MAAJABU: hii ndiyo Tanzania toka 1961 hadi sasa.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Tanzani mpaka sasa, Katika miaka
hii ya nyuma hatukuwa tunajenga
Ujamaa.
Nchi yetu, uchumi wetu, na tamaa
kubwa za watu wetu, ni tofauti
sana na jinsi zilivyokuwa kabla ya
ukoloni. Kwa jumla tumekubali
mawazo na maisha ya mabwana
zetu wakoloni. Ni kweli tuliweza
kuondoa serikali ya Kikoloni; lakini
hatujaondoa akilini mwetu
mawazo ya ubinafisi
tuliyofundishwa na wakoloni na
ambayo ndiyo yaliyokuwa msingi
wa ukoloni wenyewe. Ilikuwa ni
kutokana na wakoloni ndiko
tulikopata mawazo ya kwamba
njia ya kujipatia starehe na mali
ambayo kila mtu anataka ni
uchoyo na tamaa ya ubinafsi. Na
ni kweli kwamba kwa utaratibu
wa kibepari na kikabaila
inawezekana sana kwa watu
wachache kujipatia mali nyingi
nyingi na starehe kubwa ajabu.
Hata katika nchi maskini kama
yetu inawezekana, kama wote
tuonavyo, kwa watu wachache
kuwa na mali nyingi nyingi tena
hasa wakiwa wengi wao ni
viongozi serikalini, ingawa hali za
wengine ni za chini kuliko
zinavyostahili kuwa.
 
Back
Top Bottom