Maalim Seif: CUF imeamshwa Usingizini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
KATIBU wa Chama cha Wananchi (CUF) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad amesema wanachama walioamua kuunda chama kingine baada ya kuvuliwa uanachama ni sawa na kumuamsha mnyama mkubwa aliyekuwa
amesinzia.

Alisema wanachama hao wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid hawana ubavu wa kuleta mpasuko ndani ya CUF kwa kuwa uamuzi wa kukisaliti chama umesababisha kiamke na kuibuka na mikakati
itakayokiletea ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.

Alitoa maelezo hayo wakati akiwahutubia wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Msambweni kupitia CUF, Abdurahman Omari, uliofanyika Msambweni mjini hapa.

“Hawa walioisaliti CUF walichokifanya ni sawa sawa na kuliamsha jitu kubwa mahala ambako lilikuwa limesinzia,”alisema Maalim Seif.

Kuhusu wanaodai kwamba chama hicho ni CCM ‘B’, Katibu huyo Mkuu alisema CUF haijaungana na chama cha mapinduzi na alisisitiza kuwa kamwe hakiwezi kufanya hivyo kwa kuwa malengo yake tangu kuanzishwa kwake ni kuunda dola.

“Kilichofanyika Zanzibar ni kuunda Serikali ya umoja kwa maana ya kufanya kazi za maendeleo ya wananchi kwa pamoja, lakini kila chama kina sera zake na kinaendesha mambo yake bila kuingiliwa,”alisema
Maalim Seif.

Alisema anashangazwa na vyama vya siasa vinavyowahadaa wananchi kwa madai hayo na kubainisha kuwa hata kama chama kingine kingekuwa japo na mwakilishi mmoja angeweza kingeweza kuingia kwenye Serikali ya
umoja, lakini bahati mbaya havikupata ushindi.

Alisema tangu kuundwa kwa Serikali ya umoja, wananchi wa visiwani wanafanya kazi kwa pamoja bila kuwapo na chuki kama zamani na kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa ikiwamo kupanda kwa bei ya mkulima ya karafuu kutoka Sh5,000 hadi Sh15,000 kwa kilo moja.

Mbali ya karafuu,alisema Serikali ya umoja imewezesha kujengwa kwa zahanati, barabara na kuwapo kwa utaratibu wa kutibiwa bure kwa wananchi jambo ambalo awali halikuwapo.

Makamu huyo wa Rais alisema Serikali ya umoja imefanikiwa kupandisha mishahara kwa asilimia 25 kwa watumishi wa kima cha chini pamoja na kuwapandisha vyeo,mambo ambayo hayakufanyika katika Serikali za awali.

Alisema Baraza kuu la chama hicho limepitisha Sera ya raslimali zilizopo kugawa kwa wananchi na kubainisha kuwa umasikini uliopo hivi sasa unawakabiliwa Watanzania unatokana na Serikali ya CCM kushindwa kutumia maliasili kwa maendeleo ya wananchi.

Nafasi ya udiwani katika kata hiyo inazibwa baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Bakari Salehe wa CUF kufariki dunia katika ajali ya pikipiki Septemba mwaka jana.

Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo utakaofanyika Aprili 1, mwaka huu kimemsimamisha Godfrey Mazimu wakati Chadema mgombea wake ni Hamad Kidege.

Maalim Seif: CUF imeamshwausingizini
 
Kuna vyama vinatakiwa visome kupitia cuf.ujasir wa cuf kumchukulia hatua anaevunja taratibu,kanun za chama vyama vingi vimeshindwaa.
Demokrasia bila nidhamu hiyo ni fujo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom