Maajabu: Trafiki afa kwa kuomba rushwa kisha kuikataa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Hiki ni kisa cha kweli!!
Askari barabarani alimaarufu kama trafiki wa kituo cha kange tanga,amekufa ktk mazingira ya kutatanisha baada ya kuomba rushwa na alipoletewa alikataa!

Kisa kilianza hivi,Trafiki huyo alikuwa sehemu yake ya kazi maeneo ya Kange, na kuna mzee mmoja pale Kange anafahamika sana kwa jina la mzee Shemahonge ana gari inayofanya kazi ya kubeba mkaa vijijini na kuuleta Kange. Yule trafiki akaikamata ile gari na kuomba laki moja ndipo aiachie yule mzee akamwambia kuwa ana 20,000 tu. Mabishano yalipozidi trafiki aliamua kuipeleka kituoni, cha ajabu mkuu wa kituo alistuka sana kuiona ile gari na akamuonya yule trafiki kuwa kwanini ameileta pale ile gari kwa kuwa yule mzee ni hatari sana!

Mzee Shemahonge aliamua kwenda kutafuta ile laki moja aliyoombwa na baada ya kuipata akampelekea yule trafiki. Mkuu wa kituo na yule trafiki walimuomba sana yule mzee asitoe ile na aichukue tu gari yake lakini yule mzee akapinga vikali kwamba hachukui gari bila wao kuchukua pesa yake, mwisho polisi wakatumia nguvu kumuamru achukue gari, kweli mzee wa watu akachukua gari na laki yake akarudi nayo.

Kesho yake vimbwanga vikaanza yule trafiki akiona gari tu analia sana, mara akasema anaona mapaka, mara milio ya shilingi tumboni, yani balaa tu!

Mkuu wa kituo akamfata yule mzee na kumuomba radhi lakini yule mzee akasema gari yake tangu anunue haijawahi kukanyaga polisi sasa yule trafiki alimdharau na kumpuuza sana hivi hilo ni fundisho kwa askari wote na ni lazima afe!

Kweli baada ya wiki mbili za mateso jana yule trafiki amefariki rasmi!
 
Duh!!! hiyo imetulia kama ni kweli. Kwanini huyo mzee tusimtumie kwa hawa FFU. wakati wanapiga mabomu wawe wanatoka vinyesi!!!.
 
Mzee yule ni kiboko ya wote!! Duh, ndo ujue watanzania hatujaamua kuzitumia hizi technolojia za asili kusaidia nchi yetu kuendelea.
 
Rushwa imemtokea puani. Adhabu aliyoitoa ni kubwa sana. Bora hata angemuotesha busha kilo tano kuliko kumuu.
 
Kuna haja ya kumuajiri huyu Mzee serikalini ili awakomeshe mafisadi wote. Hakuna haja ya kusumbuana kupelekana mahakamani.
 
Hivi huyo ni wewe au kuna mtu amehack akaunt yako manake always unaongeaga uharo!
 
ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni
ukisikia mwisho ndo sasa umefika mtu wala haoni aibu wala huruuma kutoa roho ya mwenzie
 
Hiki ni kisa cha kweli!!
Askari barabarani alimaarufu kama trafiki wa kituo cha kange tanga,amekufa ktk mazingira ya kutatanisha baada ya kuomba rushwa na alipoletewa alikataa!

Kisa kilianza hivi,Trafiki huyo alikuwa sehemu yake ya kazi maeneo ya Kange, na kuna mzee mmoja pale Kange anafahamika sana kwa jina la mzee Shemahonge ana gari inayofanya kazi ya kubeba mkaa vijijini na kuuleta Kange. Yule trafiki akaikamata ile gari na kuomba laki moja ndipo aiachie yule mzee akamwambia kuwa ana 20,000 tu. Mabishano yalipozidi trafiki aliamua kuipeleka kituoni, cha ajabu mkuu wa kituo alistuka sana kuiona ile gari na akamuonya yule trafiki kuwa kwanini ameileta pale ile gari kwa kuwa yule mzee ni hatari sana!

Mzee Shemahonge aliamua kwenda kutafuta ile laki moja aliyoombwa na baada ya kuipata akampelekea yule trafiki. Mkuu wa kituo na yule trafiki walimuomba sana yule mzee asitoe ile na aichukue tu gari yake lakini yule mzee akapinga vikali kwamba hachukui gari bila wao kuchukua pesa yake, mwisho polisi wakatumia nguvu kumuamru achukue gari, kweli mzee wa watu akachukua gari na laki yake akarudi nayo.

Kesho yake vimbwanga vikaanza yule trafiki akiona gari tu analia sana, mara akasema anaona mapaka, mara milio ya shilingi tumboni, yani balaa tu!

Mkuu wa kituo akamfata yule mzee na kumuomba radhi lakini yule mzee akasema gari yake tangu anunue haijawahi kukanyaga polisi sasa yule trafiki alimdharau na kumpuuza sana hivi hilo ni fundisho kwa askari wote na ni lazima afe!

Kweli baada ya wiki mbili za mateso jana yule trafiki amefariki rasmi!
Potelea mbali na hadithi zako za enzi za mawe hapa. Dunia ya leo kama wako wanaoamini visa vya kijinga namna hii basi ni hamnazo
 
tanga kwetu. hayo mambo yanapungua kasi siku hizi, kumebaki usinga tu, mjihadhali nyie mnaopenda wake za watu.
 
Back
Top Bottom