Maadhimisho ya miaka 35 ya CCM live Star tv

Pamoja na ukata mkali lakini bado kuna "nyomi" CCM .Hapa kweli Dr. Bana anasema magamba hawana mbadala.

download+(40).jpg




download+(41).jpg
 
Huu umati wa watu unanifanya nitamani nilie,kama ikiwa hawa wote wanaiunga mkono CCM au ni wanachama wa CCM...japo najua hapo kuna watu waliotolewa mikoa mingine hasa ya kanda ya ziwa.Lakini pia,hali hii inauzunisha sana wakuu.Kama watu wanakufa kwasababu ya mgomo wa madaktari uliosababishwa na CCM na watu wake bado kuna watu waniunga mkono CCM? Kama mfumuko wa bei sasa ni 20% bado kuna mtu anaiunga mkono CCM? Kama nchi ina ombwe la uongozi na si ajabu kumsikia Spika akiongea tofauti na Raisi kuna watu bado wanaiunga mkono CCM? siamini.Umati huu wa watu unanifanya nitoe machozi.
 
Mambo kama haya ni nadra kuwafikia wananchi, baada ya hapo vinatumwa vidagaa kwenye mambo ya msingi wenyewe wanakula kuku kwa mrija. Ngoja historia iandikwe. Lakini ipo siku moja tutaelewana wote, na kujipanga kwa ajili ya nchi yetu na si chama.
 
mi ningefurahi; kama maadhimisho ya miaka 35 ya CCM yangeazimishiwa kijijini kama kule Kitonto-Kigoma, Vyadigwa-Tanga, Matombo-Morogoro au kule maeneo ya Bujugo-Kagera na siyo Mjini kama hii ya leo.
 
pamoja na ukata mkali lakini bado kuna "nyomi" ccm .hapa kweli dr. Bana anasema magamba hawana mbadala.

download+(40).jpg




download+(41).jpg

hizi picah si za sherehe za CCM 2012 Mwanza! Leteni picha tunazoziona sasa. Watu ni wengi ila wako katikati ya Uwanja na Majukwaa ni meupe. Sidhani kama wakirudi kwenye Majukwaa watajaza. Hata hivyo sio mbaya inapendeza.
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh. Dr. Jakaya Kikwete ndo anaingia na anakagua vikundi vya burudani.
 
sasa ndio najua tatizo letu watanzania ni CCM, ebu fanyeni hesabu, chama kilizaliwa 5/2/1977 leo tare 5/2/2012 ni miaka mingapi? mimi kwa kesabu zangu hii ni miaka 34! sasa wenzetuuu hiiii 35 yatoka wapi????
 
Kwenye tv wanaonekana watu wengi ila hawaonyeshi matumaini wanaonekana kama wanasubiri adhabu hv!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom