Maamuzi ya kamati ya utendaji ya CUF - Taifa (kikao kimemalizika leo Zanzibar)

Julius,

Asante kwa kulete taarifa humu haraka haraka. Hata hivyo siyo kawaida yako. Lakini pia, wewe ni Mtuhumiwa katika sakata hili. Pia, inaonekana hata unavyolichukulia ni kama unashabikia hivi. Take care! Usipokuwa makini hutofika mbali. Just my advice!
 
msiwe wa jinga wachangiaji wote humu mmelewa na mmerukwa na akili kama si akili zenu kuparalaizi. Mtu amewasilisha mada jukumu lenu mgetaka kujua na kujifunza ningewaona ni watu wenye busara , badala yake na masaburi ndo ya metawala.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIKamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Wananchi (CUF) imefanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar tarehe 30 - 31 Desemba, 2011 chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.Pamoja na kujadili ajenda kadhaa za kawaida kuhusiana na mambo ya utendaji katika Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa pia ilipata nafasi ya kupokea taarifa ya kina kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama kutoka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Nidhamu na Maadili. Taarifa hiyo ilijikita zaidi katika njama zinazoendeshwa na wanachama 14 wakiongozwa na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed zenye mwelekeo wa kutaka kukivuruga Chama.Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo. Wanachama hao ni:1. Hamad Rashid Mohamed2. Doyo Hassan Doyo3. Shoka Khamis Juma4. Juma Said Saanani5. Yasin Mrotwa6. Mohamed Albadawi7. Mohamed Masaga8. Doni Waziri9. Yusuf Mungiro10. Nanjase11. Ahmed Issa12. Tamim Omar13. Amir Kirungi14. Ayubu KimangaleKwa mujibu wa Katiba ya Chama, kifungu cha 63 kinachozungumzia Wajibu wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kifungu cha 63 (1) (d) kinafafanua wajibu huo kuwa ni "kulinda na kuendeleza heshima ya Chama na Serikali zote halali za nchi." Kifungu cha 63 (1) (j) kinaelezea wajibu mwengine kuwa ni "kuwachukulia hatua za nidhamu viongozi na wanachama wanaoshutumiwa kwa makosa mbali mbali kwa kufuata masharti ya Katiba hii na kanuni zitakazotungwa mara kwa mara kwa mujibu wa katiba hii."Kwa kuzingatia hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna haja ya kutumia uwezo iliopewa chini ya kifungu cha 62 (1) cha Katiba ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ili kutafakari hali hiyo, kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama hao, kuwapa nafasi ya kuwasiliza na kujitetea na kisha kuchukua hatua kama litakavyoona inafaa.Kikao hicho cha Baraza kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika Zanzibar, tarehe 04/01/2012 katika ukumbi wa hoteli ya Mazson.Kamati ya Utendaji ya Taifa inawaomba wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kutoa nafasi kwa vikao vya Chama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama.HAKI SAWA KWA WOTE Imetolewa na; JULIUS MTATIRO,NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA),KATIBU WA KAMATI YA UTENDAJI TA TAIFA (CUF NATIONAL CENTRAL COMMITTEE).31 Disemba 2011,ZANZIBAR.
"haiwezekani watu wakatenda dhambi mbaya ya kubagua wengine pasibo adhabu!",Mwl J.K.NYERERE
 
Mtatiro nimekufurahia gafla! Wewe ndiye alama halisi ya wanasi-hasa wetu. Unatumwa kuzungumza(na unazungumza ofkoz) hata kile ambacho ww mwenyewe hukiamini. YOU ARE JUST LIKE A BAMBOO FLUTE,JUST BLOW OUT AIR,IT WILL SOUND! kisa? Mkono uende kinywani! Najua wajua you have been used. Now get ready to be refused.

pumba zako peleka huko hata unachokiongea hukielewi. Kama vip mrudi shuleni ikiwa unashindwa hata kielewa kilicho andikwa. Haf unaongea utumbo.kweli we nusu mtu nusu fisi
 
msiwe wa jinga wachangiaji wote humu mmelewa na mmerukwa na akili kama si akili zenu kuparalaizi. Mtu amewasilisha mada jukumu lenu mgetaka kujua na kujifunza ningewaona ni watu wenye busara , badala yake na masaburi ndo ya metawala.
Unapoambiwa pombe mbaya hutaki kuelewa,kesho zikiisha rudi usome uharo huu uloandika!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Vipi huyu mjamaa? Mbona baada ya kutundika tu katoka nduki hajarudi tena!!!! What's wrong with him? Hataki kuwajibu wanaJF?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Wananchi (CUF) imefanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar tarehe 30 – 31 Desemba, 2011 chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.


Pamoja na kujadili ajenda kadhaa za kawaida kuhusiana na mambo ya utendaji katika Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa pia ilipata nafasi ya kupokea taarifa ya kina kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama kutoka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Nidhamu na Maadili. Taarifa hiyo ilijikita zaidi katika njama zinazoendeshwa na wanachama 14 wakiongozwa na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed zenye mwelekeo wa kutaka kukivuruga Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo. Wanachama hao ni:

1. Hamad Rashid Mohamed2. Doyo Hassan Doyo
3. Shoka Khamis Juma
4. Juma Said Saanani
5. Yasin Mrotwa
6. Mohamed Albadawi
7. Mohamed Masaga
8. Doni Waziri
9. Yusuf Mungiro
10. Nanjase
11. Ahmed Issa
12. Tamim Omar
13. Amir Kirungi
14. Ayubu Kimangale

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kifungu cha 63 kinachozungumzia Wajibu wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kifungu cha 63 (1) (d) kinafafanua wajibu huo kuwa ni “kulinda na kuendeleza heshima ya Chama na Serikali zote halali za nchi.” Kifungu cha 63 (1) (j) kinaelezea wajibu mwengine kuwa ni “kuwachukulia hatua za nidhamu viongozi na wanachama wanaoshutumiwa kwa makosa mbali mbali kwa kufuata masharti ya Katiba hii na kanuni zitakazotungwa mara kwa mara kwa mujibu wa katiba hii.”

Kwa kuzingatia hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna haja ya kutumia uwezo iliopewa chini ya kifungu cha 62 (1) cha Katiba ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ili kutafakari hali hiyo, kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama hao, kuwapa nafasi ya kuwasiliza na kujitetea na kisha kuchukua hatua kama litakavyoona inafaa.

Kikao hicho cha Baraza kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika Zanzibar, tarehe 04/01/2012 katika ukumbi wa hoteli ya Mazson.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawaomba wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kutoa nafasi kwa vikao vya Chama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama.


HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na;

JULIUS MTATIRO,
NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA),
KATIBU WA KAMATI YA UTENDAJI TA TAIFA (CUF NATIONAL CENTRAL COMMITTEE).
31 Disemba 2011,
ZANZIBAR.
.

Naomba mnisaidie majibu ya maswali yafuatayo;

1. Hivi makao makuu ya CUF yako Zanzibar?? Maana kila kitu cha CUF ,vikao vingi Zanzibar kwanini hamfanyi vikao vyenu huku bara? Au CUF ni chama cha visiwani tuu?

2. Suala lingine linalonishangaza nauliza hivii CUF hawana makamo wenyeviti(bara na visiwani),kazi yao ni nini?kwanini kikao kiongozwe na Seif?

3. Hivi CUF hawana wanachama wakristo? Mbona majina yote ni ya kiislam.? Ina maana ni kweli kuwa chama cha CUF ni cha kiislam?
 
Mtatiro ndugu yangu kama unataka amani achana na jamii forum tumia blogs nyingine hii jf ni kwa ajili ya viwavi wa cdm
Mtatiro naomba nikusifu kwa kuileta taarifa hii muhimu ya chama chako hapa JF. Tofauti za mawazo na Mitazamo ziwe Changamoto yako na si za kuzikimbia kwa njia yeyote ile kwani zianakujenga katika siasa.
 
Kumbukeni: Chama ni chenu; maamuzi yoyote mtakayofanya yatakiathiri au kukinufaifaisha chama chenu kwa namna moja au nyingine. Tumieni hekima ba busara ktk kufanya maamuzi yenu.
 
.

Naomba mnisaidie majibu ya maswali yafuatayo;

1. Hivi makao makuu ya CUF yako Zanzibar?? Maana kila kitu cha CUF ,vikao vingi Zanzibar kwanini hamfanyi vikao vyenu huku bara? Au CUF ni chama cha visiwani tuu?

2. Suala lingine linalonishangaza nauliza hivii CUF hawana makamo wenyeviti(bara na visiwani),kazi yao ni nini?kwanini kikao kiongozwe na Seif?

3. Hivi CUF hawana wanachama wakristo? Mbona majina yote ni ya kiislam.? Ina maana ni kweli kuwa chama cha CUF ni cha kiislam?

Acha udini wewe..
 
Mtatiro ulikuwa Udsm wa sasahv huyu ni mwangalia tumbo lake, by the way njoo ujbu hzo hoja hapo juu.
 
Bro Mtatiro! Pa1 na taarifa hii, hapo ulipo (cuf) hapakufai, au njaa? Unakuwa kama Tambwe! Unaongozwa na mkuno wa njaa ya tumbo! unakaa hata pasipokufaa!? Kwa nn usijichanganye na wapambanaji wa aina ya Lema, Mnyika, Zitto na wengine? Ushazeeka. Au kupewa cheo cha unaibu katibu mkuu ndo unaona ujanja? We jembe ila butu, njoo upate makali hapo biafra!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kama michango hii ina-reflect upeo wa WANACHADEMA, basi CCM ina haki ya kushinda miaka 50 ijayo! Mawazo ya kijinga kama ya majority ya wachangiaji kwenye thead hayawezi kuachiwa yasogelee ikulu!
 
Kama michango hii ina-reflect upeo wa WANACHADEMA, basi CCM ina haki ya kushinda miaka 50 ijayo! Mawazo ya kijinga kama ya majority ya wachangiaji kwenye thead hii hayawezi kuachiwa yasogelee ikulu!
 
Kwa kuwa si wote tuijuao vizuri katiba ya CUF, ningeshauri tusaburi tuone sakata hili mwisho wake, naamini waakuwa makini sana maana kushughulikia watu 14 si mchezo
 
Mtatiro amefuata nini zanzibar? Naona yeye ni naibu bara maana yake wa zanzibar yupo sasa inakuaje hapo? Ufafanuzi tafadhali!
 
Kama michango hii ina-reflect upeo wa WANACHADEMA, basi CCM ina haki ya kushinda miaka 50 ijayo! Mawazo ya kijinga kama ya majority ya wachangiaji kwenye thead hayawezi kuachiwa yasogelee ikulu!

Hayo mawazo ya kierevu ya wana-CUF yanakisambaratish chama, kwishney kabisa huku bara.
 
Mtatiro, mbona umehukumu tayari katika taarifa yako? Sidhani kama hii ndo "HAKI SAWA KWA WOTE"

Hii inaweza kuitwa "HAKI SAWA KWA WAFUASI WA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD"

Mnazidi kupotea na kuwapotezea dira Wazanzibari.
 
Mtatiro,
Fanya kazi yako banaa hawa wote ni kama wachambuzi tu wa mambo lakini mwisho wa siku watataka taarifa kutoka kwako ili wajue kinachoendelea. Kwani hawajui Ajira bora ni ile ya kutaka nchi yako isonge mbele kwa amani na utulivu...............! Weee piga kazi !
 
Back
Top Bottom