Maadili

Kipis

JF-Expert Member
Jul 23, 2011
492
61
Swala la maadili limekuwa tatizo sugu sana katika jamii ya kitanzania,licha ya taasisi mbalimbli za dini na zisizokuwa hizo kulikemea.

kwa watu muishio Dar es salaam hili litakuwa si jambo geni machoni mwenu. Wakati fulani serikali ilishalitolea tamko jambo hili lakini nadhani wanaohusika walilifumbia macho.

ni kawaida unapopita baadhi ya mitaa fulani ya jiji hili hasa kwa maeneo ya kariakoo,kukutana na meza za wauza magazeti zikiwa zimeambatanishwa na vijarida vyenye picha za mahaba na mambo ya kikubwa.

ukiachilia mbali wauza magazeti, pia wapo wauza "CD" za picha mbali mbali na nyingi katika hizo,naweza kusema zina vishawishi au vichocheo vya ngono kwa watu wenye kuona zikiwa pale mezani.

wana jamii! Inakuwaje serikali inavipa mwanya vitu kama hivi na kuchangia kwa kiasi kikubwa kubomoa maadili katika jamii tulionayo? wengi wa waathirika wa vitu kama hivi ni watoto wetu ambao kwa kiasi kikubwa tu tunajitahidi kuwajenga kimaadili wanapokuwa nyumbani,shuleni,makanisani na misikitini.

kutokana na sheria na taratibu za jf,sitoweza kuzianika baadhi ya hivyo vijarida na CD ambazo zina picha za utupu. Nadhani wapo walioziona pale mitaa ya Congo karibu kabisa na Vodashop. Nawasilisha..
 
pia kitu kingine ambacho hata mimi huwa najiuliza ni vile vibanda vya kuonyesha sinema uswahilini.
kuna mtaa upo manzese una vibanda viingi vya hizo sinema, sasa ukisoma matangazo waliyo bandika
ya majina ya hizo sinema hata hayaeleweki, nakumbuka moja ilisema MTI MKAVU. na watoto wanaingia kama kawaida
na wanaonyesha hadi usiku. huwa najiuliza mitaa ile ina wajumbe na wenyeviti wa mtaa?
 
Back
Top Bottom