Maamuzi ya kamati ya utendaji ya CUF - Taifa (kikao kimemalizika leo Zanzibar)

Jun 20, 2009
45
225
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Wananchi (CUF) imefanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar tarehe 30 – 31 Desemba, 2011 chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.


Pamoja na kujadili ajenda kadhaa za kawaida kuhusiana na mambo ya utendaji katika Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa pia ilipata nafasi ya kupokea taarifa ya kina kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama kutoka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Nidhamu na Maadili. Taarifa hiyo ilijikita zaidi katika njama zinazoendeshwa na wanachama 14 wakiongozwa na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed zenye mwelekeo wa kutaka kukivuruga Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna hoja za msingi na ushahidi wa kutosha dhidi ya wanachama hao 14 unaoonesha kuhusika kwao na njama hizo. Wanachama hao ni:

1. Hamad Rashid Mohamed2. Doyo Hassan Doyo
3. Shoka Khamis Juma
4. Juma Said Saanani
5. Yasin Mrotwa
6. Mohamed Albadawi
7. Mohamed Masaga
8. Doni Waziri
9. Yusuf Mungiro
10. Nanjase
11. Ahmed Issa
12. Tamim Omar
13. Amir Kirungi
14. Ayubu Kimangale

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kifungu cha 63 kinachozungumzia Wajibu wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kifungu cha 63 (1) (d) kinafafanua wajibu huo kuwa ni “kulinda na kuendeleza heshima ya Chama na Serikali zote halali za nchi.” Kifungu cha 63 (1) (j) kinaelezea wajibu mwengine kuwa ni “kuwachukulia hatua za nidhamu viongozi na wanachama wanaoshutumiwa kwa makosa mbali mbali kwa kufuata masharti ya Katiba hii na kanuni zitakazotungwa mara kwa mara kwa mujibu wa katiba hii.”

Kwa kuzingatia hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeridhika kwamba kuna haja ya kutumia uwezo iliopewa chini ya kifungu cha 62 (1) cha Katiba ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ili kutafakari hali hiyo, kusikiliza tuhuma zinazowakabili wanachama hao, kuwapa nafasi ya kuwasiliza na kujitetea na kisha kuchukua hatua kama litakavyoona inafaa.

Kikao hicho cha Baraza kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika Zanzibar, tarehe 04/01/2012 katika ukumbi wa hoteli ya Mazson.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawaomba wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kutoa nafasi kwa vikao vya Chama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama.


HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na;

JULIUS MTATIRO,
NAIBU KATIBU MKUU (TANZANIA BARA),
KATIBU WA KAMATI YA UTENDAJI TA TAIFA (CUF NATIONAL CENTRAL COMMITTEE).
31 Disemba 2011,
ZANZIBAR.
 
..nadhani chama chenu ni cha visiwani tu.

..huku bara hamna habari nako.

..Hamad Rashid yuko right kwamba chama kimejikita PEMBA tu.
 
​kwani makao makuu yenu ni zanzibar au mpaka mumfuate maalim alipo yani sijaona chama ambacho viongozi wa juu ni maboya na wanaburuzwa na mtu mmoja kama nyini CUF
 
Mtatiro,

..achana na huo ugomvi wa Wapemba.

..utatumika tu hapo lakini mwisho watakutupa.

..jifunze yaliyotokea kwa James Mapalala.

..hivi huoni Mtanganyika mwenzako Nguyuru Lipumba alivyojiweka pembeni? hivi unafikiri yeye ni mjinga?
 
Julius Mtatiro,

Asante san a kwa taarifa hizi. Kuna Hama gani ya kuitisha kikao wakati majibu mnayo?!. Mie naona kuwa hizi pesa za kuendeshea vikao mngeelekeza kwenye kujenga chama chenu Zanzibar (exclude Pemba) na Bara!?.

naomba nikupe yatakayotokea kwenye hicho kikao. Mtawafukuza baadhi na wengine watapata onyo Kali.
 
Ila Mtatiro Kama huna AJIRA sio mbaya endelea nao tu. At the end of the day mkono lazima uende kinywani wala sikulaumu.
 
Eti 'kulinda na kuendeleza heshima ya serikali zote halali za nchi'

Kumbe CUF ni mlinzi na mwendelezaji wa mambo ya CCM, for that matter cuf is another ccm
 
Mtatiro hakuna cha kumfanya Hamad Rashid,wala hamtamuweza kwa lolote maamuzi magumu waachieni CDM,mmeona NCCR wamedandia style ya kufanya maamuzi wameshaanza kumeguka leo ninyi mtaweza kitu gani,najua mnaogopa pia nguvu ya Hamad Rashid,hiyo tarehe 4 mtafanya kitu gani?,lishaharibikiwa tangu ,livyokubali kuolewa na CCM,mlipokubali kuwa CCM B tu tayari mkajimaliza mtajua wenyewe,na wewe Julius ulipote njia huko hapakufai
 
Ndugu mtatiro so what??? Anyway what did u want to tell us? Quoting ur ccm merged constitution??
 
Hivi CUF Katibu Mkuu ndio anaongoza vikao? nini kazi ya mwenyekiti? na hata kama mwenyekiti hayupo hakuna makamu wake?
 
ndugu mtatiro vipi suala la barua zilizowasilishwa na hamad mlisahau kulijadili?
 
Mtatiro nimekufurahia gafla! Wewe ndiye alama halisi ya wanasi-hasa wetu. Unatumwa kuzungumza(na unazungumza ofkoz) hata kile ambacho ww mwenyewe hukiamini. YOU ARE JUST LIKE A BAMBOO FLUTE,JUST BLOW OUT AIR,IT WILL SOUND! kisa? Mkono uende kinywani! Najua wajua you have been used. Now get ready to be refused.
 
Hivi CUF Katibu Mkuu ndio anaongoza vikao? nini kazi ya mwenyekiti? na hata kama mwenyekiti hayupo hakuna makamu wake?

kikao cha kamati tendaji sikuzote kiongozi wake ni katibu, iwe chama chochote duniani, tofauti tu ya majina ya hizo kamati. Baraza kuu la cuf ndo hiyo tarehe 4 atakuwa makamu mwenyekiti nadhani nimekujibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom