Ma-RC, wafanyakazi wa wizara kuwa Dodoma;gharama za nini?!

mwana wa mtu

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
220
53

Wakuu,
E.Wenje(MB.Nyamagana)akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu ameongelea namna aanavyokerwa na hili suala la Wakuu wa Mikoa wakati huu wa kujadili bajeti ya Waziri Mkuu kuwepo Bungeni/Dodoma; na vivyo hivyo kila wizara inapowasilisha bajeti yake wafanyakazi kadhaa wa wizara hiyo wanakuwepo vivyo hivyo. Suala kubwa alilosema ni kuwa hivi kuna ulazima gani wa kuwepo wote hao, na hizo gharama zote, usafiri,Per diem,n.k, zinazotumika ni matumizi mabovu tu;kwani zingeweza kuelekezwa kwingine!

Hoja ya Wenje, kwa mtazamo wangu ina mashiko sana!Ni kweli kwamba kunahitajika wataalamu kuwasaidia mawaziri katika kuandaa makabrasha ya bajeti, kujibu hoja n.k.; lakini kwa hali ya kawaida si kwa kiwango cha idadi hiyo ya wafanyakazi wengi wanaojazana huko Dodoma.Hata hawa wakuu wa Mikoa hivi hasa wanaenda kufanya nini,kuonekana kwamba nao wako chini ya Waziri Mkuu?!!!

Kama ndio hivyo, basi hebu hii serikali irejee adhima yake ya kwenda wote Dodoma (suala ambalo limekuwa kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano).

Kujazana Dodoma si kidhihirisho cha utendaji!
 
Sio kujazana Dodoma tu wakuu wa mikoa na wilaya huwa wana kazi gani haswa? wanachangia nini maendeleo na uchumi wa taifa? wao ni mzigo mkubwa sana kwa taifa ! hawa ndio wanaotumika kukandamiza upinzani na kuandaa mikakati ya kuiba kura wakati wa chaguzi! Mkoa una RAS kuna cjui MADED Kuna wabunge , kuna makatibu tarafa kuna madiwani mlolongo wa viongozi lakini maendeleo yako wapi? katiba mpya ipige fagio la chuma kwa wakuu wa wilaya na mikoa they are burden to our nation!!
 
Back
Top Bottom