Maajabu haya Wasabato Wenye Imani Kali

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Nimesikiliza kwa makini Wapo FM ikiwahoji waumini wa Kanisa la Waadventist wa Sabato ambao kwa maelezo yao wamesafiri toka sehemu mbali mbali nchini kuja Dar es Salaam kwa lengo la kusafiri kwenda nchi za Ulaya, Arabuni na Afrika kuhubiri. Cha ajabu wapo hapa Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar wakisubiri kusafiri kwenda Iran, Iraq, Cameroun, Ufaransa na nchi nyingine LAKINI BILA PASSPORT WALA VISA.
 
Last edited:
Bubu, asante kwa habari hii! Nataka u flshaback na uone kuwa hata mitume wa zamani hawakuwa na hizo passport, visa na hata pesa. Mitume wa sasa hawana tofauti yoyote na wale wa zamani! Tatizo ni kuwa, watu hawana imani kabisa hasa mambo makuu yasiyo ya kawaida yanavyojitokeza. We subiri na utaona wakiondoka na injili itahubiriwa kama wanavyosema.
 
Yaani hata me nimewaona jana kwenye taarifa ya habari jinsi wanavyoongelea hiyo safari yao. lakini mkumbuke kuwa hao ndo wale kipindi cha pasaka walienda msituni huko mbeya wakisema kuwa wanamsubiri mungu huko msituni. Haya mambo ya imani ni balaa kweli.
 
Hawa nadhani wangetafuta Jina lingine la Dini yao kuliko kutumia jina la Wasabato na kuendelea kulichafua. Nawaona hawa jamaa wamechanganyikiwa na kukosa mwelekeo toka kule Porini na hadi haya maajabu wanayoyafanya sasa pale airport. Tuwaombee kwa mwenyezi Mungu matatizo yao yaishe. Hii sio Imani ni matatizo ya akili na nguvu za giza au Ibilisi. Hata kama itakuwaje hauwezi kusafiri bila Passport na Visa.
 
Mungu Anaweza Kuwasaidia Wapate Passport Visa Na Nauli Kupitia Maombi Yao Ya Dhati Lakini Sio Kusafiri Bila Hizo Nyaraka

Kudhani hivyo ni upungufu unaobebwa na imani kali. Kwa nini wasingejiandaa kabla. Hawaoni hata wenzao waislam wanajiandaa japo hukesha uwanja wa ndege? hebu warudishe ujinga huko walikotoka ebo.
 
Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa wachungaji na wote wenye mamlaka kanisani kusisitiza somo la "Common Sense Christian Living" kwa sababu Mungu wetu tunayemuamini ni Mungu wa mipangilio na anaheshimu mamlaka na taratibu za nchi, kwani hata Bwana Yesu alilipa kodi kwa Pilato na kuwaamuru wanafunzi wake kuheshimu mamlaka kwani zote zinatoka kwa Mungu. Tunahitaji kuwa na imani kama wakristo, yet tunahitaji kubalance maisha yetu na reality kwani bado hatujafika mbinguni, bado tuko kwenye dunia inayoongozwa kwa taratibu.
 
Bubu, asante kwa habari hii! Nataka u flshaback na uone kuwa hata mitume wa zamani hawakuwa na hizo passport, visa na hata pesa. Mitume wa sasa hawana tofauti yoyote na wale wa zamani! Tatizo ni kuwa, watu hawana imani kabisa hasa mambo makuu yasiyo ya kawaida yanavyojitokeza. We subiri na utaona wakiondoka na injili itahubiriwa kama wanavyosema.

Hawa wana matatizo ya akili,wakapimwe ubongo wao au wapelekwe hospitali ya Milembe Dodoma,hiyo ni imani mfu na potofu,nawalinganisha na waumini wa kanisa la children of God la UK,ambao miaka ya 90 walitumia maandiko ya Mwenyezi vibaya,Mungu aliposema tupendane sisi kwa sisi basi wakatafunana bila kujali mke wa mtu au mme wa mtu.Ndipo mama fulani alizaa watoto zaidi ya 7 ambapo kila mtoto alikuwa na baba yake.
 
Mitume walieneza neno la Mungu kwa kutembea kwa miguu, tena wakati huo sehemu kubwa waliyo pita ilikuwa mapori na jangwa.
Sasa kwani kwenda Iraq lazima Ndege? wakitumia miguu si itakuwa safi maana kabla ya kufika Iraq huko wanapopita wengi watanufaika na kupata ujumbe?
 
wakati wa mitume wa zamani hapakuwa na ndege, wala mambo ya passport, lakini ukweli wa sasa ni lazima wawe na visa. Ningewaelewa kama wangekuwa kwenye balozi za nchi wanazotaka kwenda wakiomba Mungu awatendee miujiza ya kupata visa, halafu wangekuwa milangoni mwa matajiri Mungu awatendee miujiza ya kupata ticket za ndege. Mungu kamwe hawezi kuteremsha visa na ticket, anafanya kazi kupitia watu.

Nataka niwaambie wana jamii forums kuwa watu hao hawawakilishi Wasabato, ni kundi la watu tu walichanganyikiwa, Wasabato wa kweli ni watu makini. Tunao wainjilisti wasabato wanaozunguka dunia nzima wakihubiri injili lakini kamwe hawaendi bila visa.
 
Hapo nakuunga mkono, nami nasema hao sio Waadventista Wasabato, nadhani ni watu ambao ama waliasi kanisa lao la awali na kuanzisha kanisa lao au kikundi ambalo hata hivyo halijasajiliwa. Kama alivyosema Mavanza hapo juu Waadventista wa kweli ni watu makini sana na wenye mipango ya kueleweka. Waadventista husafiri sana dunia nzima kwa vikundi au mtu mmoja mmoja na kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi. Naamini katika nguvu ya maombi kufanikisha mipango kadha wa kadha inayofanyika. Lakini hao wanaotaka kusafiri bila visa, tusubiri tuone. Sikatai Mungu hutenda miujiza kwa kila mtu maana binadamu wote tu watu wake na Mungu hana ubaguzi. Let wait and see.
 
Mitume walieneza neno la Mungu kwa kutembea kwa miguu, tena wakati huo sehemu kubwa waliyo pita ilikuwa mapori na jangwa.
Sasa kwani kwenda Iraq lazima Ndege? wakitumia miguu si itakuwa safi maana kabla ya kufika Iraq huko wanapopita wengi watanufaika na kupata ujumbe?
Ni kweli na kama walikwenda kwa miguu hawa sasa wanafanya nini huko Uwanja wa ndege wa JK?
 
sasa hawa jamaa wanakula nini,na wanalala wapi? ni ndege ya nani watakayopanda? wakifika kule watakuwa na mtafisiri au watakuwa wenyewe tu. au wanaweza kuongea kiarabu kiiraki na kifaransa nk. walishawahi kufungwa lakini kwa kwenda bila utaratibu? wanalala wapi na wanatumia choo ya nani? wanaoga? wanapiga mswaki? maisha yao kama ya aina hii wanaendeshaje? hela wamepata wapi? au wana mashetani yatakayo wachukua kimiujiza wakapaa hewani hadi iraq?hahaha. mi sijawahi kuona. nyie mtaona, sio mda mtasikia wanaomba chakula wenyewe na wakizidi, polisi watawashika wawapeleke kwa daktari wachunguzwe akili kama wako sound. hahaha.
 
Polisi wawapeleke Milembe Dodoma au ile wodi ya vichaa pale muhimbili mapema ili wapewe vidonge vya kutuliza akili maana kichaa chao kitazidi na wataanza kuumiza wengine.Kwa nini huyo Mungu asiwaletee ndege huko huko walikokuwa ili wasisumbuke kusubiri hapo uwanja wa JK?Imani zingine zinatia kichefuchefu kweli.

Kwenye miaka ya 80 nyerere alifuta kidhehebu kimoja kilikuwa kule Mbeya,walikuwa hawalimi wakati wa mavuno wanasubiri kuvuna mashamba ya watu eti Mungu alisema atawalisha kama vile ndege wa angani.Upuuuzi kabisa huu.

Hivi hili dhehebu la Wasabato masalia liimesajiliwa kwa katibu wa Wizara ya mambo ya ndani?
 
yani hawa wafanyiwe utaaratibu haraka kama waliweza kuishi porini wakimsubiri Mungu basi watafanya mambo ya ajabu sana hapo air port, waondolewe kwani ni dhahiri hazijatimia vichwani mwao mapepo yamewazidi kupita kiasi hawa ndio wanasababisha air port kunakua na harufu mbaya, lazima hawaogi,kupiga mswaki haja sijui wanatolea wapi jamani hizi dini sasa zitatupeleka pabaya.
 
Bubu, asante kwa habari hii! Nataka u flshaback na uone kuwa hata mitume wa zamani hawakuwa na hizo passport, visa na hata pesa. Mitume wa sasa hawana tofauti yoyote na wale wa zamani! Tatizo ni kuwa, watu hawana imani kabisa hasa mambo makuu yasiyo ya kawaida yanavyojitokeza. We subiri na utaona wakiondoka na injili itahubiriwa kama wanavyosema.

Kwa maisha ya sasa na Ufisadi huu, Hapendwi Mtu linapendwa Pochi Mzazi
 
Hawa watu wanaletea Ukristo aibu KUBWA.... ni vile tu siwezi kukana ukristo wangu, ningeweza ningekana kabisa. Ni UPUMBAVU kumchezea Mungu eti mtasafiri na Biblia ndo itakuwa passport!!!
Tusimchezee Mungu jamani!!
 
Nadhani hao watu hawakuwa na hio safari, they are just doing that to get some misaada, or else they are running mad.
 
Bubu, asante kwa habari hii! Nataka u flshaback na uone kuwa hata mitume wa zamani hawakuwa na hizo passport, visa na hata pesa. Mitume wa sasa hawana tofauti yoyote na wale wa zamani! Tatizo ni kuwa, watu hawana imani kabisa hasa mambo makuu yasiyo ya kawaida yanavyojitokeza. We subiri na utaona wakiondoka na injili itahubiriwa kama wanavyosema.

Mkuu
hapa natofautiana na wewe! Imani ya kupeleka injili katika mataifa sipingani nayo ila napingana na suala la watu kuona kwamba njia yao halali ni kubatilisha utaratibu ambao umewekwa na mamlaka zote za kiuongozi hapa duniani! Hawa wainjilisti wanastahili kufuata taratibu zote ili hata kama wataenda ktk hizo nchi basi wapokelewe na wapewe nafasi ya kuhubiri, otherwise wataonekana kama wale watu wanaofanya mahubiri ktk vituo vya daladala huku wakivizia sadaka kutoka kwa wasafiri!!!

Nisingependa kuliona hili jambo likiachiwa liendelee maana linaweza kuleta dhana potofu kwa jamii. Mimi ni mkristu na pia ni Msabato ila ktk hili naupinga msimamo wa hawa jamaa!!
 
Nadhani hao watu hawakuwa na hio safari, they are just doing that to get some misaada, or else they are running mad.

Lorain, I admit. they hunting for something, vinginevyo nashawishika kuamini kuwa hazijatimia vichwani mwao au la zimelegea. Hapa kuna watu wengi wanahitaji injili, iweje waende ughaibuni wakati hapa hawajafanya kazi.

Any way Kichaa huingia taratibu then kinakomaa. Ni suala la kusubiri na kuona lakini cha msingi ni kuwawahisha Milembe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom