Maajabu: Familia ya weusi yapata mtoto mzungu!

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,167
2uyk2g1.jpg

2u90tx5.jpg



Wazazi weusi wanaoishi London wamebahatika kupata mtoto mweupe kama inavyo onekana kwenye picha.

Kikikutokea kitu kama hichi kule Uswazi-lazima uwe hasusa ya pombe- utakubali ni Miracle au utakimbilia kwa Mkemia Mkuu?

Habari zaidi unaweza kupata kwenye hii link:Black parents give birth to white baby | The Sun |News
 
:A S 465:Uswazi kwetu tena huku kijijini isingeeleweka hata kwa dawa na mafundisho mbadala !!! weee vumbi lingeruka!!!! But that luk OK for me as I can understand that.
 
Duh nimekubali

Hapa uswazi cha kwanza ni mateke rudi kwenu kisha kesi baadae. Wamefanya uungwana sana kuonyesha upendo na kuthibitisha kuwa mtoto wao ana afya njema kabisa.

DNA test za macho huku uswazi ni nyingi mno. Ukishaoa huwa wanasubiri kuona mkeo atapata mtoto? Ukichelewa, maswali yanaanza, wapambe wataanza kukejeli au kupendekeza mwende kwa sangoma. Mke akipata ujauzito wanasubiri kuona ni jinsi ipi, kisha anafanana na nani. Yaani ni mchanganyiko kwelikweli. Hii yote ni mdororo wa hadhi na ubora wa elimu katika mfumo tulionao

Mamlaka tulizonazo zitusaidie kubadili mitazamo yetu iendane na hali halisi ya maendeleo ya fursa zinazoendelea kuwekezwa Tanzania, mfano: kipimo cha DNA kisaidie kupunguza migogoro na kuhimiza uaminifu katika mahusiano
 
Mzungu huyooo au albino?mbona mimi namuona kama ni albino?

Yawezekana mtoto amezaliwa akiwa mgonjwa wa Vintiligo, though ni ugonjwa unaowapata watu wakiwa wamekwisha zaliwa. Ni ugongwa wa kubabuka babuka ngozi na huanzia mara nyingi vidoleni. Inasemekana Michael Jackson alipopata ugonjwa huu aliamua kujicream mwili wote asionekane na mabaka hasa mikononi ambako huanzia mara nyingi.
 
Jamani,

Ukweli utabaki pale pale,Hii ndoa inawalakini na mwanamke kweli hakuwa mwaminifu,haiwezekani mweusi kwa mweusi akatokea mzungu,"biological proved wrong"tuwe makini na wake zetu.

Na hao madaktari wanaongopea umma na labda karushwa kadogo kamatumika kumlaghai jamaa

Asante

Elisante Yona
 
Jamani,

Ukweli utabaki pale pale,Hii ndoa inawalakini na mwanamke kweli hakuwa mwaminifu,haiwezekani mweusi kwa mweusi akatokea mzungu,"biological proved wrong"tuwe makini na wake zetu.

Na hao madaktari wanaongopea umma na labda karushwa kadogo kamatumika kumlaghai jamaa



Asante

Elisante Yona

madaktari wa ughaibuni hawapokei rushwa.
 
How is that possible?....lazima demu aligawa kwa mtasha tu.......!

Hata kama angegawa kwa Mtasha basi asilimia kubwal mtoto angekuwa kachanganya na sio pure blonde blue eyes manywele dhahabu kama huyu kama alivyosema jamaa : Ben also stressed: "My wife is true to me. Even if she hadn't been, the baby still wouldn't look like that"
Vile vile kuna mabingwa wa genetics ambao wamethibitisha huyo mtoto ni mzungu na sio mix race ama albino na ni wa huyu dada, sidhani kama hawa mabingwa wanakurupuka tu lazima wameshafanya maternity test na kuthibitisha na hata ukimuangalia huyu mtoto features zake pua, mdomo nk ni kafanana na mama yake, vilevile wakati wa kujifungua hospitali kunakuwa na wakunga ambao wanampokea kiumbe anapotoka shimoni kwa mama, kwa hio walimuona kabisa akitoka mzungu.
It still puzzle me how? But I have ruled out any involvement of Smith " the milk-man" and joe the "post-man" Labda mama alipandikizwa Embryo (Surrogacy as gestational carrier) kinyemela.
Vilevile inawezekana huyu mtoto atabadilika ngozi na nywele kadiri anavyokuwa, binafsi mwanangu alizaliwa Mdosi kabisa! lakini alibadilika kuanzia miezi 3.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom