Maalim Seif awataka wawakilishi UN kuitetea Tanzania

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumamosi, Agosti 25, 2012 06:43 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amesema kazi kubwa inayowakabili wawakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ni kutetea maslahi ya Tanzania katika umoja huo.

Amesema kwamba, Tanzania pamoja na nchi nyingine zinazoendelea, inakabiliwa na changamoto nyingi na njia pekee ya kutatua changamoto hizo ni kushirikiana na kutetea maslahi ya nchi zao na Afrika kwa ujumla.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, alipokutana na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na msaidizi wake, Ramadhan Muombwa Mwinyi walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa hizo.

“Licha ya kwamba mna kazi kubwa ya kufanya kutokana na changamoto nyingi zilizopo, mnaweza kufanikisha majukumu yenu vizuri kama mtashirikiana vema na wawakilishi wengine kutoka nchi zinazoendelea.

“Nchi zinazoendelea ni nyingi mno, nazo zina wawakilishi wao katika Umoja wa Mataifa, iwapo mtashirikiana vema na wenzenu hawa, mtaweza kutatua kero zilizopo kwa urahisi.

“Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na matatizo yanayofanana kwani masuala yanayopaswa kupewa kipaumbele kwa sasa ni pamoja na mapambano dhidi ya janga la UKIMWI pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

“Pamoja na hayo mimi nawatakia kheri na nawaahidi kutoa ushirikiano unaohitajika wakati wowote katika kusogeza mbele maendeleo ya Tanzania kwenye umoja huo.

Kwa upande wake, Balozi Manongi alisema, watatumia uzoefu walionao katika kufanikisha majukumu waliyopewa na kuomba ushirikiano wa karibu kutoka kwa viongozi wa nchi.

Naye Mwinyi, alipongeza kitendo cha kukutana na viongozi mbali mbali wakiwamo Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, kwa kuwa mawazo waliyoyapata kutoka kwao, yatakuwa ni dira ya utekelezaji wa majukumu yao.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, walikutana na Maalim Seif ili kumuaga kabla hawajaondoka kuelekea kituo chao kipya cha kazi Mjini New York, Marekani mwishoni mwa mwezi huu.

Wakati huo huo, Makamu wa Kwanza wa Rais alitoa wito kwa Waislamu nchini, kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuipa nguvu zaidi dini hiyo.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
..nilitegemea Maalim Seif atadai "kiti" cha ZNZ kirejeshwe.

..wa-ZNZ hudanganyana eti Tanganyika haikuwahi kuwa na "kiti" UN.
 
kitendo cha waislamu kugomea sensa ni rais wa tz ndiye wa kulaumiwa sababu sheikh ponda ni muumini mwenzake rais na anashindwa kuwachukulia hatua kama alivyofanya kwa mgomo wa madaktari na walimu huu ni uzembe na udhaifu wa kikkwete kama rais anaweka dini mbele kuliko taifa anaamini katika hilo ushahidi upo mwingi.na kama taifa hili litaingia kwenye vita ya kidini kiongozi atakayebeba mzogo huu ni jakaya kikwete.kama angelikuwa ni mchungaji mtikila kasema wakristo wasusie sensa basi manyang'au wa usalama wa taifa na polisi wangeshamuweka ndani mtikila sasa kikwete acha udini na ongoza taifa kwa misingi ya uongozi na si vinginevyo ubaguzi wa kidini utazikwa nao hata ukienda kaburini maan wewe ndie muanzilishi n​a unaendekeza.
 
kila mtu ana jema lake hapa Maalim si mbaya kupongezwa hongera Seif, lakini najua ukienda pemba utasema kiti cha znz UN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom