William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,374
- Thread starter
- #41
Kwanza naungana na mjumbe aliyetangulia hapo juu Sn2139 kuwa kwa siku mbili tatu zilizopita umejishushia heshima mbele ya members wengi waliokuwa wanakuheshimu nikinukuu swali lako moja ulilomuuliza Slaa 'Kabla ya wewe kukuita fisadi tuambie huo mshahara wako kweli unatoa kodi kama si fisadi ni nani' tuachane na hayo.
Nampongeza sana Mh.Lowassa kwa kuwaonyesha wabunge wenzake na watanzania kuwa si lazima kila siku kuipongeza serikali kuna wakati inatakiwa kukosolewa inapokwenda kinyume na kikosoa si kuwa umekuwa mpinzani. Kwenye maelezo yako umesema Lowassa alisema maamuzi magumu ni pamoja na kutafuta madeni zaidi nafikiri hiyo sentensi si ya Lowassa ni yako mzee sijawahi kuisikia kutoka kinywani mwa Lowassa.
Ukisoma vizuri ujumbe wako sehemu nyingi unailaumu serikali kwa kutotekeleza wajibu wake umesema haina cha kuonyesha, umeme hakuna ukusanyaji kodi umeoza lakini cha ajabu unaishia kumlaumu Lowassa kana kwamba yeye bado yuko madarakani unashindwa sijui kama ni technical kuwa pin point wahusika wakuu wanaosababisha hayo yote.
Lengo lako lilikuwa kuonyesha Lowassa amekosea aliposema serikali inashindwa kufanya maamuzi magumu lakini umeshindwa kujenga hoja na matokeo yake umeanza kumvika Lowassa matatizo ya serikali kana kwamba yeye ndiye ameyasababisha ili kufikia malengo yako yaliyoshindwa ya kumlaumu Lowassa. Binafsi nilipoona heading 'Maamuzi magumu the biggest joke' nikadhani unaongelea ugumu wa CCM kujivua gamba kuwa ni joke of the Century.
- Kasome tena hotuba ya Lowassa mkuu, huwa hatukurupuki!
Willie @ NYC, USA.