Ma CEO wa mashirika ambao wangefaa kuwa Mawaziri

wimbi la mbele

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
647
266
Je Kitilya wa TRA au Kimei wa CRDB au Mchechu wa NHC au Ali Mufuruki au Ami Mpungwe au yule bosi wa PPF wangefaa kuwa mawaziri?

Je wizara zipi zingewafaa?
 
Hao wote uliowataja ni wezi waliokubuhu bahati yao nzuri wanalindwa na wezi wenzao!!
 
Nilizani unaomba ushauri watoswe vip maana kama huyo wa TRA ni kama ana hati miliki pale no wonder mapato mengi ya TRA yanaishia kwa wajanja!
 
Umewaza nini mpaka ukaamua kuwachagua hao? Kwani lazima kila siku hao hao tu? Zipo new blood nyingi tu basi majina hayajulikani.
 
Hakuna hata mmoja anaye weza kuwa waziri kati ya hawa ....

Labda kwenye hii serikali dhaifu ya CCM...chini ya raisi Dhaifu!.. kwani hata wao dhaifu tu..!!

Kimwi wa CRDB ana nini!! cha ajabu ambacho kiko tofauti na Mkama aliekuwa jiji sasa katibu mkuu wa magamba!?

Kitilya...!! anafanya nini TRA!?...

Mchechu!! anaesema zimejengwa nyumba za watanzania wa kipato cha chini zitakazouzwa milioni60!! mzima huyu!

Ami Mpungwe!!!! mesahau ufisadi wake wa SA!!

Kama ni dugu au jamaa zako pole..... hawafai...MASHUDU MATUPU!!


Mie nadhani ungesema watu wa maana kama kina John Mnyika, David Silinde, Said Arfi, S. Kasulamabayi n.k
 
Mufuruki ndiye aliyeihujumu ATCL kwa kushirikiana na South African Airways na ndiko alikopata mtaji wake wakati huo akiwa mwenyekiti wa board!!!
 
huyu MSWAHILI anafaa kama akivaa suti?

IMG_4942.JPG
 
Hao wote hawafai kuwa ma CEO of the company, na hata uwaziri,

Hivi unajua kuongoza kampuni ni kazi kuliko kuongoza wizara?

Na tena kuongoza multination company like toyota, sony, samsung etc ni ngumu zaidi kuliko kuwa rais, as mda wote kichwa lazima kiwe makini as decisions utazofanya zina affect dunia nzima as company like those employs billions of people in the world na kama ziki colapse ni balaa yaani bora nchi ianguke kuliko kampuni.

So tukisema tufate proffessonal ethics kuongoza shirika like nssf, tanesco, tra, and so on ni kazi ngumu kuliko kuongoza wizara na kama kuna smart people mmoja mnatakiwa mfanye choice aende wapi ni bora akaongoze shirika, as kwanza kwenye wizara waziri hana lolote maana mtendaji ni katibu mkuu na mkurugenzi wa wizara..

Nilishawai kuona kwenye tv raisi wa samsung sijui anaitwa kim chung nani alienda usa yaan anaongea hadi kina obama, bill gate na wenzao wanakubali kweli kichwa kinaongea...

Ukitaka kuamini ninachosema ingia wikipedia usome profile za ceo wa those company au wengine wanaitwa key people of the company as wanaongoza department zinazohitaj umakini wa hali ya juu, uone profile zao ndo utajua namaanisha nini na kwa nini wanaitwa key people... So kwa kufata ethics uwaziri ni kazi nyepesi kuliko kuongoza shirika.
 
Dhana potofu, kuwa CEO wa kampuni sio kuwa unasifa ya kuwa mwanasiasa. Maamuzi ya kisiasa ni tofauti na maamuzi ya kampuni. Kwenye kampuni unaangalia bottomline, competitive forces etc. kwenye siasa unangalia zaidi madhara ya maamuzi katika usalama, ulinzi, maendeleo na ustawi wa wananchi. Pili kwanini mtu akifanikiwa kwenye eneo lake tunataka kumfanya awe mwanasiasa? yaani dr bora tunamtaka awe mwanasiasa, mwanamichezo bora tunataka awe mwanasiasa kwanini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom