Maafisa wa serikali wakiri kukosea agizo la Rais

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::10/14/2007
Maafisa wa serikali wakiri kukosea agizo la Rais
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MAAFISA wa Serikali wamekiri kuwa waliokosea kuandika barua ya kumfukuza kazi aliyekuwa Mhasibu wa Wiazra ya Elimu, Paul Mhamba, tofauti na ushauri wa Rais Jakaya Kikwete kwamba aachinchwe kazi.

Hilo limebainika hivi karibuni, kufuatia Ikulu kuandika barua nyingine kwenda Wizara ya Elimu ikieleza kukosewa kwa agizo la awali la Rais Kikwete.

Kwa muda wa miezi miwili sasa gazeti hili limekuwa likiandika habari hiyo ambayo awali ilibainika kuwa Rais Kikwete alipotoshwa muda mfupi baada ya kuingia madarakani hadi akaidhinisha uamuzi ambao hakuufanyia utafiti wa kina.

Kufuatia uamuzi huo, mlalamikaji alimfikisha rais mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutumia madaraka vibaya kuamuru kuwa afukuzwe kazi.

Baada ya gazeti hili kufanya uchunguzi Ikulu ilianza kufuatilia na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Hamis Dihenga, naye aliamua kulifuatilia suala hilo ambalo lilitokea kabla ya kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.

Taarifa ambazo gazeti hili ilizipata mwishoni mwa wiki na kuthibitishwa na Dk Dihenga, zimesema kwamba kulikuwa na makosa ya uchapaji katika barua hiyo ya agizo la Rais.

Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka serikalini, baadhi ya maafisa wa Ikulu ambao wanadaiwa pia kumpotosha Rais Kikwete hadi kuamua kuchukua uamuzi huo, ndiyo waliochapa vibaya barua hiyo.

"Baadhi ya maafisa wa Ikulu walioshirikiana na baadhi ya maafisa wa wizara ya Elimu, ndiyo waliompotosha Rais na kumfanya aidhinishe kuachishwa kazi kwa Mhumba, lakini tena wakapotosha kuandika barua ya kumfukuza kazi," alisema.

Akizungumzia zaidi sakata hilo, Dk Dihenga alisema kwanza hilo lilikuwa ni jambo la bahati mbaya na si uzembe hivyo Mhumba atalipwa haki zake zote kama mtu aliyeachishwa kazi si kufukuzwa.

"Hili suala lilikuwa ni bahati mbaya, watu walikata rufaa kwa rais, na yeye akakubali kuwa Mhumba aachishwe kazi lakini kulitokea makosa kidogo ya kibinadamu katika kuchapa agizo hilo la rais," alifafanua Dk Dihenga.

Alipoulizwa Mhumba kwa njia ya simu kutoka Mkoani Kilimanjaro ambako anaishi, alisema hadi sasa hajajua sababu hata ya kuachishwa kazi na kusema kuwa bado haridhiki na uamuzi huo na kwamba ni vema astaafishwe kulikuo kuachishwa.

Mhumba alisema ameitumikia serikali kwa miaka 34, hivyo hakubaliani na hatua ya kumwachisha kazi kutokana na kutetea maslahi ya taifa kwa kuibua tuhuma za wizi wa zaidi ya sh 3.5 bilioni kama mishara hewa wizara ya Elimu.

Katika majibu ya maandishi ya hivi karibuni, wizara ya Elimu ilisema Mhumba aliachishwa kwa kukosa sifa pasipo kufafanua, lakini mwenyewe anapinga akisema ni baadhi ya vigogo waliopita walitaka afukuzwe ili kuziba tuhuma za wizi huo wa sh 3.5 bilioni ambazo ni fedha za walipa kodi.
 
Sasa hao waliomdanganya rais amewafanya nini?

PCCB wako wapi kwenda kumwona huyu mzee ili hao waliochota mabilioni wakamatwe?

Kama JK amegundua kulikuwa na kosa basi amrudishe huyu mzee kazini.

Inasikitisha sana, wewe unatetea maslahi ya taifa na ndio unaishiwa kufukuzwa kazi?
 
Hii nchi bwana, wanyonge wana tabu! kwani tunawafundisha nini watoto wetu? kuwa wale wanaofata na kutetea maslahi ya uma ndo waadhibiuwe na wezi wanaendelea kupeta tu. Huyo JK angekuwa anachukua hatua kama hizo fasta kwa mawaziri wake wanaostaafu ingekuwa great, but why wanyonge ndo wanapata tabu
 
"Baadhi ya maafisa wa Ikulu walioshirikiana na baadhi ya maafisa wa wizara ya Elimu, ndiyo waliompotosha Rais na kumfanya aidhinishe kuachishwa kazi kwa Mhumba, lakini tena wakapotosha kuandika barua ya kumfukuza kazi," alisema.

kama wanajulikana kwa nini hawakuchukuliwa hatua? au ndio wapo kwenye mtandao?

"Hili suala lilikuwa ni bahati mbaya, watu walikata rufaa kwa rais, na yeye akakubali kuwa Mhumba aachishwe kazi lakini kulitokea makosa kidogo ya kibinadamu katika kuchapa agizo hilo la rais," alifafanua Dk Dihenga.

Hii si kweli, barua ilichapwa kwa madhumuni husika. Ni kweli asikubali yaishe hivhivi kwa kulitumikia taifa kwa miaka 34, then unaambiwa huna sifa.
Inasikitisha sana, na inaumiza.
 
Sasa hao waliomdanganya rais amewafanya nini?

PCCB wako wapi kwenda kumwona huyu mzee ili hao waliochota mabilioni wakamatwe?

Kama JK amegundua kulikuwa na kosa basi amrudishe huyu mzee kazini.

Inasikitisha sana, wewe unatetea maslahi ya taifa na ndio unaishiwa kufukuzwa kazi?

Ndo style raisi wetu aliyoamua kutumia. Maagizo yake mengi hayana utekelezaji. Inakuwa story tu, watendaji wanasema hayafanyiki na ndo maana hata sera yao wanasema haitekelezeki. Uliza ahadi aliyotoa ya Kusomesha wanafunzi wa Ualimu na udaktari katika vyuo vikuu bila wao kuchangia kama wengine iliishia wapi! Hadithi tu.
 
Mhumba alisema ameitumikia serikali kwa miaka 34, hivyo hakubaliani na hatua ya kumwachisha kazi kutokana na kutetea maslahi ya taifa kwa kuibua tuhuma za wizi wa zaidi ya sh 3.5 bilioni kama mishara hewa wizara ya Elimu.

Pole sana ndugu Mhumba kwa kutolewa kafara, kisa? Umetetea Utanzania wako na kwenda kinyuma na matakwa ya wakubwa. Haiwezekani mtu aliyeitumikia serikali kwa miaka 34 akaonekana mbovu leo hii. Lakini usihofu, Mungu atakuwa upande wako.
 
Sasa hao waliomdanganya rais amewafanya nini?

PCCB wako wapi kwenda kumwona huyu mzee ili hao waliochota mabilioni wakamatwe?

Kama JK amegundua kulikuwa na kosa basi amrudishe huyu mzee kazini.

Inasikitisha sana, wewe unatetea maslahi ya taifa na ndio unaishiwa kufukuzwa kazi?

Very true....Nini Tofauti ya "kufukuzwa" na "kuachishwa" kazi?
 
Back
Top Bottom