Maajabu ya kaskazini

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
Atakayepinga hili akapimwe akili.
Fuatilieni tangu kuumbwa kwa ulimwengu kaskazini ndiyo iliyoinuliwa.wakati ibrahim akiachana na ndugu yake alimwambia achague kaskazini au kusini angalia ibrahim alielekea wapi?
Nitatoa mifano ya kaskazini menginemtatafuta wenyewe.
1.duniani maendeleo yalianzia kaskazini.
2.afrika maendeleo yalianzia kaskazini.
3.tanzania maendeleo yalianzia kaskazini.
4.mkoa wangu maendeleo yalianzia kaskazini
5.wilaya yangu maendeleo ya lianzia kaslkazini.
6.kijiji changu maendeleo yalianzia kaskazini.
7.ofisi ya bosi wangu ipo kaskazini.
8.nyumbani kwangu chumba changu kipo kaskazini.

naomba hapo ulipo fuatilia wewe upo wapi?na maendeleo yako yanatokea wapi?
 
Weledi, Ung'amuzi, Ukombozi. Maendeleo vyote hivi huanzia kaskazini anayebisha hajafanya utafiti
 
Ni sawa lakini pia kuna upande wa pili............

Ushoga umeanzia kaskazini......Wizi umeanzia kaskazini...........Watumwa walipelekwa kaskazini........Ubaguzi ulifanywa/unafanywa na watu wa kaskazini................Biashara ya ngono imeanzia kaskazini.............Vita ya dunia imeanzia kaskazini...............N.K
 
Ringo umechemsha. Ukila na kipofu usimshike mkono ili kipofu afe njaa.

Mods tafadhali tupa hii kwenye trash as haina viwango na vigezo kujadiliwa na great thinkers.

Ringo think big!
 
Ukisema Kaskazini lazima umalizie ni kaskazini ya wapi. Maana hata Pwani ni Kaskazini ya Lindi, Morogoro ni kaskazini ya Iringa nk. Mie zamani nilidhani Kaskazini ni juu nikawa nashangaa mto Nile unaelekea kaskazini badala ya kusini kumbe kila upande kuna juu na chini. Vivyo hivyo kila mahali kuna kaskazini, Mashariki,Magaharibi na Kusini yake. Tafadhali usiseme tu unatoka Kaskazini je ni kaskazini ya wapi? Maana pale unapopaita kaskazini ni kusini mwa eneo lingine na ni mahariki mwa eneo lingine nk.
 
Nchi hii inaongozwa na watu wa kaskazini,kikwete ni kijiko tuu wanaoongoza nchi ni chadema kila wanachoamua kinakua,chek sasa raisi amekubali kushtakiwa,kweli kaskazini ni soo
 
Ringo umechemsha. Ukila na kipofu usimshike mkono ili kipofu afe njaa.

Mods tafadhali tupa hii kwenye trash as haina viwango na vigezo kujadiliwa na great thinkers.

Ringo think big!

Duh! Mkuu Maskini Jeuri,
Busara zako ndizo zitakazowaamsha wengi....bila shaka unachotaka kutuambia ni kwamba, Ringo asimwage mchele penye kuku wengi....akifanya hivyo, hata wale Wamakonde wa Tandahimba wanaoisubiria CHADEMA kwa hamu nao watagundua kwamba CHADEMA ni ya kaskazini...!!!! hawa, hawapaswi kushikwa mkono, kwamba waingie tu kichwa kichwa na hadi watakapokuja kushituka TOO LATE!!
 
Mimi ni mtu wa Pwani....nitakuwa mjinga kuona ufahari kwavile tu mimi natoka pwani wakati sijalipa japo punje ya mchanga ili niwe mwenye asili ya pwani...yaani imetokea tu, by chance nikawa mtu wa pwani!!! Mungu angetaka, angenifanya niwe mtu wa Rukwa, K'njaro au kokote kule!! ya nini basi kukionea fahari kitu ambacho sikutumia nguvu yoyote kukipata!? Hii ni sawa na mwanaume anayejiona bora kwavile tu yeye ni mwanaume wakati nae hakutumia japo a tiny particle ya chochote kile ili awe mwanaume!!!

Ama kweli, JF Is The Home Of Greatest Thinkers!!!
 
Atakayepinga hili akapimwe akili.
Fuatilieni tangu kuumbwa kwa ulimwengu kaskazini ndiyo iliyoinuliwa.wakati ibrahim akiachana na ndugu yake alimwambia achague kaskazini au kusini angalia ibrahim alielekea wapi?
Nitatoa mifano ya kaskazini menginemtatafuta wenyewe.
1.duniani maendeleo yalianzia kaskazini.
2.afrika maendeleo yalianzia kaskazini.
3.tanzania maendeleo yalianzia kaskazini.
4.mkoa wangu maendeleo yalianzia kaskazini
5.wilaya yangu maendeleo ya lianzia kaslkazini.
6.kijiji changu maendeleo yalianzia kaskazini.
7.ofisi ya bosi wangu ipo kaskazini.
8.nyumbani kwangu chumba changu kipo kaskazini.

naomba hapo ulipo fuatilia wewe upo wapi?na maendeleo yako yanatokea wapi?
hata kwa dar temeke iko kusini na kinindoni kaskazini
 
Back
Top Bottom