Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
PELVIC INFLAMATORY DISEASES.jpg


Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.



PID husababishwa na nini?

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.


Je mwanamke huambukizwaje PID?


Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
  • Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
  • Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
  • Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
  • Pia kutapika
Vipimo vya PID
Ili kuweza kutambua kama mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo
  • Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
  • Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa Full Blood Picture.
  • Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture
  • Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono.
  • Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.
Matibabu
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa. Hata hivyo ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali ambayo imewekwa na wizara au mamlaka za afya zinazohusika. Miongozo hii hutofautiana kati ya sehemu na sehemu au nchi na nchi, ingawa kiujumla Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo limeweka muongozo wake kwa ajili ya kufuatwa na nchi mbalimbali.

Miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.
Ieleweke pia haishauriwi kujinunulia na kutumia dawa hizi bila kupata ushauri ushauri wa mtaalamu wa afya. Aidha ili kuondoa maumivu na kushusha homa, dawa kama Paracetamol (Panadol) yaweza kutumika.


Jinsi ya kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi


Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na

  • Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kama ikiwezekana kujizuia kabisa kufanya ngono.
  • Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa
  • Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).
  • Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.


Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Wadau naomba kujua chanzo,dalili na jinsi ya kuzuia tatizo hili la PID(pelvic infections).Madaktar au yeyote mwenye ujuz naomba msaada wenu
 
[FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]Pelvic inflammatory disease(PID) inasababishwa na infection kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.PID inasababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wanake na hatimae kupelekea majeraha yasiyorekebishika kwenye mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi ,mayai au hata viungo vingine vya uzazi.Matatizo haya yanaweza kupelekea hata ugumba.[/FONT]

Nini inasababisha ugonjwa huu?
[FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]​Kawaida (Cervix)mlango wa uzazi unazuia bacteria wanaotoka kwenye uke kuingia kwenye viungo via uzazi.
Kama mlango wa uzazi umeathirika na magonjwa ya zinaa kama kisonono au klamidia,mlango huo unapata infections/unadhurika na hatimae kushindwa kuzuia vijidudu kutoka kwenye uke kusambaa kwenye kizazi.Magonjwa kama kisonono na klamidia ndio yanasababisha kwa asilimia 90%.Sababu nyingine ni kutoa ujauzito/mimba,kuzaa/kujfungua na uchunguzi wa kwenye eneo hilo(kimatibabu)
[/FONT].
cervix.jpg
[FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]
Dalili zake ni zipi:
[/FONT]
  • Maumivu kwenye eneo la chini/juu la tumbo
  • Kutokwa na "Vaginal disharge" zenye rangi ya njano au kijani na zenye harufu isio ya kawaida
  • Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • Homa kali
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu wakati wa kujamiiana
Mambo yanayomuweka mwanamke katika kundi la kupata PID

  • Wanawake wenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono na klamidia
  • Wanawake walopata maabukizi ya PID awali,wana athari kubwa ya kupata gonjwa hilo tena
  • Wanawake walio "SEXUALLY ACTIVE"
  • Wanawake walio na wenza wengi,zaidi ya mmoja.






 
Pelvic inflammatory disease(PID) inasababishwa na infection kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.PID inasababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wanake na hatimae kupelekea majeraha yasiyorekebishika kwenye mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi ,mayai au hata viungo vingine vya uzazi.Matatizo haya yanaweza kupelekea hata ugumba.

Nini inasababisha ugonjwa huu?
​Kawaida (Cervix)mlango wa uzazi unazuia bacteria wanaotoka kwenye uke kuingia kwenye viungo via uzazi.
Kama mlango wa uzazi umeathirika na magonjwa ya zinaa kama kisonono au klamidia,mlango huo unapata infections/unadhurika na hatimae kushindwa kuzuia vijidudu kutoka kwenye uke kusambaa kwenye kizazi.Magonjwa kama kisonono na klamidia ndio yanasababisha kwa asilimia 90%.Sababu nyingine ni kutoa ujauzito/mimba,kuzaa/kujfungua na uchunguzi wa kwenye eneo hilo(kimatibabu)
.
View attachment 157152

Dalili zake ni zipi:


  • Maumivu kwenye eneo la chini/juu la tumbo
  • Kutokwa na "Vaginal disharge" zenye rangi ya njano au kijani na zenye harufu isio ya kawaida
  • Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • Homa kali
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu wakati wa kujamiiana
Mambo yanayomuweka mwanamke katika kundi la kupata PID

  • Wanawake wenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono na klamidia
  • Wanawake walopata maabukizi ya PID awali,wana athari kubwa ya kupata gonjwa hilo tena
  • Wanawake walio "SEXUALLY ACTIVE"
  • Wanawake walio na wenza wengi,zaidi ya mmoja.
Asante kwa maelezo,na tiba yake huwa ni nini?
 
Habari zenu wadau, madokta wa jf ninaombeni msaada kuhusu hilo gonjwa hapo juu,mimi binafsi silielewi hili gonjwa vizuri,ila mdogo wangu anasumbuliwa na huu ugonjwa kwa muda mrefu,mimi alichonieleza ni kwamba kila anapokutana kimwili na mume wake anapata u.t.i na anatokwa maji maji mengi ukeni,amehangaika sana hospital bila mafanikio na alimpata specialist mmoja huko kerege akaambiwa kwamba ni bacteria ndio wameshambulia maeneo ya kizazi,walimpatia dawa akapata nafuu sasa hivi vimerudi upya tena,naombeni msaada wenu madokta au kama kuna anaemfahamu specialist mzuri wa magonjwa hayo tumuelekeze,maana ndoa yake ipo hatarini mume kachoka kunywa dawa za u.t.i kila mara. Naomba mnisamehe kwa uandishi mbaya natumia kimeo.
 
Habari zenu wadau, madokta wa jf ninaombeni msaada kuhusu hilo gonjwa hapo juu,mimi binafsi silielewi hili gonjwa vizuri,ila mdogo wangu anasumbuliwa na huu ugonjwa kwa muda mrefu,mimi alichonieleza ni kwamba kila anapokutana kimwili na mume wake anapata u.t.i na anatokwa maji maji mengi ukeni,amehangaika sana hospital bila mafanikio na alimpata specialist mmoja huko kerege akaambiwa kwamba ni bacteria ndio wameshambulia maeneo ya kizazi,walimpatia dawa akapata nafuu sasa hivi vimerudi upya tena,naombeni msaada wenu madokta au kama kuna anaemfahamu specialist mzuri wa magonjwa hayo tumuelekeze,maana ndoa yake ipo hatarini mume kachoka kunywa dawa za u.t.i kila mara. Naomba mnisamehe kwa uandishi mbaya natumia kimeo.


UGONJWA WA KWENYE MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PELVIC INFLAMATORY DISEASES)



MAAMBUKIZI ugonjwa wa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke (Pelvic Inflamatory Diseases) ambao pia hujulikana kama shingo ya uzazi (kitaalamu huitwa cervix) ambayo hujulikana kwa jina la cervicitis hutesa sana wanawake wengi wenye umri mbalimbali.


Maambukizi hayo husambaa hadi kwenye mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia Trachomatis ndivyo vinavyosababisha ugonjwa huu kwa akina mama na wataalamu huuita Pelvic Inflamatory Diseases (PID) yanayotokea kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa huu, njia hizo ni pamoja na kufanya ngono isiyo salama, maambukizi ya njia ya uzazi hasa baada ya kujifungua.
Wanawake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama, wana uwezekano wa kupata maambukizi au wale ambao mimba hutoka (miscarriage) au wakipewa damu iliyo na vimelea vya maambukizi.
Dalili za ugonjwa huu
Dalili za ugonjwa huu wa PID ni nyingi kama vile mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu, kupata maumivu ya mgongo au mwanamke kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.
Kuna dalili nyingine kama vile kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa. Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi na mgonjwa kuwa na homa na kuhisi kichefuchefu au kutapika.
Mwanamke aliyeambukizwa maradhi haya ya maambukizi, anaweza kufanya vipimo kwa kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba.
Mkojo huchunguzwa na darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi.
Kuna kipimo kiitwacho kitaalamu Full Blood Picture hutumika ili kujua aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na maambukizi hayo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha.
Daktari anaweza kujua kama mgonjwa ana maradhi haya kwa kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture.
Mgonjwa pia anaweza kufanya vipimo vingine ili kujua kama ana maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono. Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yoyote katika mfumo wake wa uzazi.
Matibabu
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ana magonjwa hayo, atatibiwa na dawa za jamii ya antibayotiki ili kuua vimelea vya ugonjwa.
Dawa za maradhi haya zipo nyingi kama vile Cefoxitin pamoja na Doxycycline, Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin nakadhalika. Tunashauri kuwa dawa hizi zinunuliwe kwa kushauriwa na daktari.
Ushauri
Kuna njia kadhaa zinazoshauriwa kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi kama vile kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kujizuia kabisa kufanya ngono, kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza na kupimwa vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Asante sana MziziMkavu tutakutafuta sasa nimeelewa kuhusu huu ugonjwa, amepima vipimo vyote H.i.v magonjwa ya zinaa hamna yani anakunywa dawa mpaka anasema nyingine hazikumbuki hata majina.
 
Last edited by a moderator:
Pid ni tatizo linalo sababishwa na untreated u.t.i inayosababishwa na bacteria. Yaan ktk stage hiyo hiyo bacteria wanakua wamesha fika kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia ovary na mirija ya uzazi.. hali hii usababisha hizi sehem kupata chronic inflamation...pia ureter na figo zinakua ktk mashambulizi ya bacteria hao....

Ushauri;
Aende kupima ili kubaini exactly ni aina gan ya bacteria pia kufanyiwa sensitivity kwa dawa tofauti ili kubain best dawa ya kumpa...asikimbilie antibiotics ovyo kwan ndo zinaweza kuongeza tatizo... see lab scientists atasaidia zoezi hili..
 
Na kama kisha kunywa madawa ovyo inaelekea hao bacteria wame develop multidrug resistance... nadhan inahitajika sayansi nzito ya kimaabara ya kubaini combination ya dawa zitazo saidia yy kupona....kama tatizo litaendelea kuzembewa meanz atapoteza hata uwezo wa kuzaa
 
Asante mkuu,sasa unamshauri aende hospital gani maana sasa hivi mumewe hana ushirikiano kiivyo anakuwa km anamnyanyapaa.
Na kama kisha kunywa madawa ovyo inaelekea hao bacteria wame develop multidrug resistance... nadhan inahitajika sayansi nzito ya kimaabara ya kubaini combination ya dawa zitazo saidia yy kupona....kama tatizo litaendelea kuzembewa meanz atapoteza hata uwezo wa kuzaa
 
HABARI ZA LEO WAPENDWA.

Leo napenda tujifunze somo liitwalo MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA uzazi(pelvic inflammatory Disease-P. I.D).

P. I. D ni nini?
-niugonjwa ambao hushambulia mfumo wa uzazi wa mwanamke, ni mijawapo ya magonjwa yanayoambukizwa kwa Njiaa ya kujamiiana kwa wanawake.

SEHEMU ZINAZO ATHIRIWA
1.mfuko wa uzazi
2.ovary
3.milija ya falopia,pamoja na sehemu nyinginezo Katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

>kwakawaida mlango wa uzazi huzuia bacteria kuingia katika mfumo wa uzazi wanaokuja kupitia utupu WA mwanamke amabao wadudu hao husambaa mpaka ndani ya mfumo wote sasa kama mwanamke ataambukizwa na magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende, namengine mlango wa uzazi nao unakuwa umeathiriwa na hautakuwa na uwezo WA kuzuia bacteria hao au itakuwa inakiwango kidogo cha kuzuia wadudu hao.

Kwa ufupi ugonjwa huu husababishwa Na mwanamke kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.

SABABU NYINGINE ZA UGONJWA huu
1.utoaji wa mimba usio salama
2.hata wakati wa kujifungua kusiko salama.

DALILI ZAKE

-maumivu makali ya tumbo au maeneo ya chini ya tumbo au maumivu sehemu ya juu ya upande wa kulia mwa tumbo
2.uke kuvuja au kutokwa na uchafu wa njano au kijani na ukiwa na harufu
3.maumivu wakati WA kukojoa
4.homa Kali
5.kutapika pamoja na chafya
6.maumivu makali wakati wa kujamiiana
7.kuwashwa maeneo ya uke ndani na NJE

MADHARA KTK UZAZI YATOKANAYO NA MAAMBUKIZI KTK UZAZI

-kuvurukika kwa mpangilio wa homoni (hormones imbalance)
-michubuko na kuziba kwa milija ya falopia
-kuwa na mzunguko mfupi au kukosa kabisa
-husababisha uvimbe kunako milija, mfuko wa uzazi na eneo lote la via vya izazi.

NAMNA YA KUJIKINGA

-kuacha ngono zembe
-kuwa na mpenzi mmoja
-epuka matumizi ya pombe
-kuwa na usafi au kuzingatia usafi na kufanya vipimo Mara kwa mara

MATIBABU
-Mara utakapo jisikia dalili tajwa hapo juu nenda hospitali dakitali atakufanyia vipimo kama vile, vipimo vya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kipimo cha damu ,kipimo cha pelvic na matiti, kipimo cha ultrasound, nakadharika

Usiogope ugonjwa huu unatibika muone dactari
Asanteni by Dr Patrick and Francisco.



Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa somo,naomba ufafanuzi kuhusu matumizi ya pombe na PID.

Sent from my HUAWEI Y541-U02 using JamiiForums mobile app
 
Hayo magonjwa ndiyo hunifanya nifunge breki linapokuja suala la kungonoka. Unangonoka dakika kumi unajutia maisha yako yote....

Kama naogopa hata kuumwa kichwa tu, itakuwaje nitakapoumwa kaswende?...hapana kwa kweli. Mungu aepushie mbali
 
NINI MAANA YA PID?
PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Kwa kawaida maambukizi haya yanahusisha mji wa mimba( uterus), shingo ya kizazi(cervix), mirija ya kupitishia mayai ya mwanamke(fallopian tubes) na sehemu yanapozalishwa mayai haya(ovaries).


PID HUSABABISHWA NA NINI HASA?

Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wa magonjwa ya zinaa hususani gonorrhoea na chlamydia.

MWANAMKE ANAUPATAJE UGONJWA HUU WA PID?

mwanamke ataupata ugonjwa huu kupitia mambo yafuatayo:-
1. Kupitia ngono uzembe( holela).
2. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja.
3. Kufanya mapenzi bila kutumia kinga(condom).
4. Kupitia magonjwa ya zinaa hususani kaswebde na kisonono.
5. Kupitia kunyonywa ukeni mara kwa Mara.
6. Kuweka vitu ukeni ili kuufanya uke ubane au upendeze kumvutia mpenzi wake.
7. Utoaji wa mimba halafu kukosa usafishaji mzuri baada ya kuitoa.
8. Kupitia njia ya kujifungua kama wakunga hawakuwa makini.
9. Kutumia madawa na njia za kuzuia mimba kama vijiti na sindano.
10. kupitia UTI sugu.

DALILI ZA UGONJWA HUU NI ZIPI?
Mwanamke atagundulika kuwa na PID kama atakutwa na dali zifuatazo:-
1. Maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu.
2. Kupata homa za mara kwa Mara.
3. Kutokwa na uchafu wenye harufu wa rangi ya maziwa mgando, kijani au njano.
4. Kupatwa na hali ya kichefuchefu na kutapika pia.
5. Kupata maumivu wakati wa tendo LA ndoa ( kujamiiana).
6. Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana.
7. Kuumwa mgongo mara kwa mara.
8. Kutokwa na usaha ukeni wakati mungine.
9. Kupata maumivu wakati wa kukojoa.

MADHARA GANI HUMPATA MWANAMKE MWENYE UGONJWA HUU?

Kama mwanamke atapatwa na PID halafu akashindwa kutibiwa mapema, madhara yafuatayo yanaweza kumtokea:-
1. Kupatwa na tatizo la hormone imbalance.
2. Mirija ya uzazi itaziba na hivyo kushindwa kupitishia mayai yaliopevuka ili kurutubishwa.
3. Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwasababu ya hormone imbalance.
4. Uchi ( uke) kukauka mara kwa Mara.
5. Mzunguko wa hedhi(period) kubadilik mara kwa mara.
6. Wakati mungine hukosa kabisa period kwa muda mrefu.
7. Kupata Kansa ya shingo ya kizazi kutokana na kushambuliwa na bacteria.
8. Mimba kutungwa nje ya kizazi(ectopic prengancy) baada ya kizazi kuharibika.
9. Kukosa ute wa ovulation unaoashiria siku maalum za kupata ujauzito.
10. Kuharibika mirija ya uzazi.
11. Mwanamke atapata ugumba kama atashindwa kupata tiba sahihi kwa muda muafaka.


MUHIMU:-

1. Ugonjwa huu ni hatari sana kwa afya ya mwanamke hivyo basi inafaa kulinda afya ya uzazi ili kuepuka madhara ambayo nimeyataja hapo huu.
2. Ugonjwa huu unatibika kabisa kama utachua hatua mapema.

Kwa ushauri na tiba zisizo na madhara wala kemikali tafadhali unaweza kuniona kupitia WhatsApp namba yangu 0656069644.
 
PID maambukizo kwenye via vya uzazi, maambukizi haya yanasababishwa na vimelea aina ya NEISSERIA, GONORHOEA, CHLAMYDIA, TRACHOMATIS ndivyo vinavyoongoza kusababisha PID kwa wanawake.
NJIA ZINAZOSABABISHA PID;
1.kutoa mimba(abortion)
2.matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama vidonge, kondom, kitanzi nk.
3.kukaa na infection kama u.t.i na fangasi kwa muda mrefu

DALILI ZA PID
1.kutokwa uchafu mweupe kama maziwa mtindi sehemu za siri wakati mwingine inawezakuwa rangi ya kijani, kahawia brown hata njano.
2.maumivu chini ya kitovu , nyonga na kiuno
3.maumivu wakati wa tendo la ndoa
4.kukosa hamu ya tendo la ndoa.

MADHARA YA KUKAA NA PID KWA MUDA MREFU
1.kizazi kulegea
2.uvimbe kwenye mayai(ovarian cysts)
3.homon kushindwa kubalance (homonal imbalance)
4.kizazi kujaa maji maji mpaka kulowanisha nguo ya ndani
5.saratani ya shingo ya kizazi
6.mimba kuporomoka (miscarriage)
7.ugumba (infertility)

FOR BETTER LIFE
 
PID maambukizo kwenye via vya uzazi, maambukizi haya yanasababishwa na vimelea aina ya NEISSERIA, GONORHOEA, CHLAMYDIA, TRACHOMATIS ndivyo vinavyoongoza kusababisha PID kwa wanawake.
NJIA ZINAZOSABABISHA PID;
1.kutoa mimba(abortion)
2.matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama vidonge, kondom, kitanzi nk.
3.kukaa na infection kama u.t.i na fangasi kwa muda mrefu

DALILI ZA PID
1.kutokwa uchafu mweupe kama maziwa mtindi sehemu za siri wakati mwingine inawezakuwa rangi ya kijani, kahawia brown hata njano.
2.maumivu chini ya kitovu , nyonga na kiuno
3.maumivu wakati wa tendo la ndoa
4.kukosa hamu ya tendo la ndoa.

MADHARA YA KUKAA NA PID KWA MUDA MREFU
1.kizazi kulegea
2.uvimbe kwenye mayai(ovarian cysts)
3.homon kushindwa kubalance (homonal imbalance)
4.kizazi kujaa maji maji mpaka kulowanisha nguo ya ndani
5.saratani ya shingo ya kizazi
6.mimba kuporomoka (miscarriage)
7.ugumba (infertility)

FOR BETTER LIFE
TIBA......?
 
Back
Top Bottom