Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika Uwanja wa Taifa - Dar es Salaam

Jamani ivi ni kawaida rais kukagua gwaride akiwa na bodyguards pembeni tena ambao hawajavaa kijeshi??[/QUOTE
sio kawaida lakini pia ni kawaida yule jamaa kibonge ambaye hajavaa kijeshi nimemuona anatoa ulinzi tofauti na jukumu lake pale ni lingine
 
Naona hapo mama salma anaimba wimbo wa taifa huku anatingisha tingisha mabega.,sijui kadhan taarab. Huyu mkuu wa kaya ndo swaga zote anazimaliza kwa kugeukageuka anataman apungie watu mikono hku wimbo unaendelea.
 
gwaride la nje ya uwanja linaingia na lile la ndani linatoka. La nje ndilo linaingia na zana za kijeshi
 
jeshi linaonyesha karate na namna ya kutumia mwili katika vita ni onyesho zuri sana na kweli vijana wameiva
 
kweli jeshi limeweza, limethubutu na linasonga mbele mambo makubwa tunayaona kwa mara ya kwanza
 
I love my Tanzania bara a.k.a Tanganyika.Happy B'day My Land,Although you were there before 1961.Geologicaly You older than 50.
 
wanajeshi walikuwa wanapiga ngumi matofari.sasa hivi ni zana za kivita kupita mbele ya mgeni rasimi.mia
 
Pamoja na Kujichekesha chekesha Mweshimiwa El nimemsikitikia kwa jitihada zake za kumpa mkono Jk hakuweza kufanikia kwani Jk alimchunia Live Kitu TBC tizameni TBC marudio hili NAdhani ni Bifu lishaanza tena Bila kificho. Tusubiri tuone Picha litakwendaje.

Na Jeshi letu lishageuka la Kichina na Kung fu za kumwaga huku mtangazaji wa TBC akidanganya eti hizi Mbinu zilitumika kumng'oa Adui Iddi Amini oi
 
wakuu hizi zana za kivita ni za kizamani sana. nilitegemea nione magari kama yale ya gaddaf. ni ya kizamani sana. Mia
 
Miaka 50 ya uhuru kwenye taifa lililojaa umaskini, ufisadi, uchu wa wa madaraka, na ubabe katika uongozi. Sioni hata tunachosherehekea na kutumia gharama kubwa na jasho la wananchi maskini ni kitu gani hasa ukizingatia;

1.Hatuna madawa na vifaa mahospitalini
2. Ni madaktari wangapi mwaka huu wako mtaani hawajapata ajira
3. Ni waalimu wangapi wanasumbukia malipo na malimbikizo ya mishahara yao!
4. Angalia gharama za huduma mbalimbali ikiwamo umeme na maji na gharama zingine za maisha zinavyopanda kila kukicha.

Ukiyaona hayo uangalie na upuuzi wa utapanyaji wa rasilimali uliotumika kuandaa maadhimisho haya. Watu wamekuwa wakilipana maelfu ya pesa kuandaa maadhimisho haya kila kukicha wakati wananchi wa hali ya chini wanaumia. Halafu leo uniambie nishabikii Jubilei ya miaka hamsini! Ni UPUUZI MTUPU!
 
Back
Top Bottom