Maajabu ya mchepuko wangu

Usithubutu mkuu hapa mwenzio naishi kwa mashaka.
Kuna mwanamke nilikuwa naye zamani kabla sijaoa ila tukapoteana for a certain time yeye alienda Zanzibar kutafuta maisha mimi nikabaki hapa hapa naendelea kustruggle . Milima haikutani ila binadamu tunakutana mwaka jana mwezi wa pili tulikutana so tukakumbushia mchezo ila akatoa ombi kama hilo akasema tayari nina kazi yangu so nahitaji mtoto na wewe ndio nilikuwa nategemea unipatie huyo mtoto.Nikamwambia tayari nina ndoa sitoweza kuwahudumia familia mbili though uwezo huo ninao akadai yeye anachohitaji ni mimba tu ila mtoto na yeye mwenyewe watajilea coz hana shida ya pesa.Nikaingia mkenge kama Nyumbu nikamkubalia sasa hivi bado hajajifungua ila mimba ina miezi 7 napata tabu sana mara anataka niende nikalale kwake ananiomba niweke zamu kama vile nimeoa wake wawili. So mpaka niogopa kuhusu mke wangu akijua hili nitaweka wapi sura yangu.
Nakuomba mkuu usikubali kufanya huo uamuzi utaishi katika wakati mgumu sana.

TUSAIDIE JAPO PICHA MKUU.
 
hatari sana wandugu. Dada zetu (Single) wamejipanga kutuharibia ndoa zetu asee
hivi kila mtu akimng'ang'ania wife wake,wale ma dada single watakuwa na nani?si unajua kuwa tz wanaume ni wachache kuliko wanawake?mwache afanye yake,:p:p:p
 
Unasema ni kero halafu unasema unashindwa kuelewa. Unafikiri mchepuko ni sifa? Utakuja kuacha wanao yatima kwa tamaa zisizoza maana. Bora ubebe bunduki ukaibe tujue umefia vitani kuliko kufa chupini.
 
Usithubutu mkuu hapa mwenzio naishi kwa mashaka.
Kuna mwanamke nilikuwa naye zamani kabla sijaoa ila tukapoteana for a certain time yeye alienda Zanzibar kutafuta maisha mimi nikabaki hapa hapa naendelea kustruggle . Milima haikutani ila binadamu tunakutana mwaka jana mwezi wa pili tulikutana so tukakumbushia mchezo ila akatoa ombi kama hilo akasema tayari nina kazi yangu so nahitaji mtoto na wewe ndio nilikuwa nategemea unipatie huyo mtoto.Nikamwambia tayari nina ndoa sitoweza kuwahudumia familia mbili though uwezo huo ninao akadai yeye anachohitaji ni mimba tu ila mtoto na yeye mwenyewe watajilea coz hana shida ya pesa.Nikaingia mkenge kama Nyumbu nikamkubalia sasa hivi bado hajajifungua ila mimba ina miezi 7 napata tabu sana mara anataka niende nikalale kwake ananiomba niweke zamu kama vile nimeoa wake wawili. So mpaka niogopa kuhusu mke wangu akijua hili nitaweka wapi sura yangu.
Nakuomba mkuu usikubali kufanya huo uamuzi utaishi katika wakati mgumu sana.
Pole sana, umekiri kuwa wewe ni nyumbu and you deserve to be one.

⊙ Kwani ukitulia na mke wako unakosa nini, au mnaona ufahari kulala ovyo ovyo?

⊙ Na umri wako huo(naamini wewe u mtu mzima), huwezi kujiongeza ukiambiwa "nataka unipe mimba lakini nitalea mwenyewe"? Kiumbe gani wa kike anafurahia kulea mimba na mtoto bila uwepo wa mwanaume?

Kweli wewe ni nyumbu.
 
Hii tabia inashamiri sana, mnatuzalia watoto wasio na wazazi wa kuwalea kwenye maadili (familia). Kidogo kidogo tunakuwa kama mataifa mengi ya kimagharibi, watoto wanalelewa na mzazi mmoja.
 
Hivi siku hizi michepuko imehalalishwa? Yaani mchepuko sio tatizo, kinachokusumbua wewe ni hilo ombi LA ujauzito tu? Hiki kizazi chetu kinachangamoto sana.
ndo wanaume zetu hawa inabidi tu tupite tukajipooze na ndovu.
 
Usithubutu kumpa mimba huyo mchepuko

Fikiria kiumbe mtakacholeta duniani hakitapata upendo na malezi ya wazazi wote wawili

Pia linda ndoa yako, mheshimu mkeo
 
hivi kila mtu akimng'ang'ania wife wake,wale ma dada single watakuwa na nani?si unajua kuwa tz wanaume ni wachache kuliko wanawake?mwache afanye yake,:p:p:p
ni wachache kwa tofauti gani na wanawake? na umri upi ulio chini zaidi na upi ulio juu? acheni kuhalalisha ufirauni.
 
Dunia ishaisha jamani, yaani watu wanashauri jamaa kwa umakini mno juu ya kuu-hendo mchepuko vizuri. So michepuko ni halali now?
 
Back
Top Bottom