Maafa usafiri wa Noah

ms mjini kwenda rombo kama we unajua kuendesha unafika huku mguu unauma kwa kushika break jinsi noa zinavyokimbizwa.
wanasemaga ajali haina kinga lakini mi pale mbele kukaa ni marufuku unakuta dereva anaendesha mkono mmoja uko nje umeshika sigara kama ukiwa dereva ndo kabisa unatamani umshushe uendeshe wewe
 
Korogwe kwenda Handeni na yenyewe yameshika kasi lakini yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la usafiri kutoka Tanga hadi Handeni. Watu wanapanda coaster hadi korogwe halafu wanaingia kwenye Noah hadi Handeni.
 
Acha kulalamikia vitu vya kijinga kama umeona taabu kupanda Noah si ununue gari yako?

We kiazi kweli ishu hii ya msingi unaleta mambo ya kunya hApa kwanza hazilipi ushuru yaani kuna kitu kinakingiwa na kifua au mraDi wa wakubwa huu!
 
Huku kwetu mbona ndo kwenyewe kabisa!!watu tunakimbilia kupanda maana ukiondoka ni moja kwa moja mpaka home!!!huko wapi we unashangaa huu usafiri wa haraka!!!ila hapo kujaza abiria sijui!!najua inabeba watu8 tu
 
Hv kinachosubiriwa ni ajali ili iundwe tume na litolewe tamko la kupiga marufuku usafiri huu wa abiria ni wapi kilitolewa kibali gari hizi zibebe abiria!!leo nimeahirisha safari baada ya kukosa bus nikapelekwa kwenye noah yaani kilichonitisha abiria wamepangwa kama nyanya dereva kabwamdogo kako bwaksi nikajiuliza nawahi wapi bora nibaki tu maafa makubwa yaja ktk usafiRi huu wa NOAH!!

Wapi huko?
 
vipi mbona kila kitu malalamiko au wewe ni mmiliki wa hiace, noah zimepunguza ulaji nini???
 
tatizo wanajaza sana watu na wanaendesha kwa fujo sana na nivijana wadogo mno sizani hata leseni wanazo ila ukiboreshwa na kusimamiwa ipasavyo umeondoa kweli tatizo la usafiri
 
ishu ni kwamba hizi noah zinamilikiwa na matrafic,kwa mfano asilimia kubwa za noah za rombo zinamilikiwa na matrafic xo hata zikifanya makosa hazikamatwi....da kwa hali hii kwel tanzania tutafika?
 
Mwana uko rombo nini? maana huo ndo usafiri wetu 2 and 4rm moshi.
...Hata huku kwetu kuanzia Kahama, Masumbwe, Runzewe Ushirombo kuelekea Benaco - Rusumo border Noah zinatambaa kama mvua na wasukuma walivyo ma-zero ukileta Hiace hapandi wanataka Noah...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom