Maalim Seif, Hamad Rashid uso kwa uso leo

mimi nasema huyu hamad hatufai...sawasawa?, lengo lake ni kuvuruga chama chetu..sawasawa?, yeye atakuwa mfano kwa watu wenye tabia kama zake..sawasawa?, kama ya maadili aliidharau sasa namwadhibu mimi...sawa? na akitaka aende mahakamani tutamkuta..sawasawa?, na barua tushampa sawasawa?, sawa. Mia
 
Habari za hivi karibuni nilizozipata ni kwamba hiyo kamati ya utendaji imegawanyika vipande viwili. Patamu hapo.

By the way mnafahamu kwamba chini ya katiba ya CUF kamati hiyo inaongozwa na Maalim seif tu, na si mtu mwingine, na kwamba hata Lipumba haingii?
Maskini Mwenyekiti hana chake! Nadhani kabla ya kujadili katiba ya nchi tuangalie pia katiba za vyama vyetu. Tunaweza tukawa tunataka kuweka yaliyomo kwenye katiba za vyama vyetu kwenye katiba ya nchi! Sasa katiba ya namna hii si ni ya kidikteta; mwenye chama anajipa madaraka namna hiyo! Inaonyesha vimelea vya ukiritimba na uimla!
 
mimi nasema huyu hamad hatufai...sawasawa?, lengo lake ni kuvuruga chama chetu..sawasawa?, yeye atakuwa mfano kwa watu wenye tabia kama zake..sawasawa?, kama ya maadili aliidharau sasa namwadhibu mimi...sawa? na akitaka aende mahakamani tutamkuta..sawasawa?, na barua tushampa sawasawa?, sawa. Mia
Mkuu kama Maalim mwenyewe! Sawa sawa?
 
Seif%20hamad(19).jpg

Maalim Seif Sharif Hamad

Matumizi ya kubaki ama kutimuliwa ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mbunge wa Wawi kupitia chama hicho, Hamad Rashid Mohammed, sasa yamebakia kwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye leo ataongoza kikao cha Kamati ya Utendaji kumjadili na wenzake 12.

Kikao hicho ambacho wajumbe wake ni wakurugenzi wote wa idara mbalimbali za chama hicho kitafanyika visiwani Zanzibar kwa siku mbili kabla ya kuamua ama kumtimua uanachama ama kumpa onyo kali kwa barua.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Nidhamu na Maadili ya CUF, Abdul Kambaya, alisema kamati yake ilimhoji Hamad kwa saa 1:30 ambapo alitoa utetezi wake wa jumla zikiwemo nyaraka mbalimbali zinazodaiwa kuandikwa na Maalim Seif pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Hamis Hassan.

Hamad anatuhumiwa kwa makosa 11 ya kuvunja Katiba ya chama hicho ambapo mara kadhaa amekuwa akimtupia lawama Maalim Seif kuwa ameandaa mpango wa kumfukuz katika chama.

Kambaya alisema watuhumiwa 12 walifika mbele ya kamati ya Nidhamu na Maadili na kuhojiwa isipokuwa mtu mmoja, Yasin Mrotwa ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Mkoa wa Mbeya.

Alisema kamati yake imemaliza kazi iliyopewa ya kuwahoji na kuwapa fursa ya kujitetea watu waliokuwa wanatuhumiwa ambapo taarifa zao zitapelekwa kwa Kamati ya Utendaji ili zikajadiliwe na kutolewa maamuzi.

Msuaguano kati ya Hamad na Maalim Seif umefichua siri nzito, baadhi zikihusisha njama za kutaka kufukuzwa kwa mbunge huyo katika chama na nyingine zikimhusisha na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa.

Siri hizo ambazo ziliwekwa hadharani wiki hii na Hamad, baadhi zilifichuliwa kutoka kwenye waraka wa ndani wa CUF na nyingine kutoka kwenye ujumbe wa barua pepe uliotumwa kupitia mtandao wa kompyuta.
Kwa mujibu wa Hamad, njama za kutaka kufukuzwa kwake katika CUF, zilibainika kupitia ujumbe huo wa barua pepe ulioandikwa na

Maalim Seif kwenda kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Desemba 14, mwaka huu.
Sehemu ya barua pepe hiyo inaeleza: “Yeye (Hamad) muono wetu tumfukuze kwenye chama na akiamua kwenda mahakamani na mahakama kutoa maamuzi ya kumpendelea yeye mwache awe mbunge wa mahakama kama walivyokuwa akina Asha Ngede na Naila Majid.

“Wanachama walio wengi wanatudadisi kwanini hatuchukui hatua. Sisi ni kumuachia jamaa yako aendelee kufanya kazi aliyopewa na rafiki yake ya kukivuruga chama, au chama kimvuruge yeye. Ikishajulikana kuwa si mwanachama tena, atakuwa hana mashiko. Muache aende CCM au Chadema akawe mgombea mwenza.”

Hamad alisema pia kuhusishwa kwa harakati zake na Lowassa, kulifanywa kupitia waraka wa ndani ya chama, wenye kichwa cha habari: “Kuchafuka kwa hali ya kisiasa ndani ya chama.”

Alisema waraka wa ndani ya chama uliandikwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF Taifa, Hamis Hassan, kwenda kwa Profesa Lipumba, Desemba 4, mwaka huu.
Alifichua siri hizo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, wiki hii baada ya kuhojiwa na kamati ya Nidhamu na

Maadili ya CUF, katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni.
Alidai hakuhojiwa na kamati hiyo, ingawa kamati jana ilisisitiza kwamba ilimhoji baada ya kumsomea kifungu kinachowapa mamlaka nadani ya Katiba ya chama.

Alisema kwenye kikao na kamati hiyo wiki aliomba apewe tuhuma zake kwa vile barua ya wito aliyoandikiwa inaeleza kuwa aende kujieleza tuhuma za kwenda kinyume cha katiba ya chama, hivyo akataka aelezwe ni vifungu vipi vya katiba alivyokwenda kinyume navyo.

Hamad alisema apewe kumbukumbu za hadidu rejea ya kikao kilichounda kamati hiyo, lakini akaelezwa pia kuwa hilo nalo litapatikana baadaye.
Alisema pia aliomba apewe kanuni zitakazotumika kuendesha shughuli yote ya kujibu tuhuma hizo, lakini nazo pia akaahidiwa kuwa atapewa baadaye.

Alitoa sababu za kutokuwakubali wajumbe hao, akisema kwanza Mwenyekiti wa Kamati, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali, hamtaki kwa sababu alishiriki kikamilifu katika kutengeneza tuhuma dhidi yake na kumtia hatiani katika vikao mbalimbali.

Alisema mjumbe mwingine aliyemkataa ni Hamis Hassan, ambaye ni Katibu wa Kamati, Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CUF Taifa.

Wakati Hamad akisema kamati hiyo si halali na kutokuwa na imani na baadhi ya wajumbe wake, jana Kambaya aliweka wazi kwamba tuhuma hizo si za kweli na kwamba Kifungu namba 63 cha Katiba ya CUF kipengele namba 1 (E) ndicho kilichounda kamati hiyo.
Alisema baada ya Hammad kusomewa kifungu hicho alikubali kwamba kamati hiyo ni halali ingawa alibaki alilalamikia wajumbe wake kuwa hana imani nao.

CHANZO: NIPASHE
 
Mpiganaji hamad rashid baada ya kikao kitakachoongozwa na ndevu atakua mbunge wa jimbo la wawi kwa tiketi ya mahakama!
 
although is too long and since morning is a same story this is copy and paste!
 
Habari za hivi karibuni nilizozipata ni kwamba hiyo kamati ya utendaji imegawanyika vipande viwili. Patamu hapo.

By the way mnafahamu kwamba chini ya katiba ya CUF kamati hiyo inaongozwa na Maalim seif tu, na si mtu mwingine, na kwamba hata Lipumba haingii?

Kama taratibu hatuzijui tu we tunauliza,
Kikatiba CUF ina vikao vinne. 1. Kamati ya ulinzi na usalama 2. Kamati ya utendaji ya taifa 3. Baraza kuu la uongozi la taifa na 4. Mkutano mkuu wa taifa.

Katika vikao hivi vinne vya kikatiba, mwenyekiti taifa anaongoza vikao vitatu, anaongoza kamati ya ulinzi na usalama kama mwenyekiti wa kamati, anaongoza baraza kuu la uongozi taifa kama mwenyekiti wa baraza hilo na anaongoza mkutano mkuu wa taifa kama mwenyekiti wa kikao hicho.

Katibu mkuu wa CUF anaongoza kamati ya utendaji ya taifa tu. Hii ni kwa sababu taasisi nyingi duniani na zinazofanya kazi kwa uwajibikaji na haki siyo rahisi kukuta wenyeviti wanaongoza vikao vya utendaji au wao ni wajumbe wa vikao hivyo na hili liko wazi.

Haiwezekani lipumba awe mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya taifa au awe mjumbe wa kamati hiyo.
Hii ni kwa sababu kwa mamlaka yake kama kiongozi mkuu wa chama hawezi kuwa mtendaji mkuu wa chama.

Advantage tuliyonayo ni kwamba mwenyekiti wetu taifa anabakia akifuatilia masuala yote muhimu ya utendaji na akihoji na kuturudisha kwenye mstari. Na hata tunapokuwa katika vikao vya baraza kuu yeye huongoza wajumbe wa baraza huu kupata ufafanuzi wa mambo muhimu kutoka kwa kamati ya utendaji ya taifa.

Hii ina maana kuwa mwenyekiti wa chama yuko juu ya mambo ya utendaji ya chama, yeye ana-monitor, ana-advise , ana-recheck and re-correct mienendo ya kamati ya utendaji wa taifa.

Hatari ya kuwa na mqenyekiti anayeongoza utendaji katika chama ni kuwa jambo lolote dogo likiharibika, anahusishwa moja kwa moja na hiyo ni hatari kwa taasisi.

Leo pana shutuma kadhaa zimetolewa na baadhi ya viongozi wenzrtu kuwa fedha za chama zimeliwa, au helikopta ilikodiwa kwa bei ya juu n.k.(tuhuma hizi ni za kupikwa tu na hazina uthibitiaho wowote kama nilivyowahi kuthibitisha hapa).

Katika mazingira ya namna hiyo mwenyekiti taifa anapokuwa mtendaji angehusishwa na kila tuhuma ndogo katika chama, jambo amablo siyo sahihi hata kidogo.

Binafsi nadhania utaratibu wetu ni muhimu sana na muhimu ukaendelea.
 
asante sana kwa ufafanuzi mkuu, uwe unapitapita mara kwa mara humu kutolea ufafanuzi wa mambo mengi yanayo husu CUF humu ndani

Ila sasa tunaomba update za kikao hicho
 
Sasa Maalimu Mtatilo si ungetoa na update kidogo tu; naona kamau nataka kuchange muelekeo wa thread hivi
 
Maamuzi ya kubaki ama kutimuliwa ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mbunge wa Wawi kupitia chama hicho, Hamad Rashid Mohammed, sasa yamebakia kwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye leo anaongoza kikao cha Kamati ya Utendaji kumjadili na wenzake 12.

Kikao hicho ambacho wajumbe wake ni wakurugenzi wote wa idara mbalimbali za chama hicho kitafanyika visiwani Zanzibar kwa siku mbili kabla ya kuamua ama kumtimua uanachama ama kumpa onyo kali kwa barua.

Mwenye taarifa zaidi za kikaoni atujuze.

Hili nalo halijakaa kiusahihi,

Maalim seif hana maamuzi juu ya hamad rashid, vikao vya chama ndivyo vina maamuzi juu yake.

Hamad rashid na wenzie walihojiwa na kamati ya nidhamu na maadili(kamati hii ipo kikatiba na inafanya kazi kama kamati ndogo chini ya kamati ya ulinzi na usalama ya chama), baada ya hapo kamati ya ulinzi na usalama italeta taarifa yake katika kamati ya utendaji ya taifa.

Kamati ya utendaji ya taifa itapokea taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama, itaijadili na kuamua juu ya mapendekezo yaliyoletwa.
Baada ya kuamua KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA itawasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha baraza kuu la uongozi la taifa.

Kikatiba, kamati ya utendaji ya taifa haina mamlaka ya kumpa adhabu kiongozi kama mbunge, mjumbe wa baraza n.k. Hii ina maana kuwa sisi wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa hatuna mamlaka ya kutoa adhabu yoyote kwa HR na wenzie.

Baraza kuu litakapoketi ndio litaamua nini cha kufanya. Kwa mujibu wa katiba, baraza kuu linaweza kumpa onyo la maandishi kiongozi, karipio kali la maandishi, kumsimamisha, kumvua uongozi au kumfukuza uanachama(mamlaka haya yapo kamati ya utendaji taifa).

Jana tumemaliza kikao late night na leo tunaendelea siku ya pili na tunatarajia kupokea taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ambayo inaweza kuhusisha pia masuala ya HR.

In general kikao hiki cha kamati ya utendaji ya taifa siyo cha dharura, ni kikao cha kawaida cha kikatiba kinachokaa kila baada ya miezi miwili. Kikao cha mwisho kilifanyika mwezi oktoba mwishoni na kingine desemba mwishoni.

Vikao vya baraza kuu hukaa kila baada ya miezi minne kutathmini mwenendo wa chama na kukielekeza chama namna ya kujiendesha.

Vikao vya mkutano mkuu hukutana mara moja katika kila miaka mitano.

Nawajuza haya ili kupata weledi zaidi wa masuala yetu ya kivikao na ki-katiba.
 
Wamsulubishe tu, ili awe mbunge wa kwanza wa chadema kutoka pemba!
 
Simpendi Rashid, lakini ukisoma maelezo yake, kama atafukuzwa itakuwa kwa utashi wa Seif tu, na si kwa kukiuka katiba ya chama. Huyu bwana anajiamini na anasimamia kile anachokiamini. Siamini kuwa CUF inaweza kumfukuza ikabaki salama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom