Maalim Seif Atembelea Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi Juu ya Katiba

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=3]Maalim Seif Atembelea Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi Juu ya Katiba[/h]


Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad juu ya hatua waliyofikia katika maandalizi ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba, wakati Maalim Seif alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad juu ya hatua waliyofikia katika maandalizi ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba, wakati Maalim Seif alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 11/05/2012. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Mathias Chikawe.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wajumbe wa tume ya marekebisho ya katiba Tanzania wakati alipotembelea ofisi za Tume hiyo jiji Dar Es Salaa tarehe 11/05/2012. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Mathias Chikawe. Wengine kutoka kulia ni katibu wa tume hiyo Assaa Ahmed Rashid na Mwenyekiti jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wajumbe wa tume ya marekebisho ya katiba Tanzania wakati alipotembelea ofisi za Tume hiyo jiji Dar Es Salaam tarehe 11/05/2012. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Mathias Chikawe wakati alipotembelea ofisi za tume ya marekebisho ya katiba tarehe 11/05/2012. Kulia ni Mwenyekiti wa tume hiyo ni Mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba. (Picha, Salmin Said, OMKR).


Imewekwa na MAPARA at 4:56 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
 
Kwanza kuwe na Katiba ya Tanganyika halafu ndio kuwe na katiba ya Muungano, anzi za ububu na upofu zimekwisha muda wake, aliposema Pinda Zanzibar sio nchi ,jee kulikuwa na Faida gani yakuwa na katiba ya Muungano au Muungano wenyewe?

Jee Tanganyika imeungana na mkowa au wilaya?.

Msikile ndugu yetu Mh Sheh Issa Ponda


Bonyeza Vidio

– MuVideo hadhara Lumumba tarehe 26/4/2012 '1' | Mzalendo.net
 
Unafiki wa Seif unaouna hapo.. kafika bara ... sijaona hapo akizungumzia muungano.. akirudi zenji! anaenda kukusanya vikao kupinga muungano!...kuwajaza chuki wa zenji! maalim seif ni ndumila kuwili mchumia tumbo... ! apunguze unafki basi akifika bara kuonana na viongozi wa kitaifa agusie swala muungano kama kweli yupo kwa ajili ya wa znz
 
Kwanza kuwe na Katiba ya Tanganyika halafu ndio kuwe na katiba ya Muungano, anzi za ububu na upofu zimekwisha muda wake, aliposema Pinda Zanzibar sio nchi ,jee kulikuwa na Faida gani yakuwa na katiba ya Muungano au Muungano wenyewe?

Jee Tanganyika imeungana na mkowa au wilaya?.

Msikile ndugu yetu Mh Sheh Issa Ponda


Bonyeza Vidio

– MuVideo hadhara Lumumba tarehe 26/4/2012 '1' | Mzalendo.net

Kakke,

..NOOOOO!!

..muungano wa aina yoyote ile na Zanzibar hauna tija kwetu sisi wa-Tanganyika.

..kwa maoni yangu muungano uvunjwe, na tushirikiane kama mataifa huru na majirani wema kupitia EAC au SADC.

NB:

..nadhani wa-ZNZ wanaanza kuingia woga.

..baadhi yao wameanza kuomba serikali 3, au mkataba kama wa EU.
 
Back
Top Bottom