Maadili Campaign

C.K

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
394
162
...ni dhahili kwamba nchi za Afrika na hasa Tanzania zinaendelea kuwa nyuma kimaendeleo ya kiuchumi kutokana na uongozi mbaya/mbovu. Hii imepelekea rushwa, ufisadi na uwajibikaji duni kutawala miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma. Kila mtu (viongozi na watumishi wa umma) wanashughulika kwa maslahi binafsi. Hakuna utaifa tena. Hakuna uzalendo. Kila mtu kivyake... Nchi itaishia wapi?!! Nini hatma ya nchi yetu - hasa kiuchumi???. Jamani, tufanye nini au tuache tu hivihivi?!!!

Martin Luther King, Jr anasema "... kama tunahitaji kusonga mbele, ni lazima turudi nyuma kuchunguza mambo ya thamani tuliyoyaacha – ambayo kwa hakika yamesitirika katika misingi ya Maadili".

Hiyo ni kweli kabisa kwani Tanzania bila kurejea misingi ya maadili - ya kiutendaji hatutaweza kusonga mbele.

Shirika lisilo la kiserikali la Save the Society (StS) kwa kulitambua hilo limezindua kampeni ya kuhamasisha uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi na watumishi wa umma. Lengo ni kuinua ufanisi wa taasisi za umma na hatimae kukua kwa uchumi wa nchi. Pamoja na njia nyingine za kupeleka ujumbe huo kwa wahusika, shirika linatumia sticker zenye ujumbe unaosomeka;

Uwajibikaji + Uadilifu = Ufanisi wa Taasisi
Ufanisi wa Taasisi = Kukua kwa Uchumi wa Nchi.
Sisitiza Uwajibikaji
Sisitiza Uadilifu

(ANGALIA KIAMBATANISHO KWA UJUMBE NA PICHA KAMILI)

Tunalenga Kuifikia nchi nzima kwani mradi huu ni endelevu na ni kwa nchi nzima. Kwa sasa tumeanzia mkoa wa Dar es Salaam. Ukiwa kama mzalendo tunaomba utuunge mkono hasa kwa kutupatia connection na partners/donors wanaofadhili miradi ya aina hii. Hadi sasa shirika linajifadhili lenyewe. Hivyo mchango wako ni wa muhimu ili tutimize adhma yetu ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

wasiliana nasi: info@savethesociety.or.tz, 0789 333088
 

Attachments

  • Maadili - Campaign 2 - with sponsors.PP.pdf
    180.2 KB · Views: 39
Back
Top Bottom