M4C yavuruga Chato kwa Magufuli. CCM yaambulia vijiji 3 kati ya 11. Bendera na kadi bado kikwazo

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,732
Katika uchaguzi wa uliofanyika Katika kata mbalimbali za Chato, Magamba wamepigwa mweleka na CDM maana hata vijijini CCM haitakiwi.

VIJIJI ILIVYOSHINDA CHADEMA NI:-
1. Mjengo kata ya Mganza
2. Kazunguti Kata ya Nyamilembe
3. Mikonto Kata ya Nyamilembe
4. Izubangabo Kata ya Bwanga.
5. Majengo Kata y aBuziku
6. Kasala Kata ya Makuluguzi
7. Mwenda Kulima kata ya Ipalamasa
8. Nyakakalango kata ya Nyamilembe

CCM ni mkungo kata ya Bukome, Mwabasabi kata ya Ipalamasa, Mnekezi kata ya Ipalamasa

Mchakato wa M4C unaendelea kata hadi kata. Wilaya ya Chato ina kata ishirini na mbili (22) katika hizi tumezunguka kata kumi na nane na kila kata ambazo tumepita ukiitishwa uchaguzi leo kata hizo (CCM) wataambulia moja au hamna bahati nzuri umeshuhudia(Mimi Tamuganyizi nilishuhudia) M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato(CCM) akilalamika mafuriko wanayoyapata na tarehe 1/6/2012 tunaenda kata ya Bwera siku ya ijumaa.

Hii oparesheni bomoa makufuri ni kimbuga cha 2015 kuchukua Halmashauri.

Matokeo ya mIkutano yetu kila tulipopita hakuna mkutano tulipiTa bila kuvua gamba na kuvaa gwanda jumla ya magamba 66 yamevuliwa na kuvaa magwanda na wanachama zaidi wamejiunga na chama cha ukombozi(CHADEMA),

Manyanyaso mpaka sasa tuna kesi mahakamani ya M/Kiti wa kijiji cha minkoto pamoja na wenzake wawili walibambikizwa kesi ya kuchoma moto na kuua ngombe za mtuhumiwa wa ujambazi.

Kijiji anamotoka M/kiti wa halmashauri, na yeye ameshirikiana na polisi kubambikiza kesi ya ujambazi kwa wanachama wetu wawili waliofinikisha tukachukua vitongoji viwili ndani ya kata yake. Bado M/Kiti wetu kijiji cha Kibumba kata ya Makurugusi na
yeye alibambikizwa kesi ya mauaji mpaka sasa yuko mahabusu Bihalamulo.

CHANGAMOTO

Vifaa vya chama kama Bendera, Kadi na Katiba hatuna kabisa lakini tuliadika barua makao makuu pamoja na mkoa tumeelezwa kuwa bado vifaa haijaja kutoka vilipoagizwa.

My Take

Haya ni mahojiano niliyoyafanya na Katibu wa CDM wilaya ya Chato. Jamaa yuko simple ni kijana yuko Stendi pale Chato. Storage ya nyaraka muhimu alizonazo sio nzuri. Binafsi naandaa walau storage ya Hard Copies alizonazo kijana kwa kuanzia na baadaye ufumbuzi kamili. Leo CDM inaharibu kule Kata ya Bwera…nitawapa update.

Kwenye Kibanda cha kazi anapopigia kazi Kamanda huyo ametype na kuprint maandishi yasomayo hivi….." VUA GAMBA VAA GWANDA, VUA UKADA UVAE UKAMANDA"

Katibu huyo anaitwa Mange Sayi Ludongo – Wasiliana naye kwa update zaidi….0752911438

S.L.P 15,
CHATO.
 
Hilo la Bendera na kofia Chama kilifanyie kazi kwa haraka pale Jangwani niliona vijana na watu wazima wakiwauliza wale waliokuwa wamevaa au kushika zile bendera mkononi wawauzie ,walikuwa wnabembeleza kweli nadhani kuna uhaba mkubwa wa vifaa hivyo
 
Yaani watu wanagoma kugombea kwa tiketi ya ccm maana kwa sasa kuwa CCM ndani ya jamii ni sawa na aibu aipatayo mtu anayefumaniwa na mke/mme wa mtu.
 
muganyizi unaweza kubadili heading mwenyewe siyo lazima mods. click edit halafu bonyeza pale chini pameandikwa Go advanced then itakuja page yenye thread nzima pamoja na Title juu yake edit then save mambo yatakuwa pouwa
 
muganyizi unaweza kubadili heading mwenyewe siyo lazima mods. click edit halafu bonyeza pale chini pameandikwa Go advanced then itakuja page yenye thread nzima pamoja na Title juu yake edit then save mambo yatakuwa pouwa

imegoma bana
 
Nauliza, hivi Biharamulo iko Kanda gani wajameni?
Ritz, Ribo et al naomba mnijibu.
 
Kila la heri Makamanda,
Kazi yetu kubwa wengine ni kumwomba Mwenyezi Mungu atangulie katika njia hii ya Ukombozi wa Mtanzania.
 
Back
Top Bottom