Maalim aliponda Bunge la Muungano

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Minael Msuya na Elizabeth Edward
MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano hivi sasa linapoteza sifa kwa wananchi wake.​

Maalim Seif amekuwa ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kulinyoshea kidole Bunge la Jamhuri kutokana na hali ya malumbano na vurugu vinavyoendelea kutokea. Kauli hiyo ya Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), inakuja siku chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa Bunge limepoteza mwelekeo. Kauli hiyo za Jaji Warioba na Maalim Seif zinatokana na vitendo vya bunge la kumi kutawaliwa na vurugu na malumbano katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Akizungumza katika mahojiano na Televisheni ya TBC1 hivi karibuni, Jaji Warioba alisema Bunge limekosa nidhamu na kwamba, linahitaji kuchukua uamuzi mgumu kurejesha hadhi yake.

Jana Maalim Seif alisema Bunge la sasa linasikitisha kutokana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ambavyo alisema havina maslahi kwa wananchi. Aliongeza kuwa wakati nchi inakabiliwa na matatizo mbalimbali, wabunge wakionyeshana ubabe na kutukanana ndani ya Bunge badala ya kujadili masuala nyeti yanayolikabili taifa hivi sasa. Mwanasheria Mkuu Pia akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alitoa somo kwa wabunge kuhusu mvutano unaoendelea bungeni: "Peaneni nafasi kwa kila mtu na mwenzake na muwe na ushirikiano kama ambavyo mkono wa kushoto na kulia inavyoshirikiana mzuri."

Jaji Werema aliwaambia wabunge kuwa kazi ya kuwakilisha wananchi inahitaji uvumilivu kuliko kazi nyingine na akawataka wabunge wa pande zote kutumia lugha za kistaarabu wanapo kuwa ndani ya ukumbi wa bunge. Mtafaruku bungeni Jumatano ya wiki hii, Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, alitolewa bungeni na askari wa Bunge, baada ya Mwenyekiti wa Kikao, Sylivester Mabumba, aliyeongoza kikao siku hiyo kumtaka atoke nje kwa kukataa akae chini alipokuwa akiomba mwongozo.

Siku moja baada ya tukio hilo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliwatimua kikaoni wabunge watatu wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Tundu Lissu (Singida Mashariki). Wabunge hao walifukuzwa kutokana na kile Naibu Spika Ndugai alichoeleza kuwa ni kukiuka Kanuni za Bunge zinazowataka kutozungumza chochote ndani ya bunge bila idhini ya kiti cha spika. Wakati Maalim Seif akiponda mwenendo wa bunge la Jamuhuri kwa hivi sasa, alilisifia Baraza la Wawakilishi na kusema kuwa wanaendelea kujenga Zanzibar mpya kwa hoja zenye kuleta manufaa kwa wananchi wa Visiwa hivyo.

"Mijadala ya Zanzibar ni mizito, Baraza la Wawakilishi linaibana CCM vibaya, tofauti na Bunge la Jamhuri, kule (Baraza la Wawakilishi) hakuna kejeli wala matusi," alisema Maalimu Seif alipokuwa akizindua kisima cha maji katika Mtaa wa Buguruni Malapa, jijini Dar es Salaam. Aliongeza kuwa maridhiano ya Zanzibar yameleta utulivu na unawafanya wawekezaji wanaotaka kuwekeza kuondoa hofu na kwamba, hakuna mvutano kwa sababu wanafanyakazi kwa pamoja.

"Sisi tunaijenga Zanzibar, ninyi endeleeni kuvutana na miaka mitatu ijayo mtaona Zanzibar mpya kwa sababu tunashirikiana kwa mambo yenye maslahi ya wananchi kwani tunatambua kuwa ushirikianao ni jambo la msingi," alisema. Alisema wabunge wanapaswa kuacha malumbano kwakuwa mtindo huo unatoa mwanya kwa Serikali kukwepa mambo muhimu. "Wabunge ibaneni Serikali kwa hoja za msingi sio kwa malumbano, mfumo wa malumbano unaipa nafasi Serikali kukwepa kujibu mambo ya msingi yanayoihusu na yenye manufaa kwa taifa," aliongeza Maalim Seif. Pia aliwashukia watu wanaobeza maridhiano ya Serikali ya Mapinduzi kwa madai kuwa CUF sio cha upinzani tena.

"Wapo watu wanaobeza maridhiano ya Serikali ya Mapinduzi na kusema eti CUF sio chama cha upinzani, maneno gani hayo? Eti sababu wanashirikiana na CCM! Sijui watu hawa wamejifunza wapi siasa, kwani nchi mbalimbali duniani katika ngazi za uongozi vyama vinashirikiana," alisema Maalim Seif na kuongeza: "Uingereza ni mfano mzuri, ina vyama viwili tu; ‘Conservative' na ‘Labour', vyama vyote hivyo vinafanya kazi kwa pamoja na kushirikiana kikamilifu," alisema. Aliongeza kuwa CUF bado ni chama cha upinzani Zanzibar na mijadala inayofanywa visiwani humo ni mizito na ina lengo la kuijenga Serikali hiyo. Pia Maalim Seif aliwashukia viongozi wa CCM wanaobeza uongozi wake na kusema kuwa, Zanzibar iko kwenye siasa nadhifu.

Source Mwanachi Gazeti
 
Minael Msuya na Elizabeth Edward
MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano hivi sasa linapoteza sifa kwa wananchi wake.​

Maalim Seif amekuwa ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kulinyoshea kidole Bunge la Jamhuri kutokana na hali ya malumbano na vurugu vinavyoendelea kutokea. Kauli hiyo ya Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), inakuja siku chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa Bunge limepoteza mwelekeo. Kauli hiyo za Jaji Warioba na Maalim Seif zinatokana na vitendo vya bunge la kumi kutawaliwa na vurugu na malumbano katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Akizungumza katika mahojiano na Televisheni ya TBC1 hivi karibuni, Jaji Warioba alisema Bunge limekosa nidhamu na kwamba, linahitaji kuchukua uamuzi mgumu kurejesha hadhi yake.

Jana Maalim Seif alisema Bunge la sasa linasikitisha kutokana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ambavyo alisema havina maslahi kwa wananchi. Aliongeza kuwa wakati nchi inakabiliwa na matatizo mbalimbali, wabunge wakionyeshana ubabe na kutukanana ndani ya Bunge badala ya kujadili masuala nyeti yanayolikabili taifa hivi sasa. Mwanasheria Mkuu Pia akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alitoa somo kwa wabunge kuhusu mvutano unaoendelea bungeni: “Peaneni nafasi kwa kila mtu na mwenzake na muwe na ushirikiano kama ambavyo mkono wa kushoto na kulia inavyoshirikiana mzuri.”

Jaji Werema aliwaambia wabunge kuwa kazi ya kuwakilisha wananchi inahitaji uvumilivu kuliko kazi nyingine na akawataka wabunge wa pande zote kutumia lugha za kistaarabu wanapo kuwa ndani ya ukumbi wa bunge. Mtafaruku bungeni Jumatano ya wiki hii, Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, alitolewa bungeni na askari wa Bunge, baada ya Mwenyekiti wa Kikao, Sylivester Mabumba, aliyeongoza kikao siku hiyo kumtaka atoke nje kwa kukataa akae chini alipokuwa akiomba mwongozo.

Siku moja baada ya tukio hilo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliwatimua kikaoni wabunge watatu wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Tundu Lissu (Singida Mashariki). Wabunge hao walifukuzwa kutokana na kile Naibu Spika Ndugai alichoeleza kuwa ni kukiuka Kanuni za Bunge zinazowataka kutozungumza chochote ndani ya bunge bila idhini ya kiti cha spika. Wakati Maalim Seif akiponda mwenendo wa bunge la Jamuhuri kwa hivi sasa, alilisifia Baraza la Wawakilishi na kusema kuwa wanaendelea kujenga Zanzibar mpya kwa hoja zenye kuleta manufaa kwa wananchi wa Visiwa hivyo.

“Mijadala ya Zanzibar ni mizito, Baraza la Wawakilishi linaibana CCM vibaya, tofauti na Bunge la Jamhuri, kule (Baraza la Wawakilishi) hakuna kejeli wala matusi,” alisema Maalimu Seif alipokuwa akizindua kisima cha maji katika Mtaa wa Buguruni Malapa, jijini Dar es Salaam. Aliongeza kuwa maridhiano ya Zanzibar yameleta utulivu na unawafanya wawekezaji wanaotaka kuwekeza kuondoa hofu na kwamba, hakuna mvutano kwa sababu wanafanyakazi kwa pamoja.

“Sisi tunaijenga Zanzibar, ninyi endeleeni kuvutana na miaka mitatu ijayo mtaona Zanzibar mpya kwa sababu tunashirikiana kwa mambo yenye maslahi ya wananchi kwani tunatambua kuwa ushirikianao ni jambo la msingi,” alisema. Alisema wabunge wanapaswa kuacha malumbano kwakuwa mtindo huo unatoa mwanya kwa Serikali kukwepa mambo muhimu. “Wabunge ibaneni Serikali kwa hoja za msingi sio kwa malumbano, mfumo wa malumbano unaipa nafasi Serikali kukwepa kujibu mambo ya msingi yanayoihusu na yenye manufaa kwa taifa,” aliongeza Maalim Seif. Pia aliwashukia watu wanaobeza maridhiano ya Serikali ya Mapinduzi kwa madai kuwa CUF sio cha upinzani tena.

“Wapo watu wanaobeza maridhiano ya Serikali ya Mapinduzi na kusema eti CUF sio chama cha upinzani, maneno gani hayo? Eti sababu wanashirikiana na CCM! Sijui watu hawa wamejifunza wapi siasa, kwani nchi mbalimbali duniani katika ngazi za uongozi vyama vinashirikiana,” alisema Maalim Seif na kuongeza: “Uingereza ni mfano mzuri, ina vyama viwili tu; ‘Conservative’ na ‘Labour’, vyama vyote hivyo vinafanya kazi kwa pamoja na kushirikiana kikamilifu,” alisema. Aliongeza kuwa CUF bado ni chama cha upinzani Zanzibar na mijadala inayofanywa visiwani humo ni mizito na ina lengo la kuijenga Serikali hiyo. Pia Maalim Seif aliwashukia viongozi wa CCM wanaobeza uongozi wake na kusema kuwa, Zanzibar iko kwenye siasa nadhifu.

Source Mwanachi Gazeti

Walikuwa wapi kusema kuwa serikali imekosa nidhamu? Au kuokosa nidhamu kunakotakiwa kukemewa ni kwa wabunge tu na sio kwa serikali? Ina maana wazee hawa wanaona wabunge ndio hawana nidhamu, lakini hawaoni "kukosa nidhamu" kwa bunge kunatokana na nini? Kuna wakati wazee wetu hawa tunaowaheshimu ni vema wakilinda heshima yao kuliko kuiporomoa kwa kuwashutumu wabunge bila kujali matatizo yanatoka wapi.

Ni heri mapambano yanedelee bungeni kulinko yakiingia mitaani. Yanayotokea bungeni ni reflection ya feelings za wanamajimbo kuhusu hali inavyoendelea hapa nchini.

Siwezi kusema bunge la zamani lilikuwa na heshima wakati kazi yake kubwa ilikuwa ni rubber stamping. Nidhamu iliyokuwepo ilikuwa ni kukaa kimya hata kama kuna uozo mkubwa upo, hata kama wananchi hawatendewi haki. Na kulinda heshima ya chama tawala at the expense of maslahi ya taifa. Utaratibu wa namna hiyo inaonekana kuwa haufai kwa kuwa umetifikisha pabaya.

Inabidi maalimu Seif aambiwe ukweli kuwa Unigereza si nchi ya vyama viwili, na kuna vyama zaifi ya viwili. Sasa hivi inayotawala ni coalition of losers i.e Libe dems and conservatives, na opposition kuna Labour party. Hiyo tu inaonesha kuwa kuna vyama zaidi ya viwili.
 
Back
Top Bottom