Maajabu Nape na Mkama wasababisha foleni kuelekea ITV

MVUA GAMBA

Senior Member
Apr 13, 2011
102
63
Wana jf leo nimeshangaa sana hawa jamaa wa magamba wanakuja kutembelea hapa ofisini kwetu guardian cha ajabu kuanzia mwenge trafiki wametanda hapa kwetu pia hapa katika kona ya kuingia itv kuna ma[polisi na gari defenda ya polisi ulinzi uliopo maeneo haya utadhani anakuja hapa raisi wa nchi.

Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma trafiki tokea mwenge mpaka hapa wapo 9 polisi katika kona wapo watano kwenye geti letu askari waliovaa kiraia wapo wawili hiki chama tabu kabisa naomba tujadili uhalali wa hili jambo.
 
Siku zao zinahesabika wameshajua hawana ridhaa ya wananchi wanalindwa kwa vikosi maalumu vya Polisi,iwapi ile raha walikuwa nayo wakiimba nyimbo za kuwachanachana wapinzani na kuwatupa ha ha ha ha ,Nitaipenda Nchi yangu kwa nafsi yangu yote mpaka siku ya kufa kwangu
 
Hivi mkubwa wako hapo gurddian anajua unatumia rasilimali za ofisi kwa matumizi yasiokusudiwa? kama unafanya kazi hapo kwa nini usitumie magazeti yenu kuhoji hili swala huo ni woga na unafiki.
 
Hivi mkubwa wako hapo gurddian anajua unatumia rasilimali za ofisi kwa matumizi yasiokusudiwa? kama unafanya kazi hapo kwa nini usitumie magazeti yenu kuhoji hili swala huo ni woga na unafiki.

What an advise! And still yourself is is under an alias here
 
Tanzania ni taifa la kipolisi,ndiyo maana polisi wanaua raia kwa risasi kama wanaua simba mla watu bila kuchuliwa hatua.
 
kwanini mengi amewaruhusu waje kuleta siasa ofisini kwake?..mwambie mengi reginald tunapoteza imani naye..au wamemuahidi nafsi katika tenda zao za kifisadi?... na huyo nape na tabia yake ya kubembeleza magazeti yawaandike vizuri toka wajivue vigamba vyao...itamgharimu sana. mzee mukama hana nyimbo mufillisi wa kila kitu sera na mawazo mgando na hafai mara 100 ya makwamba ... poleni sana wana magamba

mdau kuhusu ushauri wa nn kifanyike ni kwamba"waache wachezee resources zetu muda wao ndio huuuu unamalizikia"
 
Siku zao zinahesabika wameshajua hawana ridhaa ya wananchi wanalindwa kwa vikosi maalumu vya Polisi,iwapi ile raha walikuwa nayo wakiimba nyimbo za kuwachanachana wapinzani na kuwatupa ha ha ha ha ,Nitaipenda Nchi yangu kwa nafsi yangu yote mpaka siku ya kufa kwangu

Yes their days are numbered. Freedom is comming tommorow.
 
What an advise! And still yourself is is under an alias here

Ni ushauri tu mkuu kwani ukizingatia magazeti ya IPP Medea yanafika kila kona ya Tanzania itakuwa vizuri akatumia vyombo vya IPP kuhoji hilo swala hapo nadhani tutaona uwajibikaji wao vilivyo. Ila kama nimekosea kumpa ushauri jf mnisamehe ni wazo tu na maoni yangu hayafungamani na mtu yoyote.
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza, Magamba wanatafuta huruma za watu wenye influence ndani ya taifa. Utakumbuka kabla na baada ya uchaguzi viongozi wa dini ndio waliwaita ama kuwafuata viongozi wa upinzani kuteta nao jambo, hasa kuhusu mustakabali wa amani ya nchi yetu.

Baada ya magamba kuona hawakupata fursa hiyo, wanajipeleka wenyewe kujipendekeza kwa viongozi wa dini. Mukama anapuyanga kiatu mara leo kwa Pengo, mara kesho kwa Mufti.

Tutasikia mengi kwa hawa viongozi wa kimabavu, tumaini lao limebaki kwenye bunduki ya polisi. Kuna siku nao polisi watawageuka kwani na wao ni watu wanaotembelewa na ugumu wa maisha uliolikumba taifa.
.
 
poleni sana kwa sababu ndiyo kawaida yao hao wana magamba sasa wanatembelea hapo kwa misingi gani au wao ni akina nani kwenye taifa hili paka wapewe heshima kubwa kiasi hicho wakati watu wanateseka na mafoleni wana magamba wanajitanua ni upuuzi mtu jamani na haya mambo waende zao hawana dili
 
Wana jf leo nimeshangaa sana hawa jamaa wa magamba wanakuja kutembelea hapa ofisini kwetu guardian cha ajabu kuanzia mwenge trafiki wametanda hapa kwetu pia hapa katika kona ya kuingia itv kuna ma[polisi na gari defenda ya polisi ulinzi uliopo maeneo haya utadhani anakuja hapa raisi wa nchi.

Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma trafiki tokea mwenge mpaka hapa wapo 9 polisi katika kona wapo watano kwenye geti letu askari waliovaa kiraia wapo wawili hiki chama tabu kabisa naomba tujadili uhalali wa hili jambo.

Kwani Mukama na Nape si ni viongozi wa siasa na sio wa Serikali?
Japo Chama chao ndio kinatawala lakini wanabaki kuwa viongozi wa Chama na sio Serikali hivyo hawana hadhi ya kuzuia njia au hata kupewa ulinzi maalum wa Polisi au doula.

Bila shaka Polisi hao wametenda kosa na wanaendeshwa kisiasa na sio kisheria. Inawapasa warudi tena shule kusoma Police General order (PGO) especially kifungu muhimu cha msafara.
 
Wana jf leo nimeshangaa sana hawa jamaa wa magamba wanakuja kutembelea hapa ofisini kwetu guardian cha ajabu kuanzia mwenge trafiki wametanda hapa kwetu pia hapa katika kona ya kuingia itv kuna ma[polisi na gari defenda ya polisi ulinzi uliopo maeneo haya utadhani anakuja hapa raisi wa nchi.Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma trafiki tokea mwenge mpaka hapa wapo 9 polisi katika kona wapo watano kwenye geti letu askari waliovaa kiraia wapo wawili hiki chama tabu kabisa naomba tujadili uhalali wa hili jambo.
hakuna uhalali wowote kwa chama chochote kutumia mapato na rasilimali nyingi za raia wenye itikadi tofauti kwa manufaa ya chama, la sivyo tupewe mchanganuo wa jinsi nchi inanufaika na maziara yao.
 
Back
Top Bottom