Viongozi na Wanachama wanakitupa mkono chama kama wamepagawa.

Naomba tujadili ndugu wanachama wa Chadema; hii ni demokrasia ya kweli kama ambavyo inatanabaishwa kupitia jina la chama chenu?

au nd'o tuiite 'democracy ala chadema'?

Hebu tufanye kidogo utaratibu wa kulinganisha mambo, akina VICKY KAMATA kule Sisiem watakua wamekidhi vigezo gani vile kabla ya kutia-timu kule Bungeni Dodoma????
 
pole kishongoooooooo!!!!!!!!!!!! usiku ni wakati tulivu kwa watu kufikiri na kujadili mambo ya msingi kwa maendeleo ya taifa, jamii na ya kwako binafsi. unajadili kitu viti maalum leo kweli wakati umekupita, wanaokutumia hawajui hata watu wa kuwatukia. lala ukue
 
Hebu tufanye kidogo utaratibu wa kulinganisha mambo, akina VICKY KAMATA kule Sisiem watakua wamekidhi vigezo gani vile kabla ya kutia-timu kule Bungeni Dodoma????

Wamechaguliwa kwa watu kupiga kura, zikahesabiwa, akapatikana mshindi kihalali.

Kwani ni ajabu Vicky kushinda ubunge? Mbona Bi mdogo Halima ameshinda?
 
Unatakiwa uwe na nidhamu na umuheshima Halima, ubunge wake si wa asante, amepambana akajitoa kimasomaso amewafunika mpaka kina Anna Abdallah
Wamechaguliwa kwa watu kupiga kura, zikahesabiwa, akapatikana mshindi kihalali.

Kwani ni ajabu Vicky kushinda ubunge? Mbona Bi mdogo Halima ameshinda?
 
Angalizo: Aliyeripotiwa kuwa ni Mshauri Mwelekezi ni mwanachama wa chama husika na ana cheo humo.
 
Wangeondoa tu hivi viti maalum, havina tija na vinaongeza mzigo kwa wananchi tu.
 
Huwa naepuka sana mijadala inayohusu watu lakini hapa nimeshindwa kuvumilia, kumlinganisha Halima na hichi kituko cha CCM ni kukosa adabu kwa mzungumzaji na upofu wa hali ya juu wa kuthamini vigezo vya uongozi. UKOME KABISA maana Halima hakuhitaji kuzaa nao kupata ubunge, wala kulala nao ili apate cheo kazini KOMA KABISA KUDHARAU watu wenye maadibi humu ndani hatuta entertain watu wa namna yako.
 
Back
Top Bottom