Maalim Seif, vipi tena?

Mwiba,
Mkuu wa ngu yaani wewe unataka kiongozi anayeweza kusema fulani ni MPUMBAVU!.. hiyo sifa gani ya uongozi kama sio ujuha wake..Na nakuhakikishia hakuna mtu mbaguzi kama Sief ukisoma taarifa zake zote ni habari za Utenganishi mtupu...
Ubaguzi wa Maalim Seif unakwenda katika kumbukumbu tokea akiwa Waziri wa Elimu katika SMZ, aliyofanya pale yalitisha na hata pale alipowekwa benchi, baada ya kuondolewa kama Waziri Kiongozi, alitumia muda wake mwingi kupandikiza ubaguzi kati ya Waunguja na Wapemba.

Watunza kumbukumbu wanasema kuwa Maalim Seif aliandaliwa mahsusi na baadhi ya wazee wa Kipemba kupandikiza ubaguzi huu ambao kwa sasa upo wazi na unazidi kukomaa kila kukicha, na unaweza kuuona hata hapa JF kwa jamaa zangu wa kisiwa cha pili.
 
Ndio akapewa uwaziri kiongozi ,hivi unafahamu kuwa Seif alikuwa mshaur wa Nyerere kuliko mtu yeyote hapa Tanzania ,ndivyo wanavyosema watunza kumbukumbu.
 
Maalim Seif na baadhi ya wenzake wa karibu wana madeni makubwa kutokwa kwa watu mbalimbali ambapo wamekuwa wakipewa fedha kwa ajili ya chaguzi zilizopita. Ahadi ya kurudisha pesa hizo ilikuwa ni kwamba wakishapata serikali tu watayalipa madeni hayo. Hayo madeni yaliedelea kukopwa hadi kwa wananchi wa kawaida kabisa.
Kwa mfano kuna kiongozi mmoja mkubwa hapo ndani ya CUF ambaye Mkapa alimpa ubunge wa kuteuliwa, wakati wa uchaguzi wa 1995 alitoa pesa yake 700m/= akitumaini ingerudi haraka baada ya kukamata serikali lakini haikuwa hivyo. Sasa sijui alilipwa vipi kutoka kwenye ruzuku haijaeleweka kwani hivi vyama haviweki mahesabu wazi for some reasons, wanaficha, halafu wakati huohuo wanataka serikali ili waongoze nchi.

Uongo namba moja huu! vinginevyo thibitisha
 
You poor Zanzibari's,
Nani aliwaloga? nani aliwaambia mkombozi wenu atatoka Sisi M?
Mimi niliposikia tangu mwanzo msanii anawadanganya na mnakubali nilijua mmelambishwa galasha.
Ningelikuwa ni mimi kiongozi tangu siku zote mnapomkimbilia kwa tofauti katika mwafaka, ningesha jitoa kwenye upuuzi huo manaouita mwafaka.
Kikwete ni msanii na atabaki hivyo hata akipambwa vipi na wasanii wenzake.
Hamuoni hata huyo muasia wa kwenu kafyata mkia? siku hizi haisemei tena sirikali ya mapinduzi kama zamani!
 
Wananchi,

Hapa, baada ya kusoma hiyo hutuba ya Maalim Seif na kwa bahati nilishasoma hotuba ya Kikwete na haya maoni yetu humu, mmii naona kinachozungumzwa mwote humo ni ushabiki wa vyama.

Kikwete kashabikia CCM, Maalim Seif anashabikia CUF na Pemba chini ya mwamvuli wa Zanzibar na sisi watoa maoni tumo katika kuitikia, Amin!

Tatizo hapa ni (a) Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo imekaa katika mkao wa CCM kula nchi milele (b) Serikali ya Zanzibar imekaa mkao wa Ubwana na kuifanya Pemba Mtwana wake na (c) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umekaa mkao wa kutokueleweka kwa wengi wa Tanganyika na wa Zanzibar.

Ni kweli kabisa hata CUF na CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa kisichokuwa CCM wabadilishe wagombea kila mwaka wa Uchaguzi Mkuu, hawawezi kupata ushindi wa kuongoza serikali wala bunge chini ya mtindo na hali ya uchaguzi iliopo.

Absolute power which CCM has corrupts absolutely. CCM imelewa madaraka na chini ya utawala wake tutaendelea na UJINGA, MARADHI, UMASIKINI, RUSHWA na UFISADI. It does not matter if at the helm anakaa mtu gani. Tutawalaumu watu binafsi kama Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Karume na mwingine yeyote ajaye mpaka tuchoke.

Kama tunataka mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi ni lazima CCM na Katiba iliyopo vibadilike. Hatuwezi kufanikiwa kama tutaendelea kushabikia siasa kama tunavyoshabikia mpira wa miguu. Muundo wa muungano ubadilike, tuwe na nchi moja na serikali moja au tuwe na serikali tatu, ya Zanzibar, ya Tanganyika na ya Shirikisho. Na mwisho wa Unguja waache mambo ya kuwafanya wa Pemba ni watwana wao. Na wa Pemba waachane na huu Uarabu-arabu. Kama mtu anataka uarabu, njia iko wazi na Arabuni nafasi bado ipo.
 
Uongo namba moja huu! vinginevyo thibitisha
Sio rahisi kukudhibitishia iwapo mambo ya ndani ya CUF huyajui. Habari kama hizi unaweza kuzipata ndani ya bar'za za CUF.. Nakumbuka mwaka 1995 wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, niliona mengi toka kwa wapambe wakubwa wa CUF na jinsi walivyokuwa wanajipanga kuchukua nafasi nyeti katika SMZ ili kufidhia michango yao mikubwa mikubwa.

Hali ilikuwa ya kuchekesha zaidi pale matokeo yasio rasmi yalipotangaza kuwa CUF imeshinda uchaguzi ule. Kulifanyika kufuru za aina yake toka kwa wapambe hao, wakitumaini kuwa wakati wa Maalim Seif kulipa madeni/fadhila zao umewadia.
 
Kwaminchi,
Hapa, baada ya kusoma hiyo hutuba ya Maalim Seif na kwa bahati nilishasoma hotuba ya Kikwete na haya maoni yetu humu, mmii naona kinachozungumzwa mwote humo ni ushabiki wa vyama. Kikwete kashabikia CCM, Maalim Seif anashabikia CUF na Pemba chini ya mwamvuli wa Zanzibar na sisi watoa maoni tumo katika kuitikia, Amin!
Mkuu wangu mimi siwezi kusema AMIN bali nawaambia hawa ndugu zangu wafahamu vizuri fika kwamba Sief ni kibaraka tu. mwongo na mnafiki.. kiongozi ambaye sio tu anazungumza kwa manufaa yake binafsi bali pia ni mbaguzi asilia..

Kibunango,
Duh kumbe unakumbuka yale ya wizara ya elimu?.. ilikuwa sooo na ndio hapo Komandoo Salmin alipopatia Ujiko!..Huyu Sief wala sifahamu kwa nini CUF wanambeba wakati ni mzigo tena yawezekana kabisa kuwa ni pandikizi..
 
Kwa mantiki hiyo ataendelea kuwa Seif yule yule. Lakini ajue wazanzibar anayejitia kuwasemea wanabadilika , na hayo anayowaasa wenziwe kuhusu Zanzibar inafaa ajiase mwenyewe kwanza. Kwa kweli sasa Wazanzibari si watu wa kudanganyika tena. Na aanze kuiangalia vizuri hiyo CUF yake kwanza.

Hakika maneno yako. Maalim yeye hasa ndiye kila kitu kwenye CUF, ndugu yetu Prof. Ibrahim yeye amekaa kana kwamba anavizia kitu fulani ambacho mimi hadi leo sikielewi hicho kinachomfanya adhalilike kwa Maalim Seif.

Seif ni yuleyule habadiliki, nakumbuka siku za nyuma Juma Duni Haji alipoanza kutajwa kama mtu mwenye upeo na uwezo wa kuongoza Zanzibar kama rais, Seif alihakikisha kuwa huyu jamaa anadhibitiwa vilivyo.

Lakini kama ilivyo wakati ni ukuta.
 
Sio rahisi kukudhibitishia iwapo mambo ya ndani ya CUF huyajui. Habari kama hizi unaweza kuzipata ndani ya bar'za za CUF.. Nakumbuka mwaka 1995 wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, niliona mengi toka kwa wapambe wakubwa wa CUF na jinsi walivyokuwa wanajipanga kuchukua nafasi nyeti katika SMZ ili kufidhia michango yao mikubwa mikubwa.

Hali ilikuwa ya kuchekesha zaidi pale matokeo yasio rasmi yalipotangaza kuwa CUF imeshinda uchaguzi ule. Kulifanyika kufuru za aina yake toka kwa wapambe hao, wakitumaini kuwa wakati wa Maalim Seif kulipa madeni/fadhila zao umewadia.

Kibunango,

Ahsante sana kwa maelezo yako nadhani umenielewa nini hasa nilichokiongea. Nina hakika wakati wa uchaguzi Mkuu wa kwanza wa kihistoria katika nchi yetu baadhi ya wachangiaji wengine hapa JF walikuwa aidha ni wadogo sana au hawakuwa katika picha kamili ya yale yaliyokuwa yanaendelea. Kuna watu kadhaa wa kadhaa ambao walikopwa na kuhakikishiwa kuwa CUF itashinda kiti cha urais Zanzibar na watarudishiwa pesa zao, habari ambazo nilizonazo wapo baadhi ya watu wameshakata tamaa ya kurudishiwa pesa zao, lakini sijui kama Mh. yule aliyetoa Milioni 700 kama yeye hajarudishiwa japo kiasi kutoka kwenye ruzuku. Mimi nilikataa kutoa kwa sababu ilikuwa ni kamari.

Kwa hiyo Seif anataka kwa hali yeyote ile awe rais au sheria ibadilishwe kwa namna yeyoye ile impatie madaraka japo ya uwaziri kiongozi. Trust me, ule mkutano wa Butiama ulimsononesha sana Seif, ulimchoma msumari wa moto katika moyo wake. Yeye alitegemea kuwa kikao cha Butiama kitaamua in favor of CUF...this guy is a joker...CCM waamue kwa maslahi ya CUF...that will never happen...hata kama mimi ningekuwa Mwenyekiti wa CCM nisinngefanya kosa la karne kama hilo. CUF sasa hivi imekosa mwelekeo kabisa inahitaji viongozi wa kuiondoa hapo ilipo na kuipeleka mbele.
 
Sasa mbona unajikanyaga Seif na madeni wapi kwa wapi,kama huyo mtu alikopesha Chama Cha CUF basi ni kwa mapenzi yake,hivyo kwa mapenzi yake hayo hayo ndio mpaka leo bado yupo CUF na hatujamsikia kupiga makelel ila unampigia wewe.Wanasema pilipili wamekula wengine wewe inakuwashia nini nilifikiri utazungumzia ruzuku wanazopewa kutoka serikalini ,anaekopesha anazo na kama hana basi na uwezo wa kukopesha pia utakuwa haupo,si umeyaona mabenki siku hizi hayatoi mikopo,tuendelee !

Alikopeshwa kama Seif ili aweze kufanya kampeni za urais wa Zanzibar na akishinda atawarejeshea pesa zao.
Na viongozi wengine nao waliombwa waende wakakope na baadhi yao walikopa kwa watu tofauti (Ikiwemo 700m/=). Sasa sijui kama wenyewe walilipwa au ndiyo walikuwa wakiambiwa ...si mnaona tunafanya juhudi kama vile kuendesha muafaka nk. hii inasaidia kumfanya anayekudai atulie kidogo. Kila movement wanayofanya CUF inabeba pia taswira ya 'bado tunashughulikia mambo'
Any way unaweza kijifariji kwa kuyaita maneno yangu vyovyote unavyotaka, lakini hali ndivyo ilivyo.
 
Ndivyo Ilivyo,

Hili la kumwambia Maalim asigombee urais hapo hamtaelewana, yeye ana malengo yaliyojificha kwenye hili la kugombea urais, hawezi kabisa kukubali.

Nani yuko tayari kwa hilo labda mimi na wewe mwenzangu tusioonja tamu ya madaraka. Kwani 2005 kulikuwa na msururu wa namna gani na angalia bado tunalia na EPA> Mwache Sefu na mwengine yeyote afuate utaratibu na wananchi (au dola) itaamuwa nani wa kuwa Rais.
 
Ubaguzi wa Maalim Seif unakwenda katika kumbukumbu tokea akiwa Waziri wa Elimu katika SMZ, aliyofanya pale yalitisha na hata pale alipowekwa benchi, baada ya kuondolewa kama Waziri Kiongozi, alitumia muda wake mwingi kupandikiza ubaguzi kati ya Waunguja na Wapemba.

Watunza kumbukumbu wanasema kuwa Maalim Seif aliandaliwa mahsusi na baadhi ya wazee wa Kipemba kupandikiza ubaguzi huu ambao kwa sasa upo wazi na unazidi kukomaa kila kukicha, na unaweza kuuona hata hapa JF kwa jamaa zangu wa kisiwa cha pili.

Wacha kumsaka Sefu kwa hili. Kibunango kama wewe ni Mzanzibari hebu tueleze Wamakunduchi walifanya nini hapo Wizara ya Elimu kabla ya kuingia Sefu au nini walifanya katika jeshi la Polisi na baada ya hapo hebu tueleze wakati wa Dr. Salmini nini alifanya hata mtu mmoja akawa hazina na sefu la kutunzia pesa na mtu wa upande fulani akihitaji pesa basi anapewa kutoka nyumbani. Baada ya kuingia Karume nini kilichotokea na sasa watu wa Kusini Unguja wanasemaje na Urais wa Zanzibar? Aidha jiulize kiongozi mwengine kutoka Pemba alikuwa vipi kwa Wapemba wenzake kiasi kwamba wasaidizi wake wote wakitoka Pemba.
Huu ni utamaduni wa Visiwani kuwafavour wale wanaotoka kwao kwa hivyo kumchaguwa Sefu tu ni kupotosha ukweli.
 
you poor zanzibari's,
nani aliwaloga? Nani aliwaambia mkombozi wenu atatoka sisi m?
Mimi niliposikia tangu mwanzo msanii anawadanganya na mnakubali nilijua mmelambishwa galasha.
Ningelikuwa ni mimi kiongozi tangu siku zote mnapomkimbilia kwa tofauti katika mwafaka, ningesha jitoa kwenye upuuzi huo manaouita mwafaka.
Kikwete ni msanii na atabaki hivyo hata akipambwa vipi na wasanii wenzake.
Hamuoni hata huyo muasia wa kwenu kafyata mkia? Siku hizi haisemei tena sirikali ya mapinduzi kama zamani!

shida ndio inayowafanya kuokoteza.
 
Hakika maneno yako. Maalim yeye hasa ndiye kila kitu kwenye CUF, ndugu yetu Prof. Ibrahim yeye amekaa kana kwamba anavizia kitu fulani ambacho mimi hadi leo sikielewi hicho kinachomfanya adhalilike kwa Maalim Seif.

Seif ni yuleyule habadiliki, nakumbuka siku za nyuma Juma Duni Haji alipoanza kutajwa kama mtu mwenye upeo na uwezo wa kuongoza Zanzibar kama rais, Seif alihakikisha kuwa huyu jamaa anadhibitiwa vilivyo.

Lakini kama ilivyo wakati ni ukuta.

Punda sikiliza hayo yakusema Seifu ndio kila kitu hayakuanza kwako wala jana au juzi tokea hapo kale ndio maneno wanayoambiwa wanachama wa CUF na kwa kweli hawajabadilika wapo pale pale au hukumbuki ile nyimbo ya ana ndevu wanamwogopa ndie uyuyo ana ndeevu !! Na ni ukweli ambao CCM wanamwogopa Seif Sharif Hamad au Ba Hamadi,kwani hata timu za mpira huwa zinamwogopa mchezaji fulani katika timu ya upinzani,hivyo mcheza aneogopwa wa upinzani ni Seif ,hilo halina mjadala ,maana kuwepo Seif kwenye majukwaa ni mtihani mkubwa kwa CCM.

Usitake kudanganya watu hapa,Juma Duni Haji mwenyewe alipanda kwenye jukwaa na kuapa kuwa hawezi hawezi kupingana na Maalim Seif.akimaanisha na kusema yasemwayo yote ni uwongo alizushiwa ,alisema na nimemsikia kwa masikio yangu,wewe nafikiri hujui ni akina nani walioanzisha CUF na kama hujui huwezi kuwataja baadhi ya watu ambao ni viongozi ndani ya CUF hawafiki hata kumi kuwa watatokea kumpinga Seif au watake aondoke,hilo halipo,kwani wenyewe wanahesabu kuwa Chama chao bado ni kichanga ukilinganisha na CCM,na kwa taarifa yako hao wasiozidi kumi ni marizevu akiwemo Juma Duni iwapo Seif atafikwa na lolote basi atakaeshika bendera ni mmoja kati ya watu hao,mpaka wamehakikisha kile wanachokipigania haki sawa kwa wote kinapatikana na timu yao imeshinda.Na ndio msimamo wao na ndivyo walivyokubaliana,sasa kuleta stori za Juma Duni ni kuwa hamyajui yaliokuwemo ndani ya Core ya CUF. Pole sana.
 
Mkuu Mwiba,
Ahsante kwa maelezo yako. Nilikuwa ninajaribu kueleza yale ninayoyafahamu mimi. Sasa nadhani itakuwa ni vizuri kupinga ninayoyafahamu mimi kwa kuelezea ni yapi mapungufu ya Maalim Seif kama kiongozi wa CUF na yake mwenyewe binafsi. (Huyu ni Kiongozi wa wananchi)

Tueleze ni yapi basi mapungufu ya Maalim Seif?
 
Wacha kumsaka Sefu kwa hili. Kibunango kama wewe ni Mzanzibari hebu tueleze Wamakunduchi walifanya nini hapo Wizara ya Elimu kabla ya kuingia Sefu au nini walifanya katika jeshi la Polisi na baada ya hapo hebu tueleze wakati wa Dr. Salmini nini alifanya hata mtu mmoja akawa hazina na sefu la kutunzia pesa na mtu wa upande fulani akihitaji pesa basi anapewa kutoka nyumbani. Baada ya kuingia Karume nini kilichotokea na sasa watu wa Kusini Unguja wanasemaje na Urais wa Zanzibar? Aidha jiulize kiongozi mwengine kutoka Pemba alikuwa vipi kwa Wapemba wenzake kiasi kwamba wasaidizi wake wote wakitoka Pemba.
Huu ni utamaduni wa Visiwani kuwafavour wale wanaotoka kwao kwa hivyo kumchaguwa Sefu tu ni kupotosha ukweli.
Ngekewa acha kupotisha facts. JF wapo wengi wenye kujua facts za Zanzibar. Wizara ya Elimu iliharibika wakati Seif akiwa Waziri, na Mbarouk akiwa Waziri Mdogo. Hata Pereira na uzoefu wake wote wa Administration aligwaya kuzima njama za Kina Seif, na hakuchukua duru aliondolewa hapo Wizara ya Elimu. Hivi lini Wamakunduchi walileta vituko Wizara ya Elimu. Miaka ipi watoto wa Kipemba waliambiwa kuwa ni mahodari, na tuliwaona wana maliza Form Six hata wakiwa hawawezi kunyoosha uzuri sentensi za Kiingereza? Una nini cha kueleza kuhusu Wizara ya Elimu na uharibifu (au upendeleo) wa Seif?
 
Punda sikiliza hayo yakusema Seifu ndio kila kitu hayakuanza kwako wala jana au juzi tokea hapo kale ndio maneno wanayoambiwa wanachama wa CUF na kwa kweli hawajabadilika wapo pale pale au hukumbuki ile nyimbo ya ana ndevu wanamwogopa ndie uyuyo ana ndeevu !! Na ni ukweli ambao CCM wanamwogopa Seif Sharif Hamad au Ba Hamadi,kwani hata timu za mpira huwa zinamwogopa mchezaji fulani katika timu ya upinzani,hivyo mcheza aneogopwa wa upinzani ni Seif ,hilo halina mjadala ,maana kuwepo Seif kwenye majukwaa ni mtihani mkubwa kwa CCM.

Usitake kudanganya watu hapa,Juma Duni Haji mwenyewe alipanda kwenye jukwaa na kuapa kuwa hawezi hawezi kupingana na Maalim Seif.akimaanisha na kusema yasemwayo yote ni uwongo alizushiwa ,alisema na nimemsikia kwa masikio yangu,wewe nafikiri hujui ni akina nani walioanzisha CUF na kama hujui huwezi kuwataja baadhi ya watu ambao ni viongozi ndani ya CUF hawafiki hata kumi kuwa watatokea kumpinga Seif au watake aondoke,hilo halipo,kwani wenyewe wanahesabu kuwa Chama chao bado ni kichanga ukilinganisha na CCM,na kwa taarifa yako hao wasiozidi kumi ni marizevu akiwemo Juma Duni iwapo Seif atafikwa na lolote basi atakaeshika bendera ni mmoja kati ya watu hao,mpaka wamehakikisha kile wanachokipigania haki sawa kwa wote kinapatikana na timu yao imeshinda.Na ndio msimamo wao na ndivyo walivyokubaliana,sasa kuleta stori za Juma Duni ni kuwa hamyajui yaliokuwemo ndani ya Core ya CUF. Pole sana.
Duni si Mfuasi tu wa Seif, na sijui alipewa fadhila gani na Seif pale alipokuwa Katibu Mkuu Katika Afisi ya Waziri Kiongozi wakati ule Seif alikuwa Waziri Kiongozi. yeye (Duni)alikuwa hana ugomvi na Utawala wa Maalim Idriss na wala na CCM wakati huo lakini aliingia kiringeni kutokana na loyalty yake kwa Sefu na Loyalty hiyo anaendelea nayo hadi leo-Maskini Mshirazi wa Kitumbatu-Zindukana Baba.
 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, kumwomba radhi Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kauli na matamshi yasiyo ya kistaarabu.Pia CCM Zanzibar imevitaka vyombo vya Dola kufuatilia kwa makini kauli zinazotolewa na viongozi wa CUF ambazo zinalenga kuleta vurugu na kuhatarisha amani na utulivu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar ikiwa imesainiwa na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kauli zilizotolewa na viongozi wa CUF katika mkutano wa hadhara wiki iliyopita, zinakwenda kinyume na maadili ya Watanzania kwa kutukana viongozi wa kitaifa hadharani.

Vuai alisema Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad alitoa matamshi ya hatari akimtaka Rais Kikwete 'akome' kuingilia masuala ya kisiasa ya Zanzibar.Aidha, aliwataka wafuasi wa CUF kujiandaa na uchaguzi mkuu mwakani na mdogo wa jimbo la Magogoni, bila kusubiri taarifa ya mtu yeyote.

Katika mkutano huo, pia Seif alisema yeye ndiye anayeijua Zanzibar na si Kikwete ambaye alikuja visiwani hapa kama Ofisa Mdogo wa Makao Makuu ya CCM Kisiwandui.

”Ni kauli mbaya ya kumwambia Rais wa nchi akome … asiwagombanishe wananchi wa Zanzibar na hana ubavu wa kulinda Mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu si Mzanzibari,” alisema Vuai.

Akifafanua, Vuai alisema Rais Kikwete ni Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia Mwenyekiti wa CCM iliyotokana na ASP na TANU, hivyo kulinda Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar ni jukumu lake kisheria na kikatiba.Hivi karibuni, CUF imekuwa ikimshutumu Rais Kikwete kwamba alitoa matamshi ya kuviza demokrasia ya vyama vingi nchini wakati wa ziara yake Pemba mwezi uliopita.

Katika taarifa hiyo, CCM ilisema Rais Kikwete aliwaambia wananchi katika mikutano yake Makombeni kwamba ushindi wa kisiasa wa mtu au chama unaweza kupatikana upesi au kusubiri kwa muda mrefu na si kwamba vyama vya upinzani haviwezi kuunda Dola iwapo vitashinda katika uchaguzi mkuu.

Katika mkutano wa Kibanda Maiti Jumamosi iliyopita, Seif na Mwenyekiti wa CUF, Professa Ibrahim Lipumba, walitumia muda mwingi kujibu hotuba na ziara ya Rais Kikwete aliyoifanya Pemba.

Mkutano huo kwa mujibu wa viongozi wa CUF, ulikuwa maalumu kwa ajili ya kujibu kauli za Rais Kikwete katika ziara yake ya Unguja na Pemba kukagua miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kuzindua baadhi na kusalimiana na wananchi
 
Back
Top Bottom