Tuko katika maadhimisho ya wiki ya maji, lakini watu wengi bado hawapati maji safi na salama. Haya ni maji kwa matumizi ya nyumbani kama kunywa, kupikia nk....
mkuu mende0 watawala wangejua ulipo ungeishi kwa shida, na laiti kama wananchi wengi wangebahatika kuona hii walahi kile chama chenye mrengo wa kushoto kingekamata hii nchi, mark my words. anyway inasikitisha sana mkuu. eep:
Picha nyingine wandugu zinasikitisha
Maji hayo hata kuyaweka tuu mdomoni hayafai ila huko vijijini ndio ya kupikia na kunywa kwa wazazi wetu
Ni aibu miaka hamsini ya uhuru tunashindwa hata kuchimba visima vya maji na kuwawekea wananchi hata pump za kutumia solar angalau wawe na maji ya uhakika
Maji kama hayo hayafai kw amatumizi ya binadam ila ndio kimbilio la wananchi wengi huko vijijini
Tuna waziri wa maji ambaye nafikiri wajibu wake umebaki kuhakikisha kuwa wakazi wa dar tuu ndio wana shida ya maji wala hajui huko vijijini au miji mingine hata tone la maji hawalioni na wanakunywa maji ya madimbwi au mvua ikinyesha ndio suluhisho kwa yale maji yaliyosimama barabarani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.