Maajabu ya Bunge letu; Spika sasa hataki Mwongozo wala Taarifa!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Jana jioni, nilipata bahati ya kushuhudia Bunge kabla TANESCO hawajanihujumu kwa kunikatia umeme.

Kwa bahati nilimkuta Mh Halima Mdee akichangia hoja ya Wizara ya Miundo Mbinu, kwa kweli alikuwa anapiga virungu vya hatari. Baadaye akafuata Mh Deo Filikunjombe, naya akaja na kauli ya kutaka Waziri anyongwe!

Wakati Mh Mdee anachangia hoja na kushusha virungu, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Mwakyembe aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Kikao; aliwasha kipaza sauti na kusimama kuomba mowngozo, Mwenyekiti alikataa akisema atashhughuilikia habari za Mwongozo baadaya!

Mh Filikunjkombe naye alipoanza kuchangia akaja na lugha ngumu ngumu na kutaka Waziri anyongwe, wakati huo Mbunge mwingine (sikumbuki nani) akawasha kipaza sauti akiomba kutoa Taarifa, Mwenyekiti wa Kikao agaoma!

Linalonishangaza na kunichosha ni jinsi sasa Spika na Wenyeviti wamekuja na syle mpya za kukataa miongozo na taarifa! Huu ni woga au ukandamizaji? Maana ni haki Wabunge kuomba mwongozo wa Spika au kutoa taarifa!

Sasa Spika na Wenyevitai wanapozuia, wanakuwa wanaamnisha nini? Ni kushindwa, ubabe au ni kitu gani?

Kwa hili nadhani sasa viongozi wa Bunge wame-prove failure, na wanafanya ukandamizaji na kukiuka kanuni zinazowapa Wabunge haki ya kuomba mwongozo wa Spika na kutoa taarifa wakati mchangiaji anapoendelea na hoja.
 
Back
Top Bottom