Maamuzi na effects zake!

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,107
2,506
Nimejifunza kitu kimoja:
Kila uamuzi una matokeo yake, maamuzi hasi huzalisha tokeo hasi na maamuzi chanya huzalisha tokeo chanya. Baba wa Taifa alilizungumzia suala la Azimio la Arusha kwamba halina mahala ambapo kuna kasoro, kumbe lile lilikuwa ni kuwapima maadili ya Viongozi na utendaji wao wa kazi, sasa leo Azimio la Arusha hakuna na lilifutwa kipindi cha Mwinyi, kile kitendo cha kufutwa kule ndiko kumepelekea kupata viongozi dizaini ya sasa maana hakuna kitengo kinachoshughulikia usafi wa kimaadili na utendaji wa viongozi, matokeo yake tunaona wazi nchi inavyoelekea kwenye direction ya uharibifu mkubwa. Ni kweli tunatakiwa kuwa makini sana katika maamuzi juu ya mustakabali mzima wa nchi maana effects zake zaweza tokea katika muda wowote ule na kwa kiwango chochote kile. Tukiangalia kila awamu na maamuzi yaliyofanyika yawe mazuri au mabaya, utaona kwamba yaliyo mabaya yameifunika yaliyo mazuri. Sijui Viongozi kama wanafundishwa au kukumbushwa juu ya Kutengeneza maamuzi makini "DECISION MAKING", maana naona kama wanajiamulia tu bila kufuata principle zinazotakiwa kufuatwa!
Ni hayo tu.
 
boringly overprolixly statement much to its nebulousness, and consequently I have completely failed to extract any point.
 
Back
Top Bottom