Maalim Seif 'aunguruma' Manzese - Dar

MANGI MASTA

Senior Member
Jul 14, 2011
175
56
Katibu mkuu wa Chama cha wananchi CUF na Makamu wa Kwanza wa serikali ya Zanzibar, Mh. Maalim Seif Hamad leo atakuwa akihutubia katika viwanja vya Bakhresa-Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana.

Viongozi wote wa kitaifa wa CUF watakuwepo isipokuwa Prof. Lipumba ambaye yuko Marekani kwa shughuli za uchumi wa kimataifa.

Atazungumzia maamuzi yalichukuliwa na CUF pia kuzungumzia Umaskini unaoikabili nchi.

Source: Mtanzania ya leo
 
Big cuf siku zote askari anapoasi vitani lazima auawe vitani.maalim anabusara sana
 
Katibu mkuu wa Chama cha wananchi CUF na Makamu wa Kwanza wa serikali ya Zanzibar ,Mh.Maalim Seif Hamad leo atakuwa akihutubia katika viwanja vya Bakhresa-Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana.viongozi wote wa kitaifa wa CUF watakuwepo isipokuwa Prof.Lipumba ambaye yuko Marekani kwa shughuli za uchumi wa kimataifa.Atazungumzia maamuzi yalichukuliwa na CUF pia kuzungumzia Umaskini unaikabili nchi Source.Mtanzania ya leo

hawa wapemba wanaitakia nini Tanganyika?
 
Kila la Heri na sarakasi zenu. Hope watu wa matawi ya Chechnia na Kosovo watahudhuria na kurudisha fenicha alizowanunulia HRM. Ila mwambie Maalim Seif asijidanganye na suala la urais wa Tanzania 2015 ataambulia aibu tu. Jussa naye atakuwepo kumuwakilisha RA?
 
seif alifukuzwa ccm na nyerere na yeye anarudia yaleyale. Kumbe nyerere hakufanya makosa kumfukuzwa ccm nilidhani yeye atasahihisha
 
Aungurumapo simba mcheza nani? Seif ni simba asiye na meno wala kucha hata akiunguruma hana mashiko.
 
Kila la Heri na sarakasi zenu. Hope watu wa matawi ya Chechnia na Kosovo watahudhuria na kurudisha fenicha alizowanunulia HRM. Ila mwambie Maalim Seif asijidanganye na suala la urais wa Tanzania 2015 ataambulia aibu tu. Jussa naye atakuwepo kumuwakilisha RA?
Sielewi sura ya Seif itakuwaje atakapoambiwa kiti alichokalia ni baadhi ya fenicha zilizotolewa na HR,

...mh. katibu mkuu karibu sana Manzase huyu HR alitaka kutuvuruga katuhonga fenicha baadhi yake ni hicho kiti ulichokalia na hiyo meza iliyo mbele yako.......hahahaaa Mpemba atakuwa kama mkizi.
 
Tangu Maalim seif atumie nguvu kubwa kumfukuza mwaasisi mwenzake wa CUF Hamad Rashid simuhitaji tena kumsikilza ikiwa ni pamoja na yule Julius Itatiro kibaraka wa Seif na kundi lake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom