Tuache unafiki, kwenye ukweli tusimamie huo ukweli.
Maalim alipigia kelele posho zake kwa sababu ilikuwa ni haki (MAFAO) yake kisheria as aliwahi kuwa WAZIRI KIONGOZI wa serikali ya Zanzibar. Alikuwa analipwa kama kiongozi wa juu mstaafu. Posho zinazopigiwa kelele na CHADEMA ni posho ambazo unamlipa mbunge wakati hicho unachomlipia ni sehemu ya kazi yake. Mbona polisi, walimu au madaktari hawalipwi wakati wanatekeleza majukumu yao?
Nakuunga mkono. Ukweli ni ukweli. Seif alikuwa waziri kiongozi nako kuna haki zake. Anachosema maalim Seif, ndio ukweli. Kwa nini mbunge alipwe posho kwa kazi anayolipwa mshahara? Chadema wako sahihi na Maalim Seif yuko sahihi. Katika hili tuungane kwani ni njia ya ukombozi kujiepusha na unyonyaji unaofanywa na viongozi wa kisiasa. Waziri Mkuu mstaafu posho yake sawa na 80% ya Waziri Mkuu aliye madarakani. Mbona wastaafu wengine hawapati 80% ya ngazi waliyokuwa nayo. Wanachukua posho na malipo ya kustaafu wanajipendelea. HUO NI WIZI TU.