Maalim Seif Shariff Hamad Aitikisa SMZ

Sivyo Hivyo ukweli ni kuwa Hapa Zanzibar sewhemu amabayo CUF inaweza kushinda ni Wilaya ya Micheweni, Wilaya ya Wete na Wilaya ya Chake. Wilaya ya Mkoani inagawana majimbo nusu kwa nusu na wapinzani wake. Unguja haiwezi kushinda katika Wilaya yoyote ya huko.
CUF wameshashinda Unguja na Pemba majimbo mengi tu MjiKongwe, Bumbwini (kwa Mamkwe) na majimbo ambayo uhakika wa kushinda bila jasho ni Tumbatu, Bububu, Mlandege, Magogoni, Mpendae n.k CCM haijapata kushinda jimbo kipande Pemba, kwa hiyo chama gani ni cha upande mmoja??? utajaza......!!!
 
Kumbe hata huko nako 'nchi' imegawanyika!!!
 
CUF wameshashinda Unguja na Pemba majimbo mengi tu MjiKongwe, Bumbwini (kwa Mamkwe) na majimbo ambayo uhakika wa kushinda bila jasho ni Tumbatu, Bububu, Mlandege, Magogoni, Mpendae n.k CCM haijapata kushinda jimbo kipande Pemba, kwa hiyo chama gani ni cha upande mmoja??? utajaza......!!!

Unamaanisha CUF?
 
Nafikiri alichosema Hamad ni very sensitive. Tunahitaji uchunguzi na ikithibitika ni kweli basi watu wawajibishwe. Tunajenga utawala bora na rule of law lakini viongozi (wanasiasa) wanatuangusha.

Ebu tujiulize kwanza. Huko Pemba Serikali iko mikononi mwa CUF. Na masheha hao ni wa CUF. Sasa hao Shariff anaolalamikia ni Masheha kutoka Chama gani? Naomba tafakali na fact zaidi.
 
Hakuna ubishi CCM wanatumia tume ya uchaguzi kujihakikishia ushindi hata pale wanaposhindwa.Maalim seif amshindwa mara zote kujifunza tangu mwaka 1995 kwamba kinachomwangusha ni tume ya uchaguzi.Nina amini kabisa Maalim alishinda uchaguzi wa mwaka 1995 lakini tume ikishinikizwa na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa wakaamua kumtangaza Dr Salimin kuwa Rais wa Zanzibar.

Tanzania inahitaji tume huru ya uchaguzi ili kuiepusha nchi yetu na machafuko ya kisiasa kama ilivyotokea kwa jirani zetu Kenya.Mara nyingi nchi zetu za kiafrika hazinafanya mabadiliko ya katiba mpaka madhara yanapotokea.Sijui Tanzania inasubiri madhara kama yalivyotokea Kenya ndiyo walete tume huru !!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Tanzania kukiwa na tume huru ya uchaguzi maisha ya viongozi yapo hatalini wanalijua hilo. Ndo maana hawatathubutu kuruhusu tume huru ya uchaguzi.
 
Hakuna ubishi CCM wanatumia tume ya uchaguzi kujihakikishia ushindi hata pale wanaposhindwa.Maalim seif amshindwa mara zote kujifunza tangu mwaka 1995 kwamba kinachomwangusha ni tume ya uchaguzi.Nina amini kabisa Maalim alishinda uchaguzi wa mwaka 1995 lakini tume ikishinikizwa na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa wakaamua kumtangaza Dr Salimin kuwa Rais wa Zanzibar
Na kwa taarifa tu yule Mw'kiti wa tume ile ya mwanzo 1995(Jaji Zubeir Juma Mzee) iliyomnyan'ganya ushindi Maalim Seif, hivi sasa ni mwendawazimu wa kuokota makopo, Mw'mungu anamlipa kwa dhulma yake. Na wengine wanafuatia kama akina Mkapa, wameuwa, wameiba, waomenyanyasa, wamepiga na sasa Mw'mungu anawalipa hawaishi kwa amani kila siku wamo midomoni mwa watu wakitajwa kwa ubaya, mpaka wafe kwa presha na sukari.
 
Tatizo WaTz mnashindwa kuunga mkono pale ambapo panaonekana pana njia ya kutokea na kuondokana na utawala huu wa CCM uliojaa ukiritimb ,hili ni tatizo na kama kweli tumekusudia kuiondoa CCM madarakani ,basi hakuna budi kuwaunga mkono watu wa Pemba kwa msimamo wao wa kuikataa CCM ,hatuwezi tukawa wenye kutaka jambo la pamoja halafu tukawatenga wale ambao tumo nao katika chombo kimoja ,itakuwa tunaunafiki ambao hauna mfano na hauelezeki na maisha yote tutabakia wenye kutawaliwa kimawazo.

Kama kweli vyama vya upinzani bara vina uelewa wa demokrasia ya kweli basi hawana budi kuitisha maandamano ya nchi nzima kupinga kitendo kinachotokea Pemba kwa sasa ,kwani mbinu zinazotumika huko ikiwa wengine watazifumbia macho basi 100% zitakuja kuathiri kwao vilevile kama tulivyoona katika mageuzi ya matokeo ya kura waliyofanyiwa CHADEMA ,haya yalianza Zanzibar na huku mliona CUF au Seif anapenda madaraka tu ,hakuna hila zozote.

Viongozi wa vyama vya upinzani ni lazima kwa hali yeyote ile wa admitt kuwa harakati za uchaguzi zinakiukwa na hivyo ni kuutaarifu umma wa waTanzania usikubali hali hiyo iendelee ni lazima ikomeshwe kuanzia sasa ,kwa ufupi waipinge na kuipiga vita huko huko ilikoanzia na sio kusema maneno ambayo athari zake zitakuja kuwageukia.

Let us stand together with the people of Pemba kwa kupinga harakazti zozote zile zinazoonekana zinaikandamiza demokrasia hapa Tanzania.
 
namsikitikia sana Hamad, kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa kutimiza ndoto zake za kuwa rais wa Zenj,CCM wanajua wanachokifanya always...
 
namsikitikia sana Hamad, kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa kutimiza ndoto zake za kuwa rais wa Zenj,CCM wanajua wanachokifanya always...
CUF wakijipanga vizuri wanaweza kutoka na ushindi lakini mgombea awe mtu mpya na Maalim Seif ampigie debe.

Kama Seif atag'ang'ania tena kugombea yatakuwa yaleyale ya chaguzi 3 zilizopita.
 
Wadau mi niko Pemba, hayo ya kusema kuna mkakati wa kukibania CUF Pemba yawezekana.

nimeongea na watu wengi sana kijiweni jana, watu huku wanamsimamo sana. wanasema unaenda kujiandikisha unaambiwa uje na ID, form ya kupata ID inapatikana kwa Sheha, ukienda kwa sheha anakuambia form zimeisha. pia waliofikisha umri na hata wazee wanadaiwa vyeti vya kuzaliwa.

wakaniambia nikienda mimi kwa sababu ni mtu wa bara na kiswahili cha kibara naandikishwa mara moja kwa mtizamoa kuwa wabara ni CCM. kuna ishu kweli. wakasema wanachofanya sasa ni kuzuia kuandikisha yeyote yule nami nikawaambia ndio dawa!!
 
CUF wakijipanga vizuri wanaweza kutoka na ushindi lakini mgombea awe mtu mpya na Maalim Seif ampigie debe.

Kama Seif atag'ang'ania tena kugombea yatakuwa yaleyale ya chaguzi 3 zilizopita.

Shida ni nani mwingine. Watu wa Pemba si rahisi kumuunga mkono mtu kama Juma Duni kwa sababu ametoka Unguja!! labda mtu kama Hamad Rashid, wanajiona wanabaguliwa sana hivyo nao wanataka mtu wao sasa.
 
Ebu tujiulize kwanza. Huko Pemba Serikali iko mikononi mwa CUF. Na masheha hao ni wa CUF. Sasa hao Shariff anaolalamikia ni Masheha kutoka Chama gani? Naomba tafakali na fact zaidi.

Masheha ni waajiriwa wa serikali sio CUF. ni kama watendaji wa vijiji bara
 
Wadau mi niko Pemba, hayo ya kusema kuna mkakati wa kukibania CUF Pemba yawezekana.
Bw. Ncha Vipi? hawakukueleza kuwa sheria za ID zinazuia kuandikishwa watu kutoka Bara (Dar na Tanga) ambao hawastahili kupiga kura Pemba, ambao hupelekwa huko na jamaa na mashemegi zao waliohamia Dar na Tanga (ambao aghalabu huwa ni wafuasi wa CUF).Hao kwa udanganyifu walipiga kura chaguzi zilizopita. Be fair- liangalie suala hilo, kwa upeo. usibabaishwe na ya vijiweni tu.
 
Ulimwengu mzima wanajua tatizo la Zanzibar na wanafamu CUF ameshaporwa ushindi katika chaguzi zilizopita ipokuwa tu CCM inatumia mabavu. Hakuna kitu kibaya kama kumnyima mtu haki yake pasi na sababu yoyote ya msingi.

Wanaosema kuwa Hamadi hana jipya lte's wait and see. Ninachoomba uchaguzi wa 2010 uishe salam otherwise i am very scared watu watapoteza maisha!!!
 
Bw. Ncha Vipi? hawakukueleza kuwa sheria za ID zinazuia kuandikishwa watu kutoka Bara (Dar na Tanga) ambao hawastahili kupiga kura Pemba, ambao hupelekwa huko na jamaa na mashemegi zao waliohamia Dar na Tanga (ambao aghalabu huwa ni wafuasi wa CUF).Hao kwa udanganyifu walipiga kura chaguzi zilizopita. Be fair- liangalie suala hilo, kwa upeo. usibabaishwe na ya vijiweni tu.

Hilo lawezekana! sijalifanyia uchunguzi na ukiwauliza wanasema halijatokea, ni ngumu kukubali hata kama ni kweli. wanachosema ni kuwa CCM huwa wana-import wabara na kuwatembeza kwa malori sehemu mbalimbali, bahati mbaya wote nilioongea nao yaonekana ni wafuasi wa CUF.

Yote nayapata vijiweni kwenye kahawa ya jioni!! sina muda wa kwenda maofisini!!
 
Pole sana ndugu yangu, sasa habari hizo zitafakari vizuri na jihadhari usije ukapandishwa jazba na wewe ukaanza kuropokwa yale ya ovyo.
 
Safari hii, Ngoma itakavopigwa ndivo itakavochezwa.. Tusubiri
.

Mimi natabiri yale ya Jan 26 na 27, mwaka 2000 yatatokeo mwaka 2010.

Mola atunusu na hilo . kwani dalili za mvua ni mawingu. Na sasa mawingu ndio hayo.

Poleni sana ndugu zangu Konde na Pujini
 
Pole sana ndugu yangu, sasa habari hizo zitafakari vizuri na jihadhari usije ukapandishwa jazba na wewe ukaanza kuropokwa yale ya ovyo.

Uzuri sina jazba kwenye haya ila hakuna ubishi hapa kuna jambo haliko sawa. kama ni kuandikisha mashemeji toka dar na tanga ni moja ya tatizo. lakini pia kuzuia watu wasiandikishwe wanostahili pia ni tatizo lingine.
 
Maskini kafu mbona mnaonewa sana? sasa nasikia mmeanza kutengeneza mabomu kuaribu miundo mbinu yenu ni kweli? we Junius ni wewe engineer wa kutengeneza kitu hii?
Wakiendelea kuwaletea fujo jitengeni muwe na serikali yenu na unguja yao au siyo?
We Junius nenda kule Bukoba kagombee badala ya Lwaka... utapewa tu maana kafu kule bado ngangali.:D
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom