Mmmm, hii ni rahisi, ila haitaki unafiki. Huku wataka na huku.mbona hili ni rahisi sana; Seif na CUF watangaze kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa; wawaongoze watu wa Zanzibar kutoka kwenye Muungano ili hatimaye Zanzibar iwe nchi nje ya Muungano ipate kiti, meza na kalamu kwenye Umoja wa Mataifa.
Wanamuomba Nani.,??
Hivi vituko! Anaiomba Marekani? Wakikataa je? Njia rahisi ni kuleta mswada BLW ili Zanzibar ipige kura ya maoni kutoka kwenye muungano na kuweka utaratibu wa kugawana mali na madeni kati yake na Tanganyika pamoja na mengineyo.
Pasco, I can't agree with you more!Thanks. Please, allow me to chip in senti sumuni.Sikujua kuwa Maalim Seif naye pia ni mtu wa kujifurahisha!. Kabla Zanzibar haijaomba hicho kiti chake kule UN, "first it has to exist"!. Katika medani za kimataifa, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar!, Zanzibar doesn't exist anymore so does Tanganyika!. Kimataifa nchi ni moja tuu Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya hiyo Tanzania!.
Ili Zanzibar iweze ku reclaim its lost glory, hatua ya kwanza sio kukimbilia kwa big brother na kuomba utambuliwe, bali ni kumwambia partner wako kuwa umemchoka, mvunje kwanza hiyo parneship yenu ya muungano, uwe huru, uwe una exist tena kama zamani, then unabisha hodi UN kwenyewe na sio kwa host wa UN!.
Hivyo ili kukipata kiti chenu, hatua ya kwanza ni kuuvunja muungano na kuirejesha jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kama alivyoshauri Mzee Mwanakijiji pale juu, tumieni BLW, mamlaka hayo mnayo kupitia ile sheria yenu ya kura ya maoni!. Hamna haja ya kuiliza bara lolote, pigine kura ya maoni kuwauliza Wazanzibari kama wanautaka muungano kwa yes or no, watakaojibu no na kama no ndio itashinda, then BLW wanapitisha azimio na taratibu za kuuvunja muungano zinafuatia ikiwemo namna ya kugawana mali!.
Maalim ana bahati sana sasa hivi ni enzi za Dhaifu, ingekuwa ni enzi ya Mwalimu, na ni kweli ameuwasilisha huo huko wa kwanza kushughulikiwa ni Shein, angeulizwa tuu, "jee unataarifa kuhusu waraka huo?, jee ulitoa baraka zako?, kama jibu ni ndiyo, then Shein angetiwa kizuizini (nyumbani) kama Jumbe!, na Maalim angeambiwa ambaki huko huko, na kama hana tujisenti twa Uswiss twa kumsetiri,yule half brother wake Sultani wa Brunei, angaokoa jahazi kumsetiri kama wanavyoifadhili CUF and that would have been the end of the story!.
marekani ana kura ya VETO .. UN.. so ni kama kuwapa taarifa nadhani...
Mkuu Nguruvi3, Zanzibar kuna vituko vya ajabu!, wengi wanadhani ni Maalim ndie autakaye sana urais wa Zanzibar, hawajui kinachotakiwa sio urais, kinachotakiwa ni kisiwa na kinatakiwa na wenyewe!.Pasco, I can't agree with you more!Thanks. Please, allow me to chip in senti sumuni.
Kama ni kweli Maalim atakuwa ameshindwa kuelewa jambo dogo sana. Farouk Karim na Ally Salehe wame-champion Zanzibar kujitoa Chama cha mpira FAT nyakati hizo. Jitihada zao za kujiunga na mashirika ya kimataifa kama FIFA zimegonga mwambwa kwa sababu alizoeleza Pasco hata pale TFF ilipowaunga mkono.
Falconer; Security council ina wanachama wa kudumu 5 (USA,Russia, China, France na UK). Halafu kuna 10 non-permanent members. Wenye kura ya turufu (Veto ni 5) sasa kama unachosema ni kweli Maalimu inabidi awaone wengine 4 maana wanaweza kupinga tu. Hoja yako! mhh
Mwanakijiji: Hakuna ugomvi na Zanzibar kwahiyo maalimu anatakiwa apeleke mswada kwanza BLW kutaka kura ya maoni au kukataa muungano kwa short kati kama ile ya katiba ya Zanzibar, kuondoa mafuta na gesi(Ahmed Rajab) n.k.
Lakini pia alitakiwa awatumie wabunge 50 wanaowakilisha Zanzibar Dodoma.
Zaidi ya hapo wapo wabunge kutoka BLW wanaoingia Dodoma.
Kinachoshangaza ni kuwa unaomba vipi kiti UN kabla hujawa na nchi?
Nadhani Ahmed Rajab anapata majibu ya akina nani wenye ajenda hii (Raia mwema) licha ya kuwatetea.
Baada ya serikali 3(Ahmed Rajab) kukosa majibu na mkataba kuonekana hauna majibu,kwanini wazanzibar wanahangaika sana? Kwanini wasivunje muungano kesho ili keshokutwa Maalim apite kwa Ban Kimoon akiwa na document za maombi.
Huwezi kuwa na kiti UN, ukawa na BLW, Rais, Mahakama halafu ukadai mkataba. Uhusu nini tena!
Seif ni mwanasiasa wa ajabu sana, wakati anachukua mafao treasury Dar es Salaam wakati huo huo anaomba kiti UN.
Maalimu Seif rudi Nyumbani uvunje muungano, acha kujificha nyuma ya serikali 3 au mkataba wewe na washirazi wenzako