Maalim Seif Hamad (Katibu Mkuu - CUF) na Kashfa ya Ufisadi wa 500M za Chama

NCCR, CHADEMA, TLP vyama hivi vipo kibiashara zaidi CUF ni Chama Dume na kinafanya kazi ya kufundisha siasa Tanzania, hemu vuta kumbukumbu 1995 kuna mkoa fulani ulichukuliwa na NCCR wote ila kwa sasa sijui hatma ya mkoa huo ipoje! Hii ndio biashara ya kisiasa inavyofanywa Tanganyika. Kwetu sisi Zanzibar siasa si biashara bali ni UKOMBOZI.
umeongea sana sasa tutakutafutia mji.
 
CCM, wakikorofishana na CUF kukosa nguvu CCM watavunja makubaliano, watarudi kwenye benchi tena!
 
Huyu ndugu yetu aliyeweka thread hii ni muongo kupindukia. Hakukuwa na tusi la namna hiyo kikaoni na wala mie wala jusa hakuna aliyemtukana HR, tumtukane kwa lipi wakati tushasema kamati ya nidhamu na maadili inakuja kufanya kazi yake?

Dhumuni la kikao cha leo lilikuwa ni kuwatoa wasiwasi wanachama ambao baadhi walianza kuamini propaganda za HR kuwa abayosema ni sahihi.
Wanacha,a wameezwa in details tuhuma zote anazotoa juu ya viongozi na chama.

Mie binafsi nimewaonesha wanachama email iliyotoka kwa rafiki wa HR ajulikanaye kama captain silaa. Wakati tunatafuta helikopta igunga niliwasiliana na HR ili kujua kama kuna kampuni cheaper ya kukodi helikopta ndani ya nchi ukiondoa zile ambazo tulizifikia.

Ivoice ya gharama za siku tatu kutumia helikopta kutoka kwa captain silaa zilikuwa ni USD 32,500.

Nimewaeleza wanachama namna gani nilivyosikitishwa na kauli za HR kwenye vyombo vya habari kuwa eti nina chenji ya helikopta na kuwa eti helikopta zinakodiwa kwa shs 20m kwa siku tatu.

Nimewaeleza wanachama namna ambavyo mie nilisaini mikataba ya helikopta iliyokuwa ya bei nafuu kuliko ya dola 32500 aliyotuletea HR tukaikataa.

Nimewaeleza wanachama namna gani nilvyosaini mikataba ya helikopta nikiwa igunga halafu ofisi kuu ndio wakawasiliana na kampuni yenye helikopta na kisha kuilipa kampuni hiyo ya uganda dola 27500.

Mie nikapokea helikopta igunga - sikuelewa hizi tuhuma zake kwangu zisizo na kichwa wala miguu kazitoa wapi.

Jambo lingine nimewaeleza wanachama kwa nini HR asitoe ushahidi kwenye vikao vya chama ili nichukuliwe hatua.

Kwa nini anakimbilia kwenye media na kutoa tuhuma ambazo hazithibitiki?

Kwa ujumla kikao chetu kilikuwa chenye tija kubwa na viongozi walikuwa makini kufuatilia.

Hakukuwa na mtu hata mmoja aliyetoka nje kwa sbb yoyote ile kwa sababu asilimia 99 ya viongozi waliohudhria hawataki chama chao kichezewe.na mtu yeyote.

Kwa hivyo msimamo ambao umetokana na ushauri wa wanachama katika kikao kile ni kuwa kamati ya nidhamu na maadili iendelee na taratibu za kuwahoji na kisha kuchukua hatua.

Hakuna aliyetukanwa, kwa hiyo - aliyeweka thread hii amepotosha ukweli wote.

Pia, waandishi hawakufukuzwa, waliruhusiwa kufanya coverage ya mambo ya utangulizi tu. Kisha waliombwa waondoke ili viongozi wa matawi na kata na wanachama maarufu wabakie na kujadili masuala ya chama.

Kwa ujumla wanachama wana msimamo katika chama na hawataki kiyumbe.

Viongozi wachache wanaomuunga mkono HR katika kukipasua chama pia walihudhuria na hatukutoa nafasi wakejeliwe. Wamekaa kwa uhuru mwanzo mwisho. Hakuna aliyezomewa wala kutukanwa katika kikao.
 
kwani mwanaharamu ni tusi?? si maana yake mtoto wa nje ya ndoa?? mbona watoto wengi walozaliwa nyumba ndogo ni wanahar... u??? labda mwendawazimu kwani hamad rashid navyomfahamu si mwendawazimu

Mkuu inabidi watu wawe wanaangalia kamusi kujua maneno haya. Mwanaharamu/bastard ni mtoto aliyezaliwa na wazazi ambao hawajafunga ndoa. Hata mwendawazini pia si tusi, nadhani ni state of mind au mental problems, na hii inawezekana kuutambuliwa pale mtu anapofanya mambo ambayo ni kinyume na kawaida au na anavyotegemewa. Sasa kama ni tusi tutafute ukweli kuhusu wazazi wa huyo Hamad Rashi kama waliooana au vipi. Na tuwaulize madakatari kama kweli jamaa akili yake ni kawaida hadi asisitahili kuitwa mwendawazimu.
 
Mimi mara nyingi hua nasema, kuna watu hapa hua wanachangia chochote kinachofikishwa hapa bila ya kukifanyia utafiti, hata jana palikuwepo na thread nikaicomment kuhusu hawa wanaoleta mada za uongo lakini kuna baadhi waliniona mimi sifai na kumbe hawajui kama hua wanaishusha hadhi hii forums! Lakini mimi sikupatwa na presha kwani najua haya ndio matatizo ya Watanzania uongo kwao ni jambo la kawaida tu ingawaje unapokuja kudhihirika ukweli wanabaki kuumbuka tu!
 
Pia, waandishi hawakufukuzwa, waliruhusiwa kufanya coverage ya mambo ya utangulizi tu. Kisha waliombwa waondoke ili viongozi wa matawi na kata na wanachama maarufu wabakie na kujadili masuala ya chama.

Kwa ujumla wanachama wana msimamo katika chama na hawataki kiyumbe.

Viongozi wachache wanaomuunga mkono HR katika kukipasua chama pia walihudhuria na hatukutoa nafasi wakejeliwe. Wamekaa kwa uhuru mwanzo mwisho. Hakuna aliyezomewa wala kutukanwa katika kikao.
Sawa Mtatiro tumekuelewa vizuri.Lakini na wewe pia kuwa mwangalifu na matumizi ya media unapokuwa unazungumzia mambo ya ndani ya chama chenu.

Pia jitahidi usionekane kama vile tayari umekwisha pitisha hukumu kabla ya hiyo kamati ya maadili. Vinginevyo tunawatakia mwisho mwema katika hayo mambo yenu.
 
Pengine amenukuliwa vibaya maana sioni kwa vipi Maalim Seif atasema hayo maneno? Kama Hamad Rashid ni mwanaharamu Maalim Seif atakuwa nani?
Nakumbushia kisa cha mtoto wa nje ya ndoa wa Sultan wa mwisho wa Zanzibar, baada ya kutorokea Uingereza, walikuwa wakifadhiliwa na Sultan wa Brunei wenye undungu wa nasaba. Ni Sultan huyo huyo wa Brunei ndie mfadhili mkuu wa CUF kupitia kwa Maalim.

Ikipitishwa sheria ya vetting ya viongozi wetu kufanywa kwa njia ya DNA, mbona hamtaamini macho na masikio yenu!, sio tuu ya Seif, hata tetesi ya Karume, pia niliwahi kuisikia!.
 
mwamakula what d u mean seif hawezi kukemea ushoga kutoka moyoni?.........................................................is he a british by citizenship?
 
Mie binafsi nimewaonesha wanachama email iliyotoka kwa rafiki wa HR ajulikanaye kama captain silaa. Wakati tunatafuta helikopta igunga niliwasiliana na HR ili kujua kama kuna kampuni cheaper ya kukodi helikopta ndani ya nchi ukiondoa zile ambazo tulizifikia.

Ivoice ya gharama za siku tatu kutumia helikopta kutoka kwa captain silaa zilikuwa ni USD 32,500.

Nimewaeleza wanachama namna gani nilivyosikitishwa na kauli za HR kwenye vyombo vya habari kuwa eti nina chenji ya helikopta na kuwa eti helikopta zinakodiwa kwa shs 20m kwa siku tatu.

Nimewaeleza wanachama namna ambavyo mie nilisaini mikataba ya helikopta iliyokuwa ya bei nafuu kuliko ya dola 32500 aliyotuletea HR tukaikataa.

Kamanda, asante sana kwa ufafanuzi wa kina. HR anatakiwa kutumia vikao halali kuzungumzia tofauti zao badala ya kutumia media amzazo kwa kiwango ikubwa hukuza migogoro kwa kutobalance story zao kwa kwa kuwatumikia wanaowalipa fedha. Kwa chama chochote, kiongozi anaposhindwa kuwa na dialogue na viongozi/wanachama wenzie thru vikao halali, huyo si kiongozi bali ni muasi!

Tatizo la HR ni usongo wa madaraka. Alilewa madaraka alipokuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alipokosa cheo hicho akaungana na CCM kupindisha kanuni ili kuunda kambi nyingine ya upinzani ili aiongoze. Kugombea nafasi yoyote ni haki ya kila mtu kwa kadri katiba za vyama vyao zinavyoruhusu, lkn kwanini si muda muafaka ukifika?

Kwanini weakness za vyama vyenu mwaziweka hadharani kwa faida ya nani? HR na Seif ni maswahiba wa muda mrefu, kwa lugha ya kisiasa siku hizi "hawakukutana barbarani" alishindwa nini hata kumkabili na wakaongea wao wawili faragha? Vikao halali vipo kwanini havikutumika? HR pia ana madhaifu yake ktk mgogoro unaofukuta CUF!
 
Adai kumshawishi Lipumba afukuzwe
headline_bullet.jpg
CCM, Chadema, Lowassa wahusishwa
headline_bullet.jpg
Aigomea kamati kumhoji kuhusu tuhuma



Hamad(1).jpg

Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu wito wa kutakiwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama chake. (Picha na Omar Fungo)


Msuguano kati ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, umefichua siri nzito, baadhi zikihusisha njama za kutaka kufukuzwa kwa mbunge huyo katika chama na nyingine kuhusishwa kwa harakati zake za sasa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa.

Siri hizo ambazo ziliwekwa hadharani jana na Hamad, baadhi zilifichuliwa kutoka kwenye waraka wa ndani (internal memo) wa CUF na nyingine kutoka kwenye ujumbe wa barua pepe uliotumwa kupitia mtandao wa kompyuta (internet).

Kwa mujibu wa Hamad, njama za kutaka kufukuzwa kwake katika CUF, zilibainika kupitia ujumbe huo wa barua pepe ulioandikwa na Maalim Seif kwenda kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye yuko nje ya nchi Desemba 14, mwaka huu.

Sehemu ya barua pepe hiyo inaeleza: “Yeye (Hamad) muono wetu tumfukuze kwenye chama na akiamua kwenda mahakamani na mahakama kutoa maamuzi ya kumpendelea yeye mwache awe mbunge wa mahakama kama walivyokuwa akina Asha Ngede na Naila Majid.

“Wanachama walio wengi wanatudadisi kwanini hatuchukui hatua. Sisi ni kumuachia jamaa yako aendelee kufanya kazi aliyopewa na rafiki yake ya kukivuruga chama, au chama kimvuruge yeye. Ikishajulikana kuwa si mwanachama tena, atakuwa hana mashiko. Muache aende CCM au Chadema akawe mgombea mwenza.”

Hamad anasema pia kuhusishwa kwa harakati zake na Lowassa, kulifanywa kupitia waraka wa ndani ya chama, wenye kichwa cha habari: “Kuchafuka kwa hali ya kisiasa ndani ya chama.”

Anasema waraka wa ndani ya chama uliandikwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF Taifa, Hamis Hassan, kwenda kwa Profesa Lipumba, Desemba 4, mwaka huu.

Hamad alifichua siri hizo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya kukutana na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya CUF, katika ofisi za chama hicho.

Katika mkutano huo, Hamad pia aligawa kwa waandishi wa habari nakala zenye ujumbe huo wa barua pepe na zile za waraka huo wa ndani wa CUF.

HAMAD AGOMA KUHOJIWA

Katika kikao na Kamati ya Nidhamu na Maadili jana, Hamad alikataa kuhojiwa na kamati hiyo kwa madai kwamba haiko kikatiba ya chama na pia hana imani na wajumbe wake watano kati ya wanane, akiwamo Mwenyekiti wa kamati kwa vile walikwishamtolea hadharani tuhuma dhidi yake na kumtia hatiani kabla ya kupewa fursa ya kusikilizwa.

Hamad alieleza kuwa, kwenye kikao na kamati hiyo jana, aliomba apewe tuhuma zake kwa vile barua ya wito aliyoandikiwa inaeleza kuwa aende kujieleza tuhuma za kwenda kinyume cha katiba ya chama, hivyo akataka aelezwe ni vifungu vipi vya katiba alivyokwenda kinyume navyo.

Hata hivyo, alisema aliambiwa kuwa jambo hilo atasomewa baadaye.

Alisema pia aliomba apewe kumbukumbu za hadidu rejea ya kikao kilichounda kamati hiyo, lakini akaelezwa pia kuwa hilo nalo litapatikana baadaye.

Hamad alisema, pia aliomba apewe kanuni zitakazotumika kuendesha shughuli yote ya kujibu tuhuma hizo, lakini nazo pia akaahidiwa kuwa atapewa baadaye.

“Lakini mimi nilitanguliza jambo moja la ziada. Nikasema hii kamati mimi siikubali, kwanza haipo kikatiba, lakini pia wajumbe wake siwakubali,” alisema Hamad.

Alitoa sababu za kutokuwakubali wajumbe hao, akisema kwanza Mwenyekiti wa Kamati, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali, hamtaki kwa sababu alishiriki kikamilifu katika kutengeneza tuhuma dhidi yake na kumtia hatiani katika vikao mbalimbali.

Alisema miongoni mwa vikao vilivyotumiwa na Machano kumtuhumu na kumtia hatiani, mbali ya kimojawapo cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa alichotamka kwamba, walimfukuza James Mapalala na wengine na wataendelea kuwafukuza wengine, ni kile kilichofanyika kati ya viongozi na wanachama katika ofisi za CUF Buguruni, hivi karibuni.

Hamad alisema katika kikao hicho cha Buguruni, Machano alitamka:“...Nitawashughulikia (kina Hamad na wenzake).”

“Sasa ukishafika hapo na wewe ndio mwenyekiti tena, kwa kweli sioni kama utafanya haki. Lakini nataka nimshukuru sana, baada ya kulisema hilo aliliona uzito wake. Alisema mimi kama jaji mwadilifu nisingeweza kuendelea na kikao,” alisema Hamad.

Alisema mjumbe mwingine aliyemkataa ni Hamis Hassan, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CUF Taifa. Hamad alisema alimkataa Hamis kwa vile ndiye muandaaji wa tuhuma zote dhidi yake.

Alisema Hamis alimwandikia Profesa Lipumba waraka wa ndani ya chama, Desemba 4, mwaka huu, akielezea juu ya kuchafuka kwa hali ya kisiasa ndani ya nchi na namna baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi walivyokwenda kwenye kikao cha baraza wakiwa na ajenda ya kutaka kumng'oa mwenyekiti, katibu mkuu na makamu mwenyekiti.

Alisema pia Hamis katika waraka huo, ameorodhesha wanachama wengi na kuwashutumu kuwa ni waasi ndani ya chama na kumweleza Profesa Lipumba kuwa wahuni 150 kwenye tawi la Chechnya, Mabibo, kwamba, Hamad aliwalipa fedha ili wawapige Blue Guard bila kushauriana naye (Hamad), huku akijua wazi kuwa hakukuwa na ugomvi wowote tawini hapo.

AHUSISHWA NA LOWASSA

Alisema pia Hamisi anadai katika waraka huo wa ndani ya chama kuwa Hamad anashikiriana na Lowassa kumvuta kasi ili agombea urais kupitia na yeye (Hamad) awe Mgombea Mwenza wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa madai kwamba uwezekano wa Lowassa kupata nafasi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mdogo.

Hata hivyo, Hamad alisema hana ukaribu na Lowassa kulinganisha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kwamba, ukaribu wake na Lowassa ni kuwasalimiana tu.

KAULI YA LOWASSA

NIPASHE iliwasiliana na Lowassa jana na baada ya kuelezwa madai hayo kwa kirefu, alijibu: “Niache kidogo, niko msibani kijijini.”

“Lakini baya zaidi (Hamis) akamwambia mwenyekiti kwamba sisi tuko tayari hata kuua ili tupate nafasi ya uongozi. Hizi ni tuhuma nzito sana,” alisema Hamad.

Alisema alichokifanya kwenye kamati jana, aliusoma waraka huo wa ndani ya chama mbele ya kamati kumkataa Hamis.

Hamad alisema pia aliwakataa wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama waliochaguliwa kuingia ndani ya Kamati ya Nidhamu na Maadili.

Alisema Kamati Tendaji kupitia kwa Mwenyekiti wake, Maalim Seif ndiyo iliyochagua wajumbe wa Kamati ya Nidhamu na Maadili wakati Kamati Tendaji tayari ilikwisha kuwa na maamuzi dhidi yao (kina Hamad).

Hamad alisema ushahidi wa hilo unathibithswa na barua pepe ya Desemba 14, mwaka huu, iliyoandikwa na Maalim Seif kwenda kwa Profesa Lipumba, yenye kichwa cha habari: “Tuwe waangalifu tusiingie kwenye mtego”, ikieleza kwamba alishauriana na Machano na kuona kuna haja ya Hamad na kundi lake kuitwa katika Kamati ya Nidhamu na Maadili kuhojiwa na kufukuzwa kwenye chama.

MAALIM SEIF

Alipoulizwa, Katibu wa Maalim Seif, Mohamed Nuru, alisema bosi wake amesema hafikirii kama ni jambo sahihi kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa vile chama kina vikao.

HAMIS

Kwa upande wake, Hamis, alisema walimuita Hamad na yeye akaitikia wito, hivyo kuzungumza mambo ya kamati kwenye vyombo vya habari ni kumvunjia heshima.




CHANZO: NIPASHE

 
Cuf ngoma inogile,lakini komaa mpiganaji hamad rashid mpaka kieleweke,huyo ndevu amezoea kuwapanda wenzie vichwani....jana nilimuona pahala kapiga picha na mzee mageni mwanzo,nikashangaa ubinadamu huu wa kuwakumbuka wazee wa bara amaeuanza lini??????????
 
Back
Top Bottom