M4C yaitesa CCM Geita; Wanachama wake 300 watimkia Chadema

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMAPILI, SEPTEMBA 23, 2012 10:32 NA VICTOR BARIETY, GEITA

*Wanachama wake 300 watimkia Chadema

ZAIDI ya wanachama 308 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Wanachama hao wamejiunga na Chadema kupitia mikutano mbalimbali ya Operesheni Sangara ya chama hicho chini ya kauli mbiu yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Mikutano hiyo inayofanyika katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Geita, inaongozwa na aliyekuwa Diwani wa Sombetini mkoani Arusha kuptia CCM, aliyehamia Chadema, Alphonce Mawazo.

Wanachama hao ambao baadhi yao ni wafuasi wa CUF, wanatoka vijiji vya Bukondo, Kaduda na Katoro, huku kati ya hao, 100 ni wanachama wapya wasiokuwa na vyama.

Wakizungumza na Mtanzania kuhusiana na sababu za kujiunga na Chadema, wanachama hao walisema ni kutokana na Serikali ya CCM kukithiri kwa ufisadi.

Walisema ufisadi na wizi wa fedha za umma umekuwa mkubwa serikalini, hali ambayo imefanya Serikali ishindwe kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kipato cha chini.

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Kadudu, aliamua kujiunga na Chadema pamoja na wake zake wawili, kutokana na kuchoshwa na uonevu aliofanyiwa na Mtendaji wa Kijiji hicho, Fundi Makanza.

Mtendaji huyo anadaiwa kumweka ndani mkazi huyo kwa kosa la kuwaandaa watu kujitokeza katika mkutano wa hadhara uliokuwa uhutubiwe na viongozi wa Chadema.

Alisema ameamua kujiunga Chadema pamoja na wake zake wawili baada ya kuchoshwa na manyanyaso ya mtendaji huyo aliyejigeuza Mungu mtu na kwamba ameigeuza ofisi yake kuwa Mahakama.

"Nashukuru viongozi wa Chadema wamenitoa, kutokana na shukurani hizi nimeamua nihamie Chadema maana pamoja na kuwa kada mzuri wa CCM sioni mabadiliko yoyote zaidi ya manyanyaso ya kila siku tunayofanyiwa na mtendaji.

"Ukifikishwa ofisini kwake ni kama umefikishwa mahakamani, maana yeye huyohuyo ni mtendaji, ni polisi na mahakama, kwa hali hiyo unawezaje kuipenda CCM na kuendelea kubaki huko?"alilalama mwananchi huyo.

 

Vizuri wote sio CCM pia Wapo Wanachama wa CUF...

GEITA ni MKOA Tajiri kwa DHAHABU...
 
Kwa speed hii, Hadi 2015 ccm itabaki nyeupe kabisa. Watakaobakia ni yule sokwe wao, kwani hata mtoto wa sokwe nae ameshaama, na akasema familia nzima, itaama, watamuacha sokwe mzee TU...
 
hali ni mbaya sana kwa CCM hasa ukizingatia mtaji wake mkubwa uko vijijini.....
nachojua kama watu 308 wamevua gwanda basi ujue kuna zaidi ya hapo kwani siasa za vijijini mtu mmoja mwenye influence huwa anabeba vichwa kama 10 hivi nyuma yake..........
 
Back
Top Bottom