Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 945
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kisiwani Pemba, imesema inamchunguza Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Seif Shariff Hamad, kama alichochea wafanyabiashara wa Pemba kususia kuuza mazao yao Unguja na kama itaibinika hivyo watamshitaki.
Kadhalika kiongozi huyo atafikishwa mahakamani kama pia itabainika kuwa ameshawishi wafanyabiashara kuwabagua wateja wanaowauzia bidhaa madukani kwa misingi ya itikadi.
Tamko hilo lilitolewa na Wakuu wa Mikoa miwili ya Pemba, Bw. Dadi Faki Dadi na Bw. Juma Kassim Tindwa, wanaowakilisha mamlaka ya utawala katika kisiwa hicho.
``Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, tahadhari mti na macho tutamchukulia hatua yeyote, hatumuogopi mtu? Seif hatumuogopi. Yeyote anayevunja sheria atachukuliwa hatua... Juzi maduka 10 tumeyafungia kama watayafungua tutawapeleka polisi na kuwafungulia mashtaka na wengine wakiendelea tutawafungia,`` alisema Bw.Tindwa.
Walisema wafanyabiashara 10 kisiwani humo wamefungiwa leseni baada ya kubainika kuwa wanafanyabiashara kibaguzi na kuwanyima huduma wateja wenye itikadi tofauti.
Akizungumza kwenye mahafali ya Chuo cha Ualimu cha Benjamin Mkapa Wete kisiwani Pemba, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, aliongeza kuwa vitendo vya kuwashawishi wafanyabiashara kutouza mazao yao Unguja na kubagua wateja kwa misingi ya kiitikadi vinakiuka masharti ya leseni na ya haki za binadamu.
Aliwashangaa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wabunge wa CUF wanaohudhuria vikao na kulipwa posho na SMZ lakini wanathubutu kuwahamasisha raia wasiuze mazao Unguja wakati wakijua kuwa uamuzi huo utaathiri mapato ya wananchi?
``Wananchi wanafanyabiashara ili kupata fedha za kuendesha, maisha kama kususia waanze Wawakilishi na Wabunge ambao wanahudhuria vikao na kulipwa posho, huku Hamad akilipwa mafao na serikali,`` alisema Bw. Tindwa.
Aliwataka wafanyabiashara kujua kuwa iwapo maduka yao yatafungwa wao ndiyo watakaoathirika.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Bw. Dadi, alisema licha ya wafanyabiashara kupinga ushauri huo wapo baadhi ya wanasiasa wanaowashawishi kutoa huduma kwa ubaguzi na itikadi za kisiasa.
Walipinga madai ya viongozi wa CUF kuwa Wapemba wametengwa kimaendeleo ikilinganishwa na Unguja wakisema hayana msingi kwa vile huduma za jamii zinatolewa pote visiwani.
SOURCE: Nipashe