Maalim Seif Sharifu Hamadi ni mgonjwa

Status
Not open for further replies.
Kuna taarifa zilioenea chini kwa chini kuwa Makamo wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi ni mgonjwa.
Nashangaa tu habari hii imekuwa kama imefichwa sijaisikia kwenye magazeti wala vyombo vya habari.
Mwenyezi Mungu amjaalie uzima na arudi katika afya yake ya kawaida.

Amyn anaumwa na maradhi gani
 
Najua watu wengi wanamchukia maalim Seif kwa kukubali kuweka kinyumba na Chama Cha Mafisadi. Lakini bado ni binadamu ambaye akiumwa tunapaswa kumuombea uzima sawa na ambavyo tungetaka tuombewe.

Hata kama Seif ni msaliti na mroho aliyeuza chama kwa maslahi binafsi, kumtakia maafa si adhabu stahiki. Usihukumu ukahukumiwa na isitoshe Seif ni mwanasiasa sawa na wale muwapendao.

Tutofautishe siasa na ubinadamu. Hata kama humpendi bado ni binadamu. Hata awekwe kimada na CCM bado maalim ni binadamu kama wewe na ndugu zako.
 
Nakumbuka Miezi kadhaa iliyopita alikuwa ziarani Arabuni ikabidi aongeze muda wa safari yake ili apate Matibabu

Akarudi alipokelewa Airport Zanzibar akawaambia waandishi wa Habari kuwa Afya yake ni Nzuri...

Naona kimemrudia kinachomzuru...
 
Nimeanza kuiamini hii theory isemayo kuwa 'Mwili hufa miaka mitatu baada ya Mawazo kufa.' Mawazo ya huyu madevu yalikufaga siku nyingi. Ugua pole maalim Seif! Sawa sawa!
 
ni kweli kabisa mkuu....hata kama ni mbara kutomtambua mAalim kama ni kiongozi ni sawa na uhaini.......pia ni kuonyesha ukomavu wako dhaifu wa kisiasa. ....ni binadamu mwenzetu....ni kiongozi wetu.......tunakuombea upone upesi uendeleee na ujenzi wa taifa....

Mkuu usiwe na mentality ya kitumwa, ati Zumari likichezwa Zanzibar watwana wanacheza hadi Maziwa Makuu!
That is gone for ever with history.

Kama Seif ni kiongozi basi hata Idi Amin alikuwa kiongozi, na alipotukwaza tulimwita nyoka iliyobidi kuondolewa na kuangamizwa,
Kiongozi huyo!

Suala hapa ni mtu kujijengea heshima ya uongozi wake kwa watu walio pande mbili za Tanzania, na kama tumeanza ubaguzi wa sehemu mtu atokayo katika huu mungano basi lazima tutegemee yule anayeuendeleza ubaguzi huo apate matokeo yake ule upande unaobguliwa.

Siyo siri waTanganika leo wanabaguliwa kwa Utanganyika wao huko Zenj, tofauti kabisa na waZenj wanavyoishi kwa amani huku Tanganyika.

Ukibaguliwa, ukasema hewala bwana, na bado usichukue hatua yoyote, basi una matatizo ya kimsingi.
 
huyu si ndio mfadhiri wa wanauamusho.? Hata hivyo namwombea apone haraka afaidi umakam wa rais wa kuchonga,maana na yeye kwa siasa zake za ngangari na ngunguri ameua watu wengi sana na wengine kupata vilema vya maisha.!
 
Jamani maalim haumwi taabani! Mukumbuke alifanya operesheni ya magoti india! Na analazimika kurejea kipindi hichi! Wewe unayejiita mnyamwezi acha kumuongelea mtu usiyemjua! Maalim si muarabu wala hana asili ya kiarabu! Uliza ujibiwe usiwasilishe chuki zako hapa! Hii unaonesha kiasi gani huna iman ya dini yeyote!
 
Mkuu uwe mkweli katika nafsi yako.
Maalim amehusika kikamilifu katika kila sokomoko la muungao isipokuwa la marehemi Karume.

Kuanguka na kuondolewa urais Jumbe , Maalim alihusika moja kwa moja kwa malengo anayoyaelewa.

Kanzu anayovaa Maalim hakuna asiyeifahamu

"wakati wangu ni mdogo kweli kweli mkuu kusoma/kujibu hoja hapa JF, ila kama utanafasika tafuta cd ya mazungumzo ya Mh Hassan Nassor Moyo na waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu aliyoyafanya siku mbili tatu zilizopita. kama hiyo haitoshi waweza tafuta cd ya semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliyokuwa wakijadili "paper" iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa Znz (hii ilifanyika tarehe 21 july, 2012) .... hapo tutamjua kweli maalim anahusika kwa kila (kama uitavyo) sokomoko la muungano na tutaielewa ile kanzu yake pia"
 
Najua watu wengi wanamchukia maalim Seif kwa kukubali kuweka kinyumba na Chama Cha Mafisadi. Lakini bado ni binadamu ambaye akiumwa tunapaswa kumuombea uzima sawa na ambavyo tungetaka tuombewe.

Hata kama Seif ni msaliti na mroho aliyeuza chama kwa maslahi binafsi, kumtakia maafa si adhabu stahiki. Usihukumu ukahukumiwa na isitoshe Seif ni mwanasiasa sawa na wale muwapendao.

Tutofautishe siasa na ubinadamu. Hata kama humpendi bado ni binadamu. Hata awekwe kimada na CCM bado maalim ni binadamu kama wewe na ndugu zako.

"nina imani ungekuwa mpinzani kweli wa ccm, basi ungefurahia unyumba huu iliyowekwa cuf na ccm. ama kama una ajenda nyengine hiyo ni kivyako. kwa sisi wa Zanzibari unyumba huu umetupa faida kubwa sana!!! laitan kiasi. nafikiri unaona nini kinaendelea sasa Znz?"

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom