Maajabu ya mapacha walioungana

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MUNGU ni wa ajabu. Ni wa ajabu kwa sababu maajabu yake ni makubwa. Ajabu hii inadhihirika katika muujiza wa watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana. Mapacha wengi wanaoungana hudumu kwa kipindi kifupi na wengine hupoteza maisha wakati madaktari wakijaribu kutumia ustadi wao wote kuwatenganisha, lakini wapo ambao Mungu huwaruhusu kuendelea na maisha na kuwapa mafanikio makubwa.

Miongoni mwa mapacha walioungana na ambao hadi sasa wanaishi vizuri ni Consolata na Maria ambao ni watoto kwenye familia ya Mwakikuti. Mungu, si tu, amewaruhusu kuendelea kuishi, bali pia ameanza kuonyesha maajabu yake kwa kuwapa mafanikio; wamefaulu mtihani wao wa darasa la saba ijapokuwa hadi sasa haifahamiki ni wapi watakaposoma masomo yao ya sekondari.

Hawa ni watoto kutoka Ikonda wilayani Makete mkoani Iringa. “Siku tuliposikia kwamba tumefaulu hatukulala kwa furaha, tuliruka na kumshukuru Mungu kwani hatukuamini kama tungeweza kufaulu kutokana na kusomea katika mazingira magumu sana,” anasema Consolata. “Hatukua na kiti cha kukalia darasani, siku zote tulikalia kibaiskeli ambacho hakitutoshi na kadri siku zilivyokuwa zikisogea ndivyo kilivyokuwa kikituumiza kwa kuwa ni kidogo,”

Kwa mujibu wa mabinti hawa, kila asubuhi rafiki zao waliwapitia ili kuwapa msaada wa kusukuma baiskeli yao hadi shuleni. Muda wa mapumziko waliwarejesha nyumbani kwao kwa ajili ya kujisaidia. Mapacha hao walipata alama zinazolingana kwenye mtihani wao wao mwisho, kila mmoja akipata alama 151, lakini kinachothibitisha kuwa hawakutazamiana wala kusaidiana kwenye mtihani ni kutofautiana kwao kwa alama kwenye baadhi ya masomo.

Katika somo la maarifa ya jamii, Consolata alipata alama 29 na Maria kupata alama 25, wakati kwenye somo la sayansi Maria amemzidi Consolata kwa kupata alama 31 dhidi ya 29 na hali ni kama hiyo kwenye somo la Kiingereza ambalo Maria amepata alama 36 na kumzidi Consolata aliyepata alama 34. Afisa elimu wa mkoa wa Iringa, Salum Maduhu anasema kutokana na kiwango chao cha kufaulu, ofisi hiyo imepeleka majina yao katika ngazi ya kitaifa ili watafutiwe shule maalum ili waweze kuendelea vizuri na masomo yao.

Walimu wasema wana heshima na wanajituma Pamoja na hali yao, Consolata na Maria ni wanafunzi wenye heshima, adabu, upendo na ambao wanajituma katika masomo, kitu ambacho walimu wanasema kiliwafanya wapate marafiki wengi, na pengine hiyo ndiyo sababu kubwa ya kufaulu kwao.

“Sijawahi kuwakuta wakiwa wamenuna... kila wakati wanacheka ndio maana wanafunzi wenzao waliwapenda sana. Walijituma kusoma na tangu darasa la kwanza walikuwa wakifanya mitihani yao vizuri,” anasema mwalimu wao wa hisabati, Kanisius Gawasike. Mwalimu mwingine, Amanyile Fungo anasema hata kabla matokeo ya darasa la saba kutangazwa, alifahamu vyema kwamba Maria na Consolata wangekuwa miongoni mwa wanafunzi ambao wangefanya vizuri katika mitihani yao.

“Hawajawahi kufeli somo langu... ingawa walikuwa wakiandika kwa shida, siku zote walikuwa kati ya nafasi ya kwanza hadi kumi. Sifa yao kubwa ni kuongozana katika masomo. Maria akiwa wa kwanza, basi Conso wa pili, na Conso akiwa wa sita basi Maria anamfuata,” anasema.

Wameungana, lakini kila mmoja nahisia zake Juhudi zao zinazolingana katika masomo na tabia zao haziwafanyi wawe watu wa aina moja licha ya kuungana tumbo. Kila mmoja ana hisia zake na ana vitu anavyopendelea. Maria ni mcheshi zaidi ya Consolata; wawachagui chakula lakini Maria akila samaki anasumbuliwa na tumbo.
Lakini kama mmoja akijisikia kwenda kulala, basi mwenzake pia atalazimika kulala kwa kuwa wameungana tumboni. Maumbile yao yanawalazimu watoto hawa wapendane na kusaidia.

“Maria akiumwa, inanibidi niwe mpole, nitulie kwa sababu nikimfanyia fujo nitamuumiza. Akitaka kulala tunaenda wote na kama litamuuma tumbo la kuharisha basi tutaenda wote uani, hatujawahi kugombana, tunapendana sana,” anasema Konsolata.
Maria anasema maisha yao ya shule yalikuwa mazuri kutokana na ukweli kwamba, watu wengi waliwapenda hivyo hawakuiona tofauti.

Habari za kuzaliwa kwao zilifichwa
Ingetegemewa kwamba katika dunia yao la utandawazi na uwingi wa vyombo vya habari, taarifa za kuzaliwa kwao zingepamba magazeti mengi, redio na televisheni. Lakini haikuwa hivyo kwa Maria na Consolata ambao walizaliwa Hospitali ya Misheni ya Ikonda mwaka 1996. Ulemavu wao ulisababisha wafichwe na kwa wakati huo habari za kuzaliwa kwao hazikuenea sana.

Walianza kujulikana wakati walipojiunga na elimu ya msingi wakati wamisheni walipolazimika kuwahamishia watoto hao kwa mama mlezi wao na kwa wakati huo, walitafutwa walezi wawili.

“Tulikuwa na akina mama walezi wawili, lakini sisi tunampenda huyu kwa sababu anaishi na sisi kama watoto wake aliowazaa. Tunaomba popote tunapoenda huyu awe mama yetu,” anasema Consolata.

Wakiwa na miaka mitatu, baba yao Alfred Mwakikuti alifariki dunia na walipofikia darasa la pili mwaka 2002, mama yao pia alifariki dunia hivyo kuwaacha wakiwa yatima. Mama yao mlezi anasema licha ya kuwa analipwa kiasi kidogo cha mshahara kutoka misheni kwa ajili ya kuwalea, bado maisha yao ni magumu sana na analazimika kulima ili aweze kukidhi mahitaji yao.

“Mzigo mzito sana, mazingira ya hapa nyumbani magumu na hayana miundo mbinu ya kuwawezesha kuishi vizuri. Wanateseka sana lakini nalazimika kulala nao chumbani kwangu ili kuhakikisha usalama wao,” anasema mlezi huyo.

Baiskeli yao imeharibika miezi sita sasa Matembezi yao yote, yakiwemo ya kwenda shuleni yanategemea sana baiskeli yao, lakini kwa miezi sita sasa chombo hicho cha usafiri kimeharibika na hawana mbinu nyingine ya kuwawezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Sasa wanaomba kutengenezewa baiskeli yao ambayo italingana na mahitaji yao ya sasa baada ya baiskeli yao ya zamani kuharibika takriban miezi sita iliyopita. Lakini maombi yao hayaishii hapo. "Tunaomba tupelekwe kwenye shule ambayo ina mambo ambayo yatakidhi mahitaji yetu... yenye miundombinu ya kutuwezesha kumudu maisha," anasema Maria.

“Tunahitaji shule ambayo itaweza kutusaidia, kama kuna uwezekano wa kupewa nyumba tutashukuru kwani hali yetu ilivyo ni tofauti na wenzetu.” Walimu wao wanashauri, ikiwa Serikali itaamua kuwasomesha, basi ihakikishe kuwa mama yao mlezi anakuwa nao karibu baada ya kuwawezesha kufikia hapo walipo sasa. “Hatufichi; bila huyu mama hawa watoto wasingefika hapa walipo. Anawajua; anajua mahitaji yao na amewazoea sana kwa kuwa anaishi nao kama wanaye. Alikuwa msaada mkubwa wakati wakiwa shule. Wakimuacha mama huyo na kuwapeleka mbali, watoto hawa wanaweza kuugua na wasifanye vyema shuleni,” anasema Kanisius Gawasike, mwalimu wa Shule ya Msingi Ikonda. Itaendelea Jumamosi ijayo
 
kweli Mungu ana miujiza yake.....nimejaribu kufikiria kwa harakaharaka jinsi watoto wa kike walivyo na mambo mengi halafu hawa ndio wameungana....kweli nitazidi kumshukuru Mungu kila dakika ya pumzi yangu
 
kweli Mungu ana miujiza yake.....nimejaribu kufikiria kwa harakaharaka jinsi watoto wa kike walivyo na mambo mengi halafu hawa ndio wameungana....kweli nitazidi kumshukuru Mungu kila dakika ya pumzi yangu
ni kweli hata kifamilia tu fikiria wangekua wa kwako ungefanyeje mie naona makampuni yajitolee hata kuwapa pikipiki na baiskeli kwaajili ya kuendea shule nampongeza sana mama mlezi kwa kujituma
 
ni kweli hata kifamilia tu fikiria wangekua wa kwako ungefanyeje mie naona makampuni yajitolee hata kuwapa pikipiki na baiskeli kwaajili ya kuendea shule nampongeza sana mama mlezi kwa kujituma

huyo mama anahitaji pongezi....hawa watoto niliwahi kuwaona kwenye TV siku moja.....niliumia sana lakini Mungu anajua sababu ya kuwafanya hivyo.....mimi ningeshauri habari yao iwekwe wazi kwenye vyombo vya habari.....huwezi jua nani na nani watajitolea......au kama utaweza mkuu kutupa maelezo yao yaliyojitosheleza....nadhani hapa hapa JF tunaweza kuwa mfano
 
huyo mama anahitaji pongezi....hawa watoto niliwahi kuwaona kwenye TV siku moja.....niliumia sana lakini Mungu anajua sababu ya kuwafanya hivyo.....mimi ningeshauri habari yao iwekwe wazi kwenye vyombo vya habari.....huwezi jua nani na nani watajitolea......au kama utaweza mkuu kutupa maelezo yao yaliyojitosheleza....nadhani hapa hapa JF tunaweza kuwa mfano
Ni kweli kabisa
 
Daah nilikuwa natafuta chaneli ya mpira nkakosea nmeangukia tbccm nikakuta habari ya hawa mapacha kumbe wamemaliza form4 mwaka, Mungu awalinde!
 
Yaani nimewaona moyo ukaguswa. ..
Maria na Consolata wana furaha na wana matumaini ya kusoma zaidi ya hicho kidato cha nne. ...
wamesema wanaomba uchaguzi wa viongozi utakaofanyika October uwe wa amani. ..Pia wameomba tuchaguwe viongozi wenye sifa zinazofaa na watakaoweza kutuletea maendeleo. .
 
Nimewaona kwenye TBC Tv ni mabinti wenye upendo na watu na nchi yao pia, kweli wanahitaji kusaidiwa kutoka kwa sisi wote watanzania. Mungu aendelee kuwapa afya tele.
 
Mungu ni wa ajabu sana, atabaki kuwa Mungu tu. Conso na maria wamekuwa mabinti sasa
 
Niliwahi kuwasikia masista wakiwaongelea redio Maria shirika la hao masista ndio wanawasomesha nakatamani sana kuwaona kumbe wamewaonyesha kwenye tv Mungu aendele kuwalinda
 
Consolata na maria mungu awabariki sana,ninawaombea kila lenye heri katika ndoto zenu za kuendelea na masoma yenu ,AMEEEENI,
 
Kwani hawa mapacha hawajawahi kupga picha na muheshimiwa Jk?? Maana angewakumbuka Leo thawabu take inazid
 
Back
Top Bottom