Maalim Seif Kaua CUF? Mrema ataua TLP

Homer

Member
May 26, 2011
99
22
CCM wamefanikiwa kuua upinzani Zanzibar na CUF kwa ujumla. Baada ya uchaguzi 2015 CUF itakuwa historia tu, na Maalim Seif atastaafu kama 1st Vice President kwa heshima zote na marupurupu ya CCM akiwa mzee wa miaka 72!

Tukumbuke kwamba Maalim Seif na wenzake walianzisha CUF 1992 baada ya kutofautiana na serikali/CCM (yeye akiwa waziri kiongozi - No.2). Alifukuzwa serikalini na kwenye CCM, akakosa jukwaa la kisiasa kwani Tanzania ilikuwa nchi ya chama kimoja tu mpaka 1992 tuliporuhusiwa vyama vingi. Kimsingi Maalim Seif, japo amejenga upinzani kwa kiasi kikubwa, nguvu yake kubwa ilitokana na chuki binafsi aliyokuwa nayo dhidi ya waliomyang'anya tonge mdomoni.

Baada ya kuukosa kosa uraisi wa Zanzibar 1995, 2000, 2005, 2010 kwa chini ya asilimia 1 (49.xx% vs. 50.xx%) huku umri ukiwa unakwenda mbio na afya kudorora, akaamua kuwalengesha Wazanzibari kwenye GNU (government of national unity), na kupewa tena cheo cha No.2 (1st Vice President). Huu ulikuwa mkakati wa CCM kumrudisha Maalim kundini kinyemela na kujisafishia wenyewe njia kwenda 2015. Ndio maana kauli zake za hivi karibuni kwamba sera zingine si zake ni utata (au uzee?) mtupu. Huyu sasa anaganga njaa tu na kutumia fedha za walipa kodi kuangalia afya yake. Ameshapata kile alichokipoteza 1988.

Prof Lipumba ana wakati mgumu kuifufua CUF bara kwa sababu hawezi kutofautiana na maamuzi ya serikali na mawaziri wake (collective responsibility). Wenye akili CUF watimkie vyama vingine ili hoja zao zipewe kipa umbele.

Huu ulikuwa wakati mwafaka wa kuimaliza CCM ya Vikongwe wanaotaka kuendesha nchi kijeshi. Wakati CHADEMA wanasambaratisha magamba bara, CUF wangekuwa wanaponda kichwa huko Zanzibar!

TLP na Mrema ni yale yale (NCCR-Marando, then TLP). Mrema anatafuta kiinua mgongo tu sasa hivi.

Anayejua mengine atuletee hapa jamvini na anayebisha leta hoja zako hapa :dance:
 
Ni kawaida ya wanasiasa uchara na wasiopenda kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka, lakini pia ni kawaida ya wanasiasa wanaopenda kuchumia tumbo. Maalim Self azma yake imetimia sasa CUF ni ya nini, Mzee wa Kilalacha yeye yupo bungeni TLP ni ya nini japo amepeita huko.
 
Mkuu sijakuelewa ulivyosema kuwa Mrema ataua TLP, hivi hiki chama kipo hai kisiasa kweli mpaka kiweze kuuliwa?
Nadhani Ubunge wa Mrema hauna uhusiano wowote na Chama chake, bali mapenzi ya wana Vunjo kwa huyu Mzee..
Kwa mantiki hiyo TLP inabebwa na Mrema na wala siyo kinyume chake..

Kuhusu Maalim Seif kuiua CUF itategemea kwa kiasi kikubwa na viongozi wenzake waandamizi..
Kifo cha CUF - Bara kinaharakishwa na ndoa waliyoifunga na CCM (sina kipingamizi kwa upande wa Visiwani)..
Kitendo cha CUF bara kuwa kinyume na madai ya wananchi na kujikuta wanawatetea watawala kinawaweka ktk nafsi mbaya..
Kwa Upande wa Visiwani, sidhani kama itakuwa rahisi sana kwa CUF kufa, (binafsi) naona viongozi wa CUF visiwani wako makini kuliko wawakilishi wake kwa upande wa Bara..
 
Tlp si chama cha siasa ila kampuni binafsi ya Mrema ,cuf nayo ikifuatilia kwa makini tangu uanzishwaji wake ni wa kutilia mashaka.
 
Vyama vingi vitakufa pale vitakapofikia tamati ya uhitaji wake kuwapo, TLP na CUF na Dovutwa wamefikia huku. nahisi watajiunga na CCM hivi karibuni.:mod:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom