Maajabu ya ndoto

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
438
65
Nakumbuka enzi za ujana wangu niliwahi kusikia kuwa, ukiota ndoto halafu unapoamka tu, igeuze shuka uliyojifunika yaani kule kichwani kuwe miguuni na miguuni kuwe kichwani, mara moja na yule uliyemuota ataanza kuiota ndoto hiyo hiyo! mimi sikuwahi kuthibitisha ukweli huu lakini kuna mtu aliwahi. Yeye aliota anafanya mapenzi na msichana fulani na alipomgeuzia inasemekana naye akaiota. Asubuhi wakawa wanaangaliana kiaibu hadi jamaa alipotoboa siri na kumwambia na mshichana alithibitisha.

Naomba atakayeweza ajaribu ili tupate ukweli wa jambo hili!
 
Huoni kesi zitakuwa nyingi? ndoto ni ndoto tu je ukiota jamaa yako wa karibu ( dada, shemegi n.k.) ugeuze shuka? Hakuna kitu kama hicho!!!
 
M'bongo upo hapo? Sharo hiphop kajibu sawa. Yaani unavyoiota ndoto ukigeuza shuka na yule uliyemuota ataiota, hata kama ni dada au kaka yako. Lakini nimewaomba wana JF tufanye majaribio, hata mimi bado sijajaribu. Si tujaribu tu? Mimi nitajaribu na nikifanikiwa nitawakumbusha.
 
Mh! kuna ndoto nyingine nitatamani kutupa shuka kabisa...sijui inakuaje hapo!??
 
Kumbuka kama hujajifunika shuka, geuka wewe ulale upande tofauti. Kichwanikuwe miguuni!!
 
M'bongo upo hapo? Sharo hiphop kajibu sawa. Yaani unavyoiota ndoto ukigeuza shuka na yule uliyemuota ataiota, hata kama ni dada au kaka yako. Lakini nimewaomba wana JF tufanye majaribio, hata mimi bado sijajaribu. Si tujaribu tu? Mimi nitajaribu na nikifanikiwa nitawakumbusha.


Mmh! Wa Nyumbani naomba ufanye experiment kisha utatueleza maana mmm... nakosa cha kusema
 
siwezi amin sana,naona ni imani tu za jamii fulani,huyo aliyekwambia alithibitisha?
 
Wajameni, kugeuza shuka si lazima. Kama unaona ndoto imekudhalilisha kwa nini ugeuze shuka? lakini kama unapenda huyo aliyekudhalilisha naye ashuhudie alivyokudhalilisha, basi geuza shuka. Raha ni kama ndoto hiyo ina faida na wewe na unataka na huyo uliyemuota naye aiote ndiyo unageuza shuka. Kama unaona ni tatizo bora uache usigeuze shuka!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom