Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yatumike kwa tafakuri badala ya kusheherekea

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Tangu nchi yetu ipate uhuru takribani miaka 50 iliyopita, imepata mafanikio mengi ya kujivunia. Pengine makubwa kuliko yote ni; amani, utulivu, na mshikamano wa wananchi bila yakujali rangi, kabila na dini. Tunu hizo zilijengwa kwa umahili mkubwa wakati wa awamu ya kwanza ya uongozi. Hivi sasa kuna kila dalili zinazodhihilisha wazi kwamba tunu hizo zinazidi kupotea hatua kwa hatua; na hivyo bila ya kuchukuliwa tahadhali uenda tukajikuta tunatumbukia kwenye shimo. Ni kutokana na sababu hiyo natoa maoni kwamba, katika kuhadhimisha miaka 50 ya uhuru, badala ya kuteketeza raslimali nyingi kwenye sherehe, ingelikuwa vyema ukaandaliwa utaratibu wa wananchi wenyewe kufanya tathmini ya kina, ili kubaini ni wapi sisi kama taifa tumekwenda kombo, na ni hatua zipi zinahitajika kurekebisha hali hiyo.
 
Mkuu,
Umekumbusha jambo la mbolea. Nimesikitika sn kumsikia JK akitangaza kwmb sherehe za miaka 50 safari hii zitakuwa kubwa sn na maandalizi yake yatakuwa hayana mfano. imenisikitisha sana kwa mkuu huyu kuongelea maandalizi ya vitu badala ya kuifanya kuwa siku maalum ya kujadili kitaifa mustakabali wa nchi.
 
JK = loser

Njia kuu za uchumi anamiliki yeye pamoja na mashoga wenzake kwa hiyo anapanga sherehe ya kujipongeza .... swali ni Je, ataiona hiyo miaka 50?
 
Hiyo miaka hamsini ni ya Tanganyika au Tanzania?

Tanganyika 1960 = 2010
Tanzania 1964 = 2014

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom