Maalim Seif Amfariji Bi-kidude

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2]Saturday, August 18, 2012[/h][h=3]Maalim Seif aendelea na ziara zake kuwatembelea wazee na wagonjwa[/h]

Bi Fatma bint Baraka maarufu Bi Kidude akisisitiza kwamba yeye ni mzima hasa kwa wale waliojaribu kumzushia kwamba amefariki ila miguu ndiyo inamsumbua kwa sasa.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Bi. Fatma Baraka Khamis maarufu Bi. Kidude wakati alipomtembelea nyumbani kwa mwanae anakojiuguza maradhi ya miguu, huko Kihinani, Wilaya ya Magharibi Unguja.

Makamu wea Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiomba dua pamoja na msaniii mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Bi Fatma bint Baraka alipomtembelea. (Picha na Salmin Said OMKR

Khamis Haji, OMKR


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa na wazee kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.


Miongoni mwa wagonjwa waliotembelea na Maalim Seif ni msanii maarufu hapa Zanzibar, Bi. Fatma binti Baraka maarufu Bi. Kidude ambaye anasumbuliwa na maradhi ya miguu kwa wiki kadhaa sasa.

Bi. Kidude akizungumza na Maalim Seif huko nyumbani kwa mwanawe Kihinani, Wilaya ya Magharibi Unguja, alimueleza kuwa anasumbuliwa na maradhi ya miguu, lakini amekuwa akifanya shughuli zake nyingi za kawaida.


Hata hivyo, Bi. Kidude alisema amesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya watu kueneza uvumi kwamba amefariki wakati bado ni mzima na anafanya shughuli zake kama kawaida.


Alimueleza Maalim Seif kuwa kitendo cha watu hao licha ya kumsikitisha yeye binafsi, pia kimesababisha usumbufu na hofu kubwa miongoni mwa jamii na baadhi ya watu ambao walilazimika kufunga safari kuja Zanzibar kutoka nchi mbali mbali. “Kuna watu wameeneza taarifa za uongo kwamba nimekufa, wapo watu waliofunga safari kutoka nchi tafauti kuja Zanzibar, lakini walipofika walishangaa kuniona nipo hai”, alisema Msanii huyo maarufu wa muziki wa taarab hapa Zanzibar na Afrika Mashariki.


Katika ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuwatembelea wagonjwa na watu wazima iliyoanza juzi, pia aliwafariji, Mzee Khamis Makungu wa kijiji cha Ndijani, Mzee Abdulrazak Mukri wa Mkunazini, Mzee Ali Haji Pandu wa Mpendae na Sheikh Habib Ali Kombo wa Kiembesamaki.



Imewekwa na MAPARA at 4:46 PM
 
Mungu awajaalie wagonjwa wote, popote walipo, waliotembelewa na wasotembelewa, maarufu na wasiokuwa maarufu, wapone haraka.
 
Mbona maalim amekanyaga mkeka wa bi Kidude na viatu ilihali Bi. Kidude mwenyewe hana viatu?
 
Siku hizi siamini kama kweli Seif huwa anamaanisha anachosema au kufanya; kila mara zinahitajika jitihada za ziada kutambua kuwa ana maana gani kihalisia.
 
Hivi ikiwa kwa huku Bara,waziri Mkuu kuzungukia wazee si itamchukua miaka 3 na hatawamaliza,Zbar wazee wako wachache hivyo au wazee wachaguliwa wale maarufu?kazi kweli kweli...viongozi wamejaazana hawana kazi za kufanya.....aje bara ahimize maendeleo vijijini azunguke mikoani kusaidia kuhimiza kilimo na kupata kero za wananchi na kuwasaidia wakienda Uarabuni kuhemea wajue wanahemea nini!sio suti
 
Hii nchi kweli tunahitaji nguvu ya ziada kujihakikishia maisha bora. Nimesikitika Hali ya hiyo nyumba na mazingira yake kwa jumla. Msanii wa kiwango chake kuishia hapo ni jambo linalohitaji tafakari."..napenda pasi kifani..."wimbo wake huu unanigusa ndani sana kwe moyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom